JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa Mkoa, Queen Sendinga amesema ajali iliyotokea jana Agosti 31, 2024 ikihusisha Costa iliyobeba Wanafunzi wa Shule ya Endasak Sekondari na Lori la mizigo lililokuwa linatokea Burundi, imepoteza Wanafunzi Watatu na dereva wa Costa huku majeruhi wakiwa 31
Amesema “Ajali imetokea eneo la Guardian, Halmashauri ya Babati, uchunguzi umeonesha kulikuwa na uzembe wa dereva wa Lori, amekimbia lakini ameacha vitambulisho vyake na vitu vingine, tumevitambua, Jeshi la Polisi na Vyombo vya Usalama vinaendelea kumtafuta.”
Ameongeza “Majeruhi wote wanatibiwa kwa gharama za Serikali, miili ya marehemu imehifadhiwa ikisubiri taratibu za familia na Serikali tutatoa ushirikiano wote watakapohifadhiwa