Acha mawazo ya kidini ndugu yangu, ukifikiria hivo basi unataka hata Rais, waziri, na wengineo wanapoenda ktk mikusanyiko ya dini wasitumie magari ya serikali bali watumie magari binafsi, achana na huo mtazamo sio mzuri. mbona makamu wa rais hutumia magari ya serikali kwa ajili ya kwenda msikitini jioni na ijumaa?
mbona hufikirii gharama anayoitoa huyu ndg Kimei kwa ajili ya kusafirisha hao wafanyakazi bali wewe umeng'anania misa tu? nafikiri toka hapo ulipo and start thinking positively. huoni gharama zinazotumiwa na CRDB kwenye family day kulipia vinywaji vyenye kilivi wewe umeona misa tu? acha hivo ndugu yangu........................
Kati yangu mimi ninayesema dini hairuhusiwi katika kuendesha chombo chenye wateja na wafanyakazi wenye dini tofauti na wengine wasio na dini, na nyie mnaotetea dini moja ku dominate chombo hiki, nani ana mawazo ya kidini?
Mimi siwezi kuwa na mawazo ya kidini kwa sababu siamini dini yoyote.
Nimeongelea gharama, nikaongelea misa. Ili kui account gharama inabidi ujue gharama inakwenda wapi.
Tatizo letu ni kwamba lack of exposure inafanya kitu ambacho primarily kinahusu "corporate governance", na secular ethics mnakiona kama udini.
Alichofanya Kimei hapo, ni kama baba mwenye watoto wawili, kamnunulia kiatu mmoja, halafu mwingine hajamnunulia.
Huyu mtoto asiyenunuliwa kiatu atajionaje?
Hilo moja, pili. Alichofanya Mtei hapo hakina tofauti na kuchukua pesa ya CRDB kujenga kanisa kwa minajili ya kutoa shukurani kwa mungu.
Watu wanaojali haki sawa kwa wote wataonaje? Achilia mbali watu wa dini nyingine, Wakristo wenyewe wako na madhehebu lukuki, Wa-Anglikana, Wa-Lutheri, Wakatoliki, etc sasa hawa nao wakitaka kila dhehebu lifanyiwe hivyo kutabaki benki hapo?