Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
MANYARA: BILIONI 3 KUTUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA HOSPITALI YA MANYARA KWA MWAKA 2024/2025
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema Serikali imejipanga kuboresha huduma za afya katika mkoa wa Manyara kwa kutenga Shilingi Bilioni 3 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya kuboresha miundombinu Hospitali ya Mkoa wa Manyara.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Manyara, Mhe. Regina Ndege, aliyehoji ni lini Serikali itaanzisha ujenzi wa wodi za wanaume na wanawake, Dkt. Mollel amesema hospitali hiyo kwa sasa imekuwa ikitoa huduma kwa kutumia jengo la mama na mtoto kama OPD, lakini sasa Serikali imechukua hatua za makusudi kujenga miundombinu ya kisasa.