Manyara: Baba mbaroni kwa kuwabaka binti zake watatu

Manyara: Baba mbaroni kwa kuwabaka binti zake watatu

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Polisi wanamshikilia baba mwenye miaka 57 mkazi wa Kijiji cha Ndaleta mkoani Manyara kwa tuhuma za kuwabaka binti zake watatu wenye miaka 15, 17 na 18. Wizara ya Maendeleo ya Jamii imesema watoto hao tayari wamepatiwa matibabu na wanaendelea kupatiwa msaada wa kisaikolojia.

---
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57, mkoani Manyara Kaskazini mwa Tanzania anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake watatu wa kike alhamisi ya juma lililopita.

Akitoa taarifa jijini Dodoma mapema leo, Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Prudence Constantine amesema kuwa baba huyo anadaiwa kuwafanyia tendo hilo la kikatili mabinti zake hao wenye umri wa miaka 15, 17 na 18 katika Kijiji cha Ndaleta, wilaya ya Kiteto.

Constantine alisema kuwa wizara imesikitishwa na taarifa za tukio hilo na inapenda kutoa taarifa kuwa tayari mtuhumiwa yupo mikononi mwa polisi kwa taratibu zaidi za kisheria.

Aidha, amesema kuwa watoto wameshapatiwa huduma za kiafya na wanaendelea kupatiwa huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii.

Mkuu huyo alisema kuwa hivi karibuni kwenye jamii kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili kwenye makundi yote ya jamii ikiwemo watoto.

Hivyo alisema kuwa Wizara inawaomba wananchi kuungana kupinga ukatili wa makundi yote kwa ujumla wake na kutoa taarifa mapema kwenye vyombo vya serikali na vyombo vya kijamii vinavyoweza kutoa msaada wa haraka pale tukio linapotokea.

Chanzo: BBC
 
Aisee,watoto wetu wamkimbilie nani sasa?
JamiiForums-797185051.jpg
 
mambo ya kukataa kuoa mnabaka watoto na bado adi mbake mende
 
Hizi habari huwa ni za ukweli au ni abrakadabra tu? Yaani baba abake watoto wake wa kuwazaa haingii akilini. Kwanza hao mabinti ki umri ni wakubwa kuweza kumkatalia baba yao na kumkimbia wasibakwe. Labda huyo baba akili zake haziko sawa kiasi cha kutokuona aibu ya kubaka wanawe wa kuzaa na hana maadili ya dini
 
Duh huyu baba kiboko aisee watatu duh[emoji849][emoji849]
Screenshot_20220117_170044.jpg
 
Akiulizwa kulikoni atasema shetani alimpitia mara tatu.
 
Aliwabaka namna gani? Hebu elezea vizuri tafadhali.
 
Back
Top Bottom