Manyara: RC Nyerere afungua kongamano la watu wasioona

Manyara: RC Nyerere afungua kongamano la watu wasioona

John Walter

Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
68
Reaction score
63
Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amesema serikali itaendelea kushirikiana na watu wenye ulemavu katika kuwapatia huduma zote zinazohitajika kama watu wengine.

Amezungumza hayo katika kongamano la watu wasioona linalofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria mjini Babati leo oktoba 19,2022 ikiwa ni maadhimisho ya fimbo nyeupe duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Manyara.

Amesema kongamano hilo ni muhimu kwa watu wasioona kwa kuwa linatoa fursa kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzifanyia kazi.

Aidha amewahakikishia usalama watu hawa wasiiona muda wote wa maadhimisho ya fimbo nyeupe lakini pia katibu tawala Mkoani hapa Caroline Mthapula akiitaka jamii na wadau mbalimbali kutambua wajibu wao na haki kwa wasiiona nchini katika kuchangia maendeleo ya taifa.

Kilele cha maadhimisho hayo ni Oktoba 21,2022 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa yenye Kauli mbiu isemayo “Watu wasioona,tujumuishwe katika ajira,michezo na Teknolojia ya habari na mawasiliano kwa maendeleo endelevu”.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha watu wasioona Tanzania (TLB) Omary Sultan amewataka wasiiona kutotumia ulemavu huo kama njia ya kufanya mambo yaliyo kinyume cha taratibu na sheria za nchi.

Sultan amesema ni vyema watu hawa wenye ulemavu wa kutokuona kuheshimu sheria na kutokujichukulia tofauti na makundi mengine ya raia nchini.

Makamu mwenyekiti wa TLB Selemani Idrisa amesema mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameacha alama kubwa katika nchi kwa watu wasioona ambapo aliwahi kuwapa fursa ya kugusana nae japo hawaoni.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Manyara Simon Lulu amesema chama cha Mapinduzi kitaendelea kuwaunga mkono watu wenye ulemavu katika kila Nyanja kama walivyofanya waasisi wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Karume.

DSC_1570.JPG
 
Back
Top Bottom