Manula apumzishwe hadi mwisho wa ligi

Manula apumzishwe hadi mwisho wa ligi

MANULA NI MUOGA NA MOYO WAKE NI YANGA

Mimi ni mshabiki kindakindaki wa Simba , nimemfuatilia kwa karibu manula kwa mechi alizocheza na yanga ni dhahiri hakubali yanga kufungwa, hivyo yeye ni mmoja wa wachezaji wanaoisaidia Simba kufungwa, hii imedhibitishwa na magoli aliyofungwa duru la kwanza na mechi ya Leo Yana ufanano, hii mechi alipaswa kudaka kakolanya na siyo huyu , manula ni kipa mzuri kwenye mazoezi na si kwenye derby Kama hii.

Huyu dhahiri pamoja anaichezea Simba sports club ila moyoni mwake ni yanga.
Hali kadhalika kocha mkuu hafai kwani ni mtu asiyechukua maamuzi sahihi kwa wakati kwa kutokufanya substitution mapema.

Nashauri manula asipangwe Hadi msimu uishe wa duru la pili, pia kocha mkuu amalizie msimu aende zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pimbi kabisa
 
Wewe huna hoja kabisa. Timu kufungwa ni kawaida hata Manchester City wamefungwa na Man U tena mara mbili, ushindi wa Man U ukichangiwa na makosa ya kipa Ederson wa Man City lkn hatujasikia wakisema kuwa anaipenda Man U au hatujasikia wakisema Guardiola afukuzwe.

Acheni ushamba na mambo ya kiswahili, kwani Simba ni nani ndio wasifungwe? Ushabiki mwingine ni maandazi kabisa.
 
Swali je forward kina Boko na Kagere walikuwa wapi?
Simba Kwa Sasa haina Mshambuliaji wa Kiwango cha Simba.
Sijui kwanini Benchi la ufundi limeshindwa kabisa kutafuta washambuliaji vijana hata Wakitanzania wenye kiwango hata cha Iddi Selemeni NADO.
Kamwe Mzee Boko na Mzee Kagere hawawezi kutumainiwa Kwa Mechi ngumu, kama Ile ya Yanga.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
na Mkude nae ni Yanga asipangwe.
Mkude siku zote kwenye mechi ya Simba na yanga anacheza rafu nyingi za makusudi na kiwango Cha uchezaji wake kinakuwa kidogo, huyo naye naamini ni yanga, wachezaji wawili hao wakiendelea kupangwa watatusababishia kufungwa mechi nyingi, wana tamaa, GSM iliwapa chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magoli anayofungwa De gea hatujawahi kusikia mambo kama haya, tatizo mnakua mamluki katika soka hivyo hamuelewi chochote juu ya mchezo huu pendwa,
Mtu wa mpira hawezi kumlaum manula kwa goli lile la adhabu ndogo, siku zote adhabu ndogo mtu wa kwanza kucheza ni wale waliopanga mstari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba Kwa Sasa haina Mshambuliaji wa Kiwango cha Simba.
Sijui kwanini Benchi la ufundi limeshindwa kabisa kutafuta washambuliaji vijana hata Wakitanzania wenye kiwango hata cha Iddi Selemeni NADO.
Kamwe Mzee Boko na Mzee Kagere hawawezi kutumainiwa Kwa Mechi ngumu, kama Ile ya Yanga.


Sent using Jamii Forums mobile app
Nado ni mtu sahihi kulik kahata na Luis combined

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Manura kafungwa , viungo pamoja na washambuliaji walifanya juhudi gani kurudisha bao na kuongeza bao la ushindi.

Kwa ujumla timu ilicheza hovyo , bao walizokosa kina Kagere zilitosha kuamua mchezo mapema.

Walikosa umakini tangu mwanzo na kujiamini kwingi,

Tatizo lingine faulo nyingi ndio ziliigharimu timu,Mkude ni vizuri apewe ushauri plus clatous Chama rafu za nini badala ya kutengeza nafasi, upuuzi upuuzi mwingi tu.

Alafu mechi kama hizi lazima wachezaji wakomae kazi kazi mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom