Manny Pacquiao Kuachana na Ngumi, atatundika gloves mwaka 2016

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Bondia kutoka nchini Philippines, Manny Pacquiao atatundika gloves mwaka 2016 baada ya kuutumikia mchezo wa masumbwi tangu mwaka 1995.

Taarifa za kustaafu kwa bondia huyo zimetolewa na promota wake Bob Arum alipokua akihojiwa na muandishi wa habari wa tovuti ya TMZ huko West Hollywood nchini Marekani, siku ya jumanne.

Arum alisema Pacquiao amepanga kuchukua uamuzi huyo kwa kutaka kupumzika na kuwapisha wengine ili watambulike na kutimiza malengo yao kwenye mchezo wa masumbwi ambao umebeba vijana wengi duniani kote. Anatataka apate muda wa kutosha wa Kujishughulisha na Siasa ili Mwakani apate Useneta huko kwao Philippines.

Promota huyo alisema bondia huyo anayetambulika kimataifa ana umri wa miaka 36 na mwezi Disemba mwaka huu atafikisha umri wa miaka 37, hivyo anaamini ni wakati mzuri kwake kufanya maamuzi ya kujiweka pembeni.

==============================



Chanzo:www.tmz.com
 
Last edited by a moderator:

..alryt; all the best manny.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…