Manzese kwanini haiendelei?

kazuramimba

Senior Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
126
Reaction score
57
Wakuu,

Manzese ni moja kati ya kata za kitambo sana, 1975 tayari ilikuwa ni kata kamili yenye miundombinu inayoekeweka, ndio eneo la kwanza Tanzania kuwa na Daraja la wavuka Kwa miguu ambalo liligeuka kuwa kivutio enzi zile, Kwa miaka mingi manzese imekuwa kitovu cha biashara, burudani Na soko kubwa la unga wa mahindi.

Ajabu ni kuwa hii kata bado ni fukara sana, makazi yake ni duni sana, ukizunguka kwenye mitaa yake kuna ufukara wa kutupwa, mitumba kama sidilia ndiyo inauzika mno eneo hili. Shida iko wapi?

 
Manzese imebadikika sana ndg, mahoteli ya ghorofa kibao, inaenda kuipiku Magomeni mapipa, maduka makubwa usiseme, barabara za lami na mitaro ipo Kila sehemu, sijui unazungumzia manzese ya mwaka Gani? Pita na kagua tena, utaamini nikiongeacho ndg.
 
Haka ka jamaa na kamera zake ipo siku watakakaba tu wakaibie

Ulianza kwa dada poa kule ukaonywa hukuskia shauri yako we kuwa makini tu
 
Kwa nini hujajiuliza swali muhimu kwanza. Mbona Tanzania haiendelei?..
 
Manzese sehemu ya biashara mzee
Huoni sahv magorofa yanaporomoshwa....
Achana na manzese uwanja wa fisi huko

Ova
Nashangaa jamaa sijui anazungumzia manzese ipi? Kuanzia Argentina, Tiptop hadi kwa mfuga mbwa magorofa yanaporomoshwa balaa labda manzese ya midizini kule ndio bado.
 
Manzese, mburahati, kigogo, ilala, kuendelea hayo maeneo mpaka waliopo wote na walio wazaa wote wafe waje wengine[emoji3][emoji3][emoji23][emoji23] LABDA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…