SoC01 Manka binti mrembo, Mzaliwa wa Machame na mkazi wa Tandale alivyobahatika kuacha ukahaba mpaka kuwa dereva Ikulu

SoC01 Manka binti mrembo, Mzaliwa wa Machame na mkazi wa Tandale alivyobahatika kuacha ukahaba mpaka kuwa dereva Ikulu

Stories of Change - 2021 Competition

Amina68

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
298
Reaction score
547
Kwa majina naitwa Manka, Mzaliwa wa Moshi Machame, mkazi wa Tandale Dar es salaam.

Nilifanikiwa kuanza masomo yangu ya msingi Dar, na kufanikiwa kujiunga masomo ya Sekondari shule wanafunzi wenye vipaji maalumu Tabora Girls, ambapo nilisoma mpaka kidato cha nne, na kufanikiwa pia kuendelea na masomo yangu hapo hapo shule ya wasichana Tabora Girls kidato cha sita.

Kiukweli niliishi maisha ya raha sana kutokana na wazazi wangu wote kuwa wafanyakazi mama akiwa mfanyakazi Wizara ya Mambo ya nje na baba akiwa balozi wa Tanzania nchini Australia.

Maisha yalikuja badilika baada ya baba angu mzazi kupata ajali ya gari akitokea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akielekea Machame nyumbani ambapo aligongana uso kwa uso na roli. Baada ya taarifa kufika nyumbani mama nae alipata mshtuko akafariki kwa ugonjwa wa moyo, hivyo nikapoteza baba na mama kwa wakati mmoja. Niliumia sana, na hapo maisha yangu yakaanza kubadilika rasmi.

Baada ya wiki moja ndugu wenye tamaa walikuja nyumbani na kuanza taratibu za kuchukua Mali mpaka nyumba yetu iliuzwa ndani ya miezi mitatu tu, kumbuka wakati huo nilikuwa katika utaratibu wa kujiandaa kwenda chuo kikuu udsm kusomea uhandisi wa Umeme. Niliumia sana,nilifukuzwa pia nyumbani nikawa sina pa kuishi wala pa kula.

Nilianza kuishi mitaani,na Kama unavyojua maisha ya Dar ni magumu sana, ilinilazimu kujiingiza katika maisha ya ukahaba ili tu maisha yaweze kwenda.

Wakati wa ukahaba wangu, nimewahi kukutana na changamoto mbalimbali sana Kama kulala njaa kwa kukosa chakula maana Kuna siku unaweza toka uspate hata mwanaume mmoja, na Kuna baadhi ya siku nilikuwa nasafiri mpaka morogoro msamvu kusaka wateja,maisha yalikuja magumu sana i

Siku moja nikiwa nimekaa zangu, sehemu niliyokuwa nimepangisha Mtoni kijichi,mida ya saa 4 asubuhi Mara ikaja gari moja, ikasimama mbele ya nyumba ile, wakashuka watu wawili wote wanawake wakanifata wakanisalimia na wakaniuliza, samahani wewe ndio manka Anthony Mushi, nikawajibu ndio Mimi.

Wakajitambulisha wametokea ofisi ya Rais utumishi na utawala bora,ninahitajika na bosi wao ofisini nilishtuka sana,na nikawauliza huyo bosi wao ananijua? Wakanijibu wao wamepewa maelekezo ya kunitafuta na ndipo walipojua ninapoishi.

Nilijiandaa nikaondoka zangu,huku nikiwa na mawazo akilini kwangu,je huyu bosi niliwahi kutoka nae? Au Ni mteja wangu? Ila nilipiga moyo konde nikaenda na kusema nitajua huko huko.

Nilifika na kupelekwa moja kwa moja ofisini kwa huyo bosi.baada ya kufika sikumkumbuka ,ila akajitambulisha kuwa yeye Ni katibu ofisi ile iliyopo Mjini Dar es Salaam.aliniuliza maswali mengi sana na mwisho wa siku akaamua kupasua ukweli.

