Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Mtuhumiwa huyo amekamatwa kutokana na mtego ulioandaliwa na askari wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA), Askari wa Burunge WMA na askari wa Taasisi ya Chemchem association ambayo imewekeza shughuli za Utalii katika eneo hilo.
Meja ambaye amekuwa akisakwa kwa tuhuma za uwindaji wa Twiga na kuuza Nyama maeneo mbalimbali amekamatwa maeneo ya Mfulwang'ombe kwenye Kambi ya samaki.
Mtuhumiwa huyo ambaye haikuwa rahisi kutiwa nguvuni alikamatwa na kikosi cha askari maalum wa Wanyamapori James Misuka, Samweli Bayo, Khamis Chamkulu, Mohamed Abdallah, Pascal Mandao, Emmanuel Duxo, Wilfred Ngitoor na Karoli Umbe baada ya kupata taarifa kwa siri.
Mwendesha Mashitaka wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA) Getrude Kariongi amekiri kukamatwa mtuhumiwa huyo.
"Ni kweli amekamatwa huyu mtuhumiwa alikuwa anakabiliwa na kesi kadhaa za ujangili na tayari amekabidhiwa polisi," amesema.