RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji amedai kuwa ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa timu hiyo utaanza ndani ya siku 90 baada ya kupewa ridhaa na wanachama.
Manji ameyasema hayo leo wakati wakiwahimiza wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili katika Mkutano Mkuu ili kuchangia masuala ya msingi kwa maendeleo ya klabu hiyo.
Amesema katika Mkutano huo atazungumza na baada ya hapo atatoka nje ili kutoa nafasi kwa wajumbe kujadili mambo kwa uhuru na kufanya maamuzi.
Katika mkutano huo, suala kubwa linalotarajiwa kuteka sehemu kubwa ya mkutano huo ni ukodishwaji wa klabu hiyo kwa kampuni ya Yanga Yetu ambao umekuwa ukikosolewa na watu wengi na wadau wakubwa wa soka nchini.
===================
Habari Zaidi
===================
WANACHAMA wa klabu ya Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika Oktoba 23 Makao makuu ya klabu Jangwani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali likiwemo suala la ukodishwaji.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo Yusuph Manji amewaambia waandishi wa Habari kuwa mkutano huo utakuwa wa wazi na kila mwanachama atapewa nafasi ya kutoa maoni yake juu ya suala zima la uendeshwaji kwa ajili ya maendeleo ya Yanga.
Manji alisema badala ya wanachama kukimbilia kwenye vyombo vya Habari kuongea kuhusu masuala ya klabu wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo ili kuchangia kwa manufaa ya Yanga.
"Mkutano utakuwa huru na wa haki kila mwanachama ambaye amelipia kadi yake atapewa nafasi ya kutoa duku duku lake kabla ya makubaliano kufikiwa," alisema Manji.
Manji alisema baada ya makubaliano hayo kufanyika Uwanja wa mazoezi utaanza kujengwa ndani ya siku 90 katika eneo la Gezaulole lililopo Kigamboni kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa na kampuni ya Yanga.
Aidha Manji alisema kuhusu suala la kusainiwa kwa mkataba na bodi ya wadhamini dhidi ya kampuni ya Yanga Yetu kila kitu kitajadiliwa kwenye mkutano huo ambapo wanachama wametakiwa kuwahi mapema huku ulinzi ukiwa ni uhakika.