Akanambia kwamba ofisi yake imeanza kunifatilia tangu nilipochaguliwa kidato cha kwanza tabora girls na wamenifatilia nyendo zangu kwa muda wa miaka 9, na ndipo Leo imekuwa tamati na ninatakiwa kujiunga nao ili na Mimi nianze kufatilia watu,sikumuelewa ila nilipiga moyo konde nikasema liwalo na liwe.

Waliniruhusu nirudi nilipopanga nikachukue vitu vyangu vya muhimu nirudi pale,baada ya hapo nilipelekwa kwenye nyumba Safi na siku 3 zijazo nikapelekwa jeshi la kujenga taifa, nikaanza mafunzo na nilipomaliza, nilipangiwa kwenda kozi maalumu kurasini,na baada ya hapo nilipewa first appointment ikulu.

Hivyo napenda kuwaasa ndugu zangu hasa wadada, usikate tamaa, Hujui kusudi la maisha yako hapa duniani.

Thanks
 
Upvote 62
Ikulu ya wapi? Mbona kwenye list ya majina ya watumishi wa Ikulu haumo? Kumbuka hum JF kuna HR Department wa Ikulu wanao weza kuangalia kwenye database muda wowote . So tutajie ID number yako uliyokuwa unatumia kwanza.

Kumbuka kwa watumishi wa Ikulu ID zao zina namba maalum so taja kwanza ndo tuweze kuamin story yako...
 
Jamaa aliumiza kichwa Sana kupitia huo wimbo pia Kuna ule wa sister sister aliomshirikisha Paulina Zongo nao unaujumbe mzito sana

Hata Simba wa Africa nao ni mzuri ,kuna pini la GK wa zamani sana alimshirikisha fina mango unaitwa Mama nao ni mzuri sema haupatikani kabisa online.(Nikupe nini mamaaa(Fina mango) ,mtoto hakui kwa mama(GK).
 
Kwa kazi unayoifanya inaonekana haitakiwi ujulikane hadharani, sasa huoni kwa story hii ni kama umejianika?
 

Boko boko hili! If you are 29 means, ulimalza form4 2009. Lkn Kwa story unatuambia Mzee alipofariki ulikua unajiandaa kwenda Chuo Kikuu. Alafu kuna mdau umejibu Mzee alipata ajali 2009[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1430] #FictionHizi
 
Kwanza mimi pale alipoanza kusema tu eti ofisi ya Nyeti ya serikali ilianza kumfuatilia tangu akiwa anasoma sekondari nikaona ni uongo tayari.
Siku hizi hakuna kazi za kupewa kinamna hiyo,ilifutika siku nyingi sana hiyo staili.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nimevutiwa na kichwa cha habari ndio maana nimesoma hadi mwisho ingawa najua hii ni ufupisho wa habari ndefu, kama, nasema tena, kama ni ya kweli! Hata hivyo wakati nasoma nilipoona habari za wazazi na hiyo ya kusoma Tabora Girls (TG), nikaanza kuunganisha DOTS ili nipate habari kamili. Hivyo vigezo viwili, cha kazi za wazazi wako na kusoma TG nikapata muunganiko wa DOTS, kwani mimi nilisoma Tabora Boys (TB) na ninajua namna Serikali ilivyo kuwa inapenda kuajiri wanafunzi toka shule hizo mbili kwenye Idara nyingi nyeti kama Ikulu, Usalama wa Taifa na huko Majeshini. Nimalizie kwa kusema kuwa kama habari hii ni kweli basi wadada wengine waione na WASIKATE TAMAA.
Umeingizwa chaka

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Iwapo walikuwa wanakufuatilia,Kwanini hawakukusaidia usiingie kwenye wimbi la kuuza hapo mnapotolea watoto kuja ulimwenguni
 
Back
Top Bottom