Manunuzi ya Joseph Mbilinyi Sugu kwenye Soko la Igawilo huko Mbeya Mjini yaleta mtikisiko mkubwa

Manunuzi ya Joseph Mbilinyi Sugu kwenye Soko la Igawilo huko Mbeya Mjini yaleta mtikisiko mkubwa

mtafutieni Jimbo lingine , vinginevyo mtapoteza spika wenu
Tanzania hii spika akadhindwe na Mbunge wa chama pinzani, ntakuwa nje ya Tanzania kiufupi ni fantasy cheo Cha spika akipatikani hovyo hovyo .
 
Leo hii huko Mbeya Mjini kulikuwa na ziara ya manunuzi ya nyanya na mishikaki iliyofanywa na Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo bilionea Joseph Mbilinyi ambaye pia anafahamika kama Sugu au Real Jongwe kama anavyofahamika siku hizi, ama waweza kumtambua kama mfungwa wa kisiasa.

Kama masihara tu akaibuka kwenye Soko la Igawilo ambako alienda kununua nyanya na vitunguu, yaani viungo mbalimbali zikiwemo karoti na pilipili hoho kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake, baadaye wadau wakampeleka hadi eneo la kuchomea mishikaki, ili waitafune kidogo.

Basi bwana kufumba na kufumbua akajikuta amezungukwa na umati ambao haufahamiki ulikotokea! Hakika huyu jamaa anapendwa Mbeya Mjini! Kwa kifupi ni kwamba shughuli za soko ni kama zilisitishwa kwa muda kupisha Sugu anunue nyanya! Yaani ilifika wakati tukahofia kwamba huenda polisi wangevurumisha mabomu ya machozi, maana umati wake unazidi ule wa mechi ya Yanga dhidi Al Hilal ya Sudan kwa Mkapa.

Kwenye Hili nimejifunza jambo moja kubwa sana, kwamba usishindane na aliyejaaliwa, utadhalilika sana. Wazaramo wana msemo mmoja kwamba, "Acholile kachora".
View attachment 2395663
View attachment 2395664
View attachment 2395665
View attachment 2395668
Ila haya ma sifa ulivyompamba ni bora ungempelekea ex wake Faiza, mbona Sugu mwenyewe wa kawaida sana. Wengine tunamfahamu Sugu toka amekuja mjini Daslama akapanga chumba kinondoni yupo choka mbaya tunamnunulia bia kwa Manyanya na PR camp. alikua mshamba mshamba tu.
 
Back
Top Bottom