SoC01 Manka binti mrembo, Mzaliwa wa Machame na mkazi wa Tandale alivyobahatika kuacha ukahaba mpaka kuwa dereva Ikulu

SoC01 Manka binti mrembo, Mzaliwa wa Machame na mkazi wa Tandale alivyobahatika kuacha ukahaba mpaka kuwa dereva Ikulu

Stories of Change - 2021 Competition

Amina68

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
298
Reaction score
547
Kwa majina naitwa Manka, Mzaliwa wa Moshi Machame, mkazi wa Tandale Dar es salaam.

Nilifanikiwa kuanza masomo yangu ya msingi Dar, na kufanikiwa kujiunga masomo ya Sekondari shule wanafunzi wenye vipaji maalumu Tabora Girls, ambapo nilisoma mpaka kidato cha nne, na kufanikiwa pia kuendelea na masomo yangu hapo hapo shule ya wasichana Tabora Girls kidato cha sita.

Kiukweli niliishi maisha ya raha sana kutokana na wazazi wangu wote kuwa wafanyakazi mama akiwa mfanyakazi Wizara ya Mambo ya nje na baba akiwa balozi wa Tanzania nchini Australia.

Maisha yalikuja badilika baada ya baba angu mzazi kupata ajali ya gari akitokea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akielekea Machame nyumbani ambapo aligongana uso kwa uso na roli. Baada ya taarifa kufika nyumbani mama nae alipata mshtuko akafariki kwa ugonjwa wa moyo, hivyo nikapoteza baba na mama kwa wakati mmoja. Niliumia sana, na hapo maisha yangu yakaanza kubadilika rasmi.

Baada ya wiki moja ndugu wenye tamaa walikuja nyumbani na kuanza taratibu za kuchukua Mali mpaka nyumba yetu iliuzwa ndani ya miezi mitatu tu, kumbuka wakati huo nilikuwa katika utaratibu wa kujiandaa kwenda chuo kikuu udsm kusomea uhandisi wa Umeme. Niliumia sana,nilifukuzwa pia nyumbani nikawa sina pa kuishi wala pa kula.

Nilianza kuishi mitaani,na Kama unavyojua maisha ya Dar ni magumu sana, ilinilazimu kujiingiza katika maisha ya ukahaba ili tu maisha yaweze kwenda.

Wakati wa ukahaba wangu, nimewahi kukutana na changamoto mbalimbali sana Kama kulala njaa kwa kukosa chakula maana Kuna siku unaweza toka uspate hata mwanaume mmoja, na Kuna baadhi ya siku nilikuwa nasafiri mpaka morogoro msamvu kusaka wateja,maisha yalikuja magumu sana i

Siku moja nikiwa nimekaa zangu, sehemu niliyokuwa nimepangisha Mtoni kijichi,mida ya saa 4 asubuhi Mara ikaja gari moja, ikasimama mbele ya nyumba ile, wakashuka watu wawili wote wanawake wakanifata wakanisalimia na wakaniuliza, samahani wewe ndio manka Anthony Mushi, nikawajibu ndio Mimi.

Wakajitambulisha wametokea ofisi ya Rais utumishi na utawala bora,ninahitajika na bosi wao ofisini nilishtuka sana,na nikawauliza huyo bosi wao ananijua? Wakanijibu wao wamepewa maelekezo ya kunitafuta na ndipo walipojua ninapoishi.

Nilijiandaa nikaondoka zangu,huku nikiwa na mawazo akilini kwangu,je huyu bosi niliwahi kutoka nae? Au Ni mteja wangu? Ila nilipiga moyo konde nikaenda na kusema nitajua huko huko.

Nilifika na kupelekwa moja kwa moja ofisini kwa huyo bosi.baada ya kufika sikumkumbuka ,ila akajitambulisha kuwa yeye Ni katibu ofisi ile iliyopo Mjini Dar es Salaam.aliniuliza maswali mengi sana na mwisho wa siku akaamua kupasua ukweli.

