Manji: Ujenzi uwanja wa mazoezi kuanza ndani ya siku 90 baada ya ridhaa ya wanachama

Manji: Ujenzi uwanja wa mazoezi kuanza ndani ya siku 90 baada ya ridhaa ya wanachama

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji amedai kuwa ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa timu hiyo utaanza ndani ya siku 90 baada ya kupewa ridhaa na wanachama.

Manji ameyasema hayo leo wakati wakiwahimiza wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili katika Mkutano Mkuu ili kuchangia masuala ya msingi kwa maendeleo ya klabu hiyo.

Amesema katika Mkutano huo atazungumza na baada ya hapo atatoka nje ili kutoa nafasi kwa wajumbe kujadili mambo kwa uhuru na kufanya maamuzi.

Katika mkutano huo, suala kubwa linalotarajiwa kuteka sehemu kubwa ya mkutano huo ni ukodishwaji wa klabu hiyo kwa kampuni ya Yanga Yetu ambao umekuwa ukikosolewa na watu wengi na wadau wakubwa wa soka nchini.

===================
Habari Zaidi
===================
WANACHAMA wa klabu ya Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika Oktoba 23 Makao makuu ya klabu Jangwani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali likiwemo suala la ukodishwaji.

Mwenyekiti wa Klabu hiyo Yusuph Manji amewaambia waandishi wa Habari kuwa mkutano huo utakuwa wa wazi na kila mwanachama atapewa nafasi ya kutoa maoni yake juu ya suala zima la uendeshwaji kwa ajili ya maendeleo ya Yanga.

Manji alisema badala ya wanachama kukimbilia kwenye vyombo vya Habari kuongea kuhusu masuala ya klabu wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo ili kuchangia kwa manufaa ya Yanga.

"Mkutano utakuwa huru na wa haki kila mwanachama ambaye amelipia kadi yake atapewa nafasi ya kutoa duku duku lake kabla ya makubaliano kufikiwa," alisema Manji.

Manji alisema baada ya makubaliano hayo kufanyika Uwanja wa mazoezi utaanza kujengwa ndani ya siku 90 katika eneo la Gezaulole lililopo Kigamboni kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa na kampuni ya Yanga.

Aidha Manji alisema kuhusu suala la kusainiwa kwa mkataba na bodi ya wadhamini dhidi ya kampuni ya Yanga Yetu kila kitu kitajadiliwa kwenye mkutano huo ambapo wanachama wametakiwa kuwahi mapema huku ulinzi ukiwa ni uhakika.
 
Ili kulinda maslahi ya club ni vema Manji aachwe awekeze lakini asiendelee na nafasi yake ya uenyekiti.. Wanachama wote WA yangu tukutane kwenye mkutano mkuu
 
hizi ndizo story za 'mkishinda kila mchezaji milioni mbili' bila kueleza hiyo nguvu ya kushinda wataipata wapi!
Kama kweli una nia ya ushindi si unawapa wachezaji hiyo milioni mbili mwezi mmoja kabla ili wajiandae kushinda!?
Sema tu ufinyu na woga wetu katika kufanya maamuzi lakini hawa jamaa sio wafadhili bali ni wafadhiliwa.
 
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji amedai kuwa ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa timu hiyo utaanza ndani ya siku 90 baada ya kupewa ridhaa na wanachama.

Manji ameyasema hayo leo wakati wakiwahimiza wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili katika Mkutano Mkuu ili kuchangia masuala ya msingi kwa maendeleo ya klabu hiyo.

Amesema katika Mkutano huo atazungumza na baada ya hapo atatoka nje ili kutoa nafasi kwa wajumbe kujadili mambo kwa uhuru na kufanya maamuzi.

Katika mkutano huo, suala kubwa linalotarajiwa kuteka sehemu kubwa ya mkutano huo ni ukodishwaji wa klabu hiyo kwa kampuni ya Yanga Yetu ambao umekuwa ukikosolewa na watu wengi na wadau wakubwa wa soka nchini.
Inamaana miaka 6 wanachama bado walikuwa hawajampa ridhaa ya kuanza ujenzi... dah kweli siasa iko katika kila sehemu.
 
Hata Chief Mangungu wa Msowero aligawa alikumbana NA vishawishi kama hivi miaka hiyo. Mbona siku zote hakuwaza kujenga uwanja?
 
hizi ndizo story za 'mkishinda kila mchezaji milioni mbili' bila kueleza hiyo nguvu ya kushinda wataipata wapi!
Kama kweli una nia ya ushindi si unawapa wachezaji hiyo milioni mbili mwezi mmoja kabla ili wajiandae kushinda!?
Sema tu ufinyu na woga wetu katika kufanya maamuzi lakini hawa jamaa sio wafadhili bali ni wafadhiliwa.
Hilo jambo ndo lipo katika timu ya simba kwa sasa sipati picha mo katika mechi moja asipotoa hela itakuwaje
 
-->>WANA YANGA TUSIREJESHWE NYUMA NA WALAFI WACHACHE WANAOTAKA KUITUMIA CLUB HII KAMA BIASHARA YA KUJIKIMU KIMAISHA.
•manji songa mbele.../
 
Mbagala kuu hatuna hamu nae....maana hata wana ukawa walimpa kura kisa tajiri hana njaa za kupiga vijisenti. Maskini akichaguliwa ni hadi ajitajirishe ndo awasaidie wananchi. Leo hii wanajuta
 
Yanga ni kubwa kuliko manji. Wanayanga tusikubali kudanganyika kwa hadi Kama hizo. Manj.atuachie timu yetu Kama anapenda michezo hasa mpira kuna timu nyingi hapa tz zimekwama kwa kukosa wawekezaji ni bora aende huko.

Kuna wapenzi wa yanga wanao msupport huyo ukiwauliza mafanikio ya manj wanasema kuifunga simba na kuchukua ubingwa kana kwamba yanga haijawahi kuifunga simba wala kuchukua ubingwa.
Lazima wajue lengo kuu la yanga kama klabu ni kutwaa ubingwa na kumfunga mpinzani na inafanya hivyo toka enzi za Abbas gulamal
 
Back
Top Bottom