Kwa sababu za kiusalama si vema watoto wachanga kuwa karibu na paka, na haswa wakiwa peke yao. Kama inavyojulikana paka ni mmoja wa wanyama wanao penda sana joto joto... na ndio maana hawaweshi kuwa karibu na watu wanao wafuga. Kwa sababu hii paka anapo achiwa kuwa karibu na mtoto, na ikatokea kwa bahati mbaya kulaliwa na mtoto wako paka anaweza kumdhuru mwanao kwa niya ya kujihami na dhahma aliyo ipata na hii inaweza kusababisha mtoto wako kupata majeraha makubwa na kusababisha kumpoteza mwanao.
Wafugaji wa paka wanashauriwa kuwa waangarifu sana pale wanapokuwa wanaishi na watoto wachanga pamoja na paka ndani ya nyumba...
Pia inasemekana kuwa paka ni mnyama mwenye wivu, na haswa akiwa yeye ndiye aliyetangula kuja ndani ya nyumba kabla ya mtoto kuzaliwa... hii pia inaweza kusababisha mtoto kudhuriwa na paka kwa sababu paka yu aona kuwa ule upendo aliokuwa anaupata kwa baba na mama mwenye nyumba umehamia kwa mtoto mpya.
Kuhusu madai ya mama (yako) kuhusu manyoya ya paka kuwa ni sumu si kweli, uchunguzi wa kitaalam unasema kuwa ni majimaji yanayo toka kwa paka ndiyo yanaweza kuleta madhara kwa binadamu... kuna aina ya protein inayopatikana kwenye mate, jasho au maji maji ya paka ndio yanayoweza kusababisha allergen.
Protein aina ya Fel d 1 ndio inayopatikana kwenye hayo maji maji, aina hii ya protein inaweza kujipenyeza na kuweka makazi yake ndani kabisa kwenye mapafu ya mwanadamu.
Protein hii mara inapofika na kuweka makazi yake kwenye mapafu, inaweza kusababisha dalili za mhanga kuanza kushindwa kupumua vizuri, ikiwa ni pamoja na kuchochea shambulio la pumu.
NB:
Mama (yako) yupo sahihi kwa njia moja au nyingine kuhusu
madhara yanayoweza kuletwa na paka dhidi ya mtoto wako.