Manula apumzishwe hadi mwisho wa ligi

Manula apumzishwe hadi mwisho wa ligi

tatamajuva

Member
Joined
Sep 11, 2019
Posts
74
Reaction score
84
MANULA NI MUOGA NA MOYO WAKE NI YANGA​

Mimi ni mshabiki kindakindaki wa Simba , nimemfuatilia kwa karibu manula kwa mechi alizocheza na yanga ni dhahiri hakubali yanga kufungwa, hivyo yeye ni mmoja wa wachezaji wanaoisaidia Simba kufungwa, hii imedhibitishwa na magoli aliyofungwa duru la kwanza na mechi ya leo Yana ufanano, hii mechi alipaswa kudaka kakolanya na siyo huyu , manula ni kipa mzuri kwenye mazoezi na si kwenye Derby kama hii.

Huyu dhahiri pamoja anaichezea Simba sports club ila moyoni mwake ni Yanga. Hali kadhalika kocha mkuu hafai kwani ni mtu asiyechukua maamuzi sahihi kwa wakati kwa kutokufanya substitution mapema.

Nashauri Manula asipangwe hadi msimu uishe wa duru la pili, pia kocha mkuu amalizie msimu aende zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika historia ya soka ni kipa mmoja tu toka Colombia ambaye angeweza kuokoa goli lile.
 
Hujui mpira wewe..! Kuna muda ni muhimu kutoa Kongole kwa mpigaji..!
 
Msisingizie manula, hilo zeruzeru lenu ndio limetutia hasira tukaamua kuupiga mwingi
 
Kama snafungwa Alison Becker sembuse na Manula ?! . Ok amefungwa bao moja , hao wachezaji wengine wamefanya nini ?!

Punguza uswahili

Sent using Jamii Forums mobile app

Umenikumbusha ya Athuman Mambosasa na goli lililofungwa na Sunday Manara kwenye fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki Zanzibar (1975 kama sikosei). Mashabiki wa mikia walimtuhumu Mambosasa kuachia hilo goli nae akawauliza: "kama mimi niliachia goli moja wengine wangefunga magoli 3 tungepoteza mechi"?
 
ohoooo manula ameuza mechi ohooooo sijui kitu kidogo kimetembea, acheni kujidanganya mkia nyie, kile kilikuwa ni 'kirungu' kizito, a.k.a 'intercontinental ballistic missile la ki-russia 'SS20', hakuna kipa duniani anaye weza kukizuia
 
Back
Top Bottom