Mantiki ya kiingilio 7-7 ni nini?

Mantiki ya kiingilio 7-7 ni nini?

educator2025

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Posts
395
Reaction score
455
WAKATI MAONYESHO YA 7-7 YAKIENDELEA UWANJA WA MWL. NYERERE KILWA ROAD NAJIULIZA HIVI IWEJE TANTRADE WAWEKE VIINGILIO KWA ANAEINGIA HUMO UWANJANI?

WAKATI HAKUNA HUDUMA YOYOTE (mfano vyoo, maji nk) wanayotoa kwa waonyeshaji au wanunuzi? je hawaoni kuweka kiingilio kunafanya watu wengi kutotembelea maonyesho hayo? hivyo wafanyabiashara kuzidi kukosa wateja?
 
hata mi sikutegemea kuwepo kiingilio yale maeneo ila jana nimeshangaa nadaiwa Tsh.3000 kama ada ya kuingia!!
 
Hao TANTRADE hawana justification yoyote ya kuwatoza kiingilio wanaoingia maana tayari hao wafanyabiashara wameshatoa pesa ya kukodisha nafasi humo ndani, zaidi humo ndani kuna matangazo kibao ya biashara ambayo yanalipiwa sasa ya nn tena kiingilio? yaani ni kama uambiwe ulipie kiingilio wakati unaingia SUPERMARKET.
 
WAKATI MAONYESHO YA 7-7 YAKIENDELEA UWANJA WA MWL. NYERERE KILWA ROAD NAJIULIZA HIVI IWEJE TANTRADE WAWEKE VIINGILIO KWA ANAEINGIA HUMO UWANJANI? WAKATI HAKUNA HUDUMA YOYOTE (mfano vyoo, maji nk) wanayotoa kwa waonyeshaji au wanunuzi? je hawaoni kuweka kiingilio kunafanya watu wengi kutotembelea maonyesho hayo? hivyo wafanyabiashara kuzidi kukosa wateja?

Mkuu, kwani hayo ni Maonesho ya Biashara ama Biashara??? make vitu vyote vinauzwa hapo, sema tu ni kwa bei pungufu.
 
Kiingilio kinasaidia kupunguza vurugu mle ndani. Sipati picha bila ya kiingilio hali ingekuwaje, "pocket" wangejazana mle ndani. Naunga mkono kiingilio kidogo kama kile, sio ishu sanaaa. Mtu ambaye yuko serious kufuatilia maonesho kama sehemu ya kuangalia fursa huwezi ukaumizwa na kiingilio cha sh elfu tatu. Binafsi nimejifunza mengi ukizingatia ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria na Inshallah sitokosa tena kama afya na muda utaruhusu. TUKUTANE KWENYE NANE NANE.
 
Mkuu, kwani hayo ni Maonesho ya Biashara ama Biashara??? make vitu vyote vinauzwa hapo, sema tu ni kwa bei pungufu.
Kwa hiyo ulitaka vile vitu vinavyooneshwa vigawiwe bure kwa watanzania ili iwe maonesho ya biashara siyo? Kuna haja ya WaTZ tukaweka haya mambo ya UKAWA pembeni tuwe serious kwenye kutafuta.
 
Nchi hii ya maajabu kweli ndo nchi pekee (kwa ufahamu wangu) unalipia PANTONI. wakati ndugu zetu Kenya hapo pamoja na kupenda sana pesa lakin Pantoni zao ni bure. Sasa sisi tunatoza pesa kila sehemu ukiuliza unaambiwa kama huna pesa PIGA MBIZI.
 
Mkuu unaongelea panton, njoo Moro mtaa wa Kichangani uone vijana wametengeneza daraja lililotelekezwa na Halmashauri na wanajikusanyia fedha kwa raha zaaao...Serikali usingizini fofofo
 
Back
Top Bottom