Akanambia kwamba ofisi yake imeanza kunifatilia tangu nilipochaguliwa kidato cha kwanza tabora girls na wamenifatilia nyendo zangu kwa muda wa miaka 9, na ndipo Leo imekuwa tamati na ninatakiwa kujiunga nao ili na Mimi nianze kufatilia watu,sikumuelewa ila nilipiga moyo konde nikasema liwalo na liwe.

Waliniruhusu nirudi nilipopanga nikachukue vitu vyangu vya muhimu nirudi pale,baada ya hapo nilipelekwa kwenye nyumba Safi na siku 3 zijazo nikapelekwa jeshi la kujenga taifa, nikaanza mafunzo na nilipomaliza, nilipangiwa kwenda kozi maalumu kurasini,na baada ya hapo nilipewa first appointment ikulu.

Hivyo napenda kuwaasa ndugu zangu hasa wadada, usikate tamaa, Hujui kusudi la maisha yako hapa duniani.

Thanks
 
Upvote 62
Wazazi wanatakiwa kuweka title deed bank au mahakamani na note za urithi kama lolote litatokea, inauma Sana wazazi wanaondoka watoto wanakuwa chokolaa mtaani. Familia zingine ni balaa sana. Hazina utu, hizo nyumba wangefanya utaratibu kuwapa watoto Mali za wazazi wao.
Ni kweli Kokolo

Thanks kwa kunielewa
 
Ntakuwa nilisha kula kipindi uko girls na msamvu pia.
HADITHI YAKO NIKAMA NAKUFAHAMU VILEEEE,

one day tuta onana, HAO NYOKA NDIO VYAKULA VYANGU.....
 
Huu utungaji wa Shigongo au ni kweli?

Lies hizi

Hivi sijui mtu anaamua kutunga fiction na kupoteza muda wake kuandika vitu virefu ambavyo ni fiction ili imsaidie nini hasa?

Lies plus lies equals to pile of shit!
Thanks,mwenye kuthibitisha hili Ni Mimi tu na sio mwingine,sio unaandika shits pia,

Kama una dukuduku uliza ujibiwe
 
hmmm yaani kwa sasq uko na 29 yrs na form6 ume maliza 2009 aiseeeeeeeeeeeee


tumepigwa hapa wazeeeee
Ulitaka nimalize mwaka gani?

Nimemaliza la Saba Nina miaka 13, nimemaliza F4 Nina miaka 17(kasoro) nimemaliza f6 Nina miaka 20(kasoro)

Wewe ulitaka niwe na miaka mingapi labda?
 
Bora yangu,nimeaamua kutoa story inayonihusu na inaweza insipire vijana wengine wasijate tamaa,

Ila MWIGULU ni tajiri na bado anachukua tozo zetu
 
Dereva wa ikulu unaifukuzia Ml5😁.
Moderator kweli huu uzi ufaa kuwa humu au mmejisahau?
Kumbe hata visa na mikasa vinaruhusiwa humu pia!
Kwani kuna kipengele kinasema story iwe kweli...

Ushaambiwa ni story (kwahio hata kama ni fiction) so long as inaweza kuleta mabadiliko..., nadhani kosa ni kama tu kafanya plagiarism
 
Kwani kuna kipengele kinasema story iwe kweli...

Ushaambiwa ni story (kwahio hata kama ni fiction) so long as inaweza kuleta mabadiliko..., nadhani kosa ni kama tu kafanya plagiarism
Exactly ,thanks Keyser Söze kura yako tafadhali
 
Kiukweli,niliishi maisha ya raha sana kutokana na wazazi wangu wote kuwa wafanyakazi mama akiwa mfanyakazi wizara ya Mambo ya nje na baba akiwa balozi wa Tanzania nchini Australia.

Ndugu yangu huyu ni wakishua aliyepitia mtaa sema inawezekana kutokana na konekisheni ya wazazi ndio maana ameingia kitengo kwa sababu wizara ya mambo ya nje imejaa wanakitengo na inawezekana hata hao wazazi vifo vyao sio kawaida ni kutokana na kazi zao hivyo awe makini inawezekana ameingizwa huko kuna kazi inatakiwa kufanya
 
Back
Top Bottom