GE2025 Manyara: Mgombea udiwani alalamikia kubadilishiwa jina siku ya kupiga kura za maoni

GE2025 Manyara: Mgombea udiwani alalamikia kubadilishiwa jina siku ya kupiga kura za maoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mgombea Udiwani Kata ya Masakta, Wilayani Hanang, Mkoani Manyara, Mathias Daqaro, ametoa malalamiko kuhusu kubadilishwa kwa jina lake kwenye fomu za kupigia kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), jambo ambalo alidai limechangia kushindwa kwake katika mchakato huo.

Mathias amesema baada ya matokeo ya kura za maoni kutangazwa, tukio hilo limevunjwa haki yake kama mwanachama na mtia nia wa nafasi hiyo. Ameomba uongozi wa juu wa CCM kuingilia kati ili kuhakikisha haki yake inatendeka.

Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Naye, Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Bi. Neema Adam, alipotafutwa kwa njia ya simu kuhusu malalamiko hayo, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa mmoja wa wagombea na kutoa maelezo zaidi kuhusu hatua zinazochukuliwa.
 
Back
Top Bottom