Manyerere, kwa makala hii umepotea sana (Tatizo la Tanzania si Katiba mpya)

JipuKubwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2013
Posts
2,341
Reaction score
2,390
Nimesoma makala ya Manyerere katika gazeti la Jamhuri la 23/12/15, nimegundua kuwa mwandishi hajui katiba ni nini.

Chanzo: Jamhuri
 
Samahani ,ni toleo la 23/12/15.
 
Ngoja uzi ujae ujae nitarudi kucomment baadae
 
huyu Manyerere Jackton ni mganga njaa kama makanjanja wengine walivyo wala asikupe shida.
 
Last edited by a moderator:
Umesahau kuwa juma nkamia alisema hawa jamaa ni makanjanja?
 
Andiko lina ujumbe mzito japo haliwezi kuondoa uhalali wa katiba mpya
 
Katiba mpya ni muhimu kwa wakati wa sasa na vizazi vijavyo, maana usitegemee siku zote Rais atakuwa Magufuli.

Tunahitaji Bunge huru, mahakama huru, na Tume ya uchaguzi huru.

Lakini pia muundo wa serikali ie baraza la mawaziri lazima liwekwe kwenye katiba.

Hii itaepusha kuwa na serikali ya kitabaka, kifamilia, kimtandao, kubwa, ya mizigo, isiyowajibika yenye watu walafi nk
 
Umesahau kuwa juma nkamia alisema hawa jamaa ni makanjanja?

Unampa sifa asiyostahili, huyo muita wenzake makanjanja.

Naye pia aliitwa kanjanja na aliyewahi kuwa "boss" wake alipokuwa BBC-Swahili,Tido Mhando...
 

Haya ndiyo mambo waandishi wetu wanatakiwa kujua.
 
Mleta mada ndiye hajui kilichoandikwa na manyerere. Kwa ufupi, mwandishi amejaribu kuonyesha kuwa watanzania wanapaswa kubadilika kifikra na kiutendaji. Hapingi katiba, isipokuwa anasema kwa mwenendo huu wa watu kupuuza mambo, hata ikija katiba mpya itakuwa bure tu. Anahimiza watu kubadilika kifikra. Msome mara mbili mbili utajua anachomaanisha.
 
msingi ni kubadilika kifikra pasipo kujali KATIBA YA 1977 ama MPYA; Uongozi uliopo wapaswa kufuatilia yaliyoko katika KATIBA vinginevyo ni kazi bure
 

Siyo kosa lako,kufikiri na kutafakari ni kazi ngumu sana ndiyo maana siyo kila mtu huifanya hiyo kazi.Yote aliyolalamikia Manyerere,msingi wa utatuzi wake ni katiba mpya.Soma basi hata makala ya Jenerali iliyopita utaelewa kwanini tunasema katiba mpya ni muhimu.
 
Mambo
We ndo umeelewa vibaya... Kwa ufupi manyerere anatumiwa kuwapamba wakubwa.
Katibu mpya sio tu kuwa ni muhimu bali ni lazma, jua hvo..
 
Mambo
We ndo umeelewa vibaya... Kwa ufupi manyerere anatumiwa kuwapamba wakubwa.
Katibu mpya sio tu kuwa ni muhimu bali ni lazma, jua hvo..
Sijaona wapi anapamba wakubwa. Kasema vizuri sijui kwanini akili zenu zimelala. Anachosema ni kwamba Katiba mpya pekee siyo suluhisho la matatizo ya nchi yetu, bali ni kuwa na viongozi wawajibikaji. Unaeweza kuwa na katiba nzuri kama kenya lakini ufisadi ukawa pale pale. Waulize kenya nini kimebadilika na sasa wanataka kuibadili. Mwelewe manyerere siyo mnashambulia tu.
 
Katiba ambayo raisi wa nchi hashitakiwi popote unatarajia nini hasa kwa hawa viongozi wetu wa kiafrika?
 
Comments zinanifanya niamini kweli watanzania wengi wana IQ ndogo sana. . . Mtu katoa hoja nyingi na za msingi lakini pumbavu moja tu linakuja na kujibu kirahisi tu huyu mwandishi anatumiwa...

Hoja kuu ya mwandishi ni kuwa katiba pekee sio suluhisho la kuleta maendeleo kwa watu, na hajasema hakuna umuhimu wa katiba mpya ili raisi aweze kushtakiwa...

Tatizo la watanzania wengi ni UNYUMBU, jitu likiaminishwa jambo baaasi halitafakari wala kujiuliza mara mbili....


Haya tusubiri ije katiba mpya af we endelea kumuomba mamako vocha kisha ushinde instagram, jf na facebook uone hayo maendeleo...

Jambo la msingi ni kuwa na viongozi wachapakazi, waadilifu na wasikilizaji. Katiba mpya ije kama silaha au ngao dhidi ya wale watakaokiuka uadilifu, uzalendo na uchapakazi.

Katiba mpya pekee sio suluhisho pekee. .
 
hivi na manyerere nae ni muandishi wa habari? sishangai kuwa alitaga f4 na kwenye uandishi yupo kwa sababu hakuwa na namna ingine ya kuishi.
 
hivi na manyerere nae ni muandishi wa habari? sishangai kuwa alitaga f4 na kwenye uandishi yupo kwa sababu hakuwa na namna ingine ya kuishi.
Mbweha kabisa wewe. Manyerere humfikii kwa namna yoyote. Kosoa hoja, siyo kuropoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…