Maofisa sita wa Polisi walilia DPP awapunguziwe adhabu kupitia Plea Bargaining

Maofisa sita wa Polisi walilia DPP awapunguziwe adhabu kupitia Plea Bargaining

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
21 October 2026
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam
1792596018790.jpeg

Maofisa sita waomba DPP wapunguziwe adhabu
Katika muendelezo wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili waliokuwa maofisa wa polisi na raia wengine, washtakiwa watano (kati ya tisa) wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiomba kukiri mashtaka yao ili kupunguziwa adhabu (Plea Bargaining).

Kesi hiyo ilipotajwa Oktoba 21, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ilielezwa kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 26 yakiwemo ya kujipatia Sh85.2 milioni kwa njia ya udanganyifu kwa ahadi ya kutoa leseni za kumiliki silaha.

Washtakiwa waliowasilisha maombi hayo kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa mahakamani na gazeti la Mwananchi ni pamoja na:
  • Sajenti John Kaposwe (46) – Aliyekuwa ofisa wa Jeshi la Polisi (F.5092)
  • PC Julieth Moshi (30) – Aliyekuwa ofisa wa polisi (WP 10050)
  • Damson Mnyilenga (59)
  • Simon Aloyce (60)
  • Vernand Liberio (29)
Washtakiwa wengine wanne waliosalia katika kesi hiyo bado hawajawasilisha ombi lolote kwa DPP
 
Kwenye list ya majina ya watuhumiwa lingekosekana jina la mtu kutoka kaskazini ningesema hao wamesingiziwa ..
 
Wazitapike hela zote walizokula. Hawa jamaa wamezoea sana kutuibia hela zetu.
 
Back
Top Bottom