mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Manyara!
Jeshi la Polisi mkoani Manyara linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Silaloda Mji wa Mbulu, Harold Hhando, kwa tuhuma za kumuua mtoto wa kaka yake, Emmanuela Hando (13), kisha kumtoa viungo vya mwili.
Inadaiwa kuwa Hhando alimuua mtoto huyo wa Kaka yake kwa kumpasua katikati ya miguu (mapaja) na kumtenganisha vipande viwili, Kisha kumtoa maini na kutaka kuyapika ili ale'
===

Inadaiwa kuwa Hhando alimuua mtoto huyo wa kaka yake kwa kumpasua katikati ya miguuu na kumtenganisha vipande viwili kisha kumtoa maini na kutaka kuyapika, ili ayale.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Marrison Mwakyoma, akizungumza mwishoni mwa wiki, alisema tukio hilo lilitokea kijijini hapo.
Kamanda Mwakyoma alisema chanzo cha tukio hilo ni ushirikina, kwani Hhando ameeleza kuwa aliambiwa na Mungu wake amuue mtoto wa kaka yake na kula maini, ili avune mazao mengi.
Alisema Hhando ni mkulima wa eneo hilo la Silaloda, hivyo imani za kishirikina zimesababisha kumuua mtoto huyo kwa kumpasua na kudai kuwa ameoteshwa kufanya hivyo.
“Mtuhumiwa anadai kuwa ameoteshwa na Mungu wake na ana akili zake timamu, hivyo alitarajia kula viungo hivyo, ili aweze kupata mazao mengi zaidi shambani kwake,” alisema Kamanda Mwakyoma.
Kamanda Mwakyoma alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutojihusisha na imani za kishirikina na kusababisha mauaji kama hayo ya kikatili ikiwamo kuuana ndugu kwa ndugu.
Wakizungumza na Nipashe baadhi ya wananchi wa eneo hilo, akiwamo, John Baynet alisema wananchi wa eneo hilo wamesikitishwa na kitendo hicho cha Hhando kumuua binti huyo mdogo ambaye ni mtoto wa kaka yake.
Alisema: “Hhando hakuwa na matukio mabaya ila tumeshangazwa na mauaji hayo ya kikatili aliyomfanyia mtoto wa kaka yake kwani hana taarifa za matukio ya uhalifu”
Chanzo: Nipashe