DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Olympic hawatoagi helaMfano spain timu ya wanaume ya mpira imechukua gold medal, hela hiyo inagawiwa au anaoewa kila mmoja?
Vipi Olympic wenyewe wanatoa kiasi gani kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa 3 pembenj ya medali?
Kwahiyo watu wanagombea medal tu, ile medal ina gram ngapi?Olympic hawatoagi hela
Idadi ya gram sifahamu, wao kikubwa medali labda na vile mnavokaa pale kipindi husikaKwahiyo watu wanagombea medal tu, ile medal ina gram ngapi?
Sifahamu mgao wa pesa kwa michezo ya kitimu ila kwa nchi kama Marekani, wanamudu hivyo viwango walivyoweka kulipa mtu mmoja mmoja.Mfano spain timu ya wanaume ya mpira imechukua gold medal, hela hiyo inagawiwa au anaoewa kila mmoja?
Vipi Olympic wenyewe wanatoa kiasi gani kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa 3 pembenj ya medali?
Medali za Olympics zina thamani kubwa kwa nchi na washindi wenyewe.Kwahiyo watu wanagombea medal tu, ile medal ina gram ngapi?
Mfano ile medal ya dhahabu ina uzito gani?Sifahamu mgao wa pesa kwa michezo ya kitimu ila kwa nchi kama Marekani, wanamudu hivyo viwango walivyoweka kulipa mtu mmoja mmoja.
Pia sidhani kama Olympics wanalipa pesa yoyote kwa washindi.
Medali za Olympics zina thamani kubwa kwa nchi na washindi wenyewe.
Kevin Durant ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa basketball mwenye medali nne za dhahabu. Fikiria wamepita mastar wangapi ambao hawana hiyo rekodi? Hawa kina Lebron ndiyo wanaondoka hawawezi kumfikia. China wenyewe kuweka rekodi ya kulingana idadi ya medali za dhahabu na Marekani kwenye hii Olympics ni big deal sana katika angle ya kisiasa.
Kwa kucheki haraka haraka nimeona wanasema medali ya dhahabu ya olympics ina gramu 523 za silver na gramu 6 tu za dhahabu.Mfano ile medal ya dhahabu ina uzito gani?
Idadi ya gram sifahamu, wao kikubwa medali labda na vile mnavokaa pale kipindi husika
Na Norway nao wanakaujinga fulani ka kujifanya wajamaa wa mchongo 🤣😂🤣Tanzania kwa wote ingekuwa kuandaliwa chakula cha jioni ikulu na kupelekwa kupigiwa makofi bungeni na labda kupewa viwanja mji mpya wa serikali Dom
Tanzania wangepewa kadi za chama tawalaMashindano ya Olympics yana michezo mingi sana na mingine ni nadra sana kwa mwanamichezo kutengeneza kipato nje ya mashindano yale. Umewahi kujiuliza wanamichezo wanaoshiriki michezo ya Olympics wanafaidikaje ukiacha nafasi ya kushinda medali?
Ngoja nikuwekee mkeka wa mifano ya nchi kadhaa ujionee mwenyewe jinsi wenzetu walivyo serious na bendera za nchi zao (viwango katika shilingi ni kwa rate za leo za USD 1 = TSH 2,700.50)
Norway:
Gold - 0
Silver - 0
Bronze - 0
Kazakhstan:
Gold - Apartment ya vyumba 3
Silver - Apartment ya vyumba 2
Bronze - Apartment ya chumba 1
Ujerumani:
Gold - $21,900 (TSH milioni 59.1)
Silver - $16,400 (TSH milioni 44.2)
Bronze - $10,950 (TSH milioni 29.5)
Marekani:
Gold - $37,500 (TSH milioni 101.2)
Silver - $22,500 (TSH milioni 60.7)
Bronze - $15,000 (TSH milioni 40.5)
Ufaransa:
Gold - $71,200 (TSH milioni 192.2)
Silver - $27,400 (TSH milioni 73.9)
Bronze - $16,400 (TSH milioni 44.2)
Hispania:
Gold - $102,900 (TSH milioni 277.8)
Silver - $52,600 (TSH milioni 142)
Bronze - $32,900 (TSH milioni 88.8)
Italia:
Gold - $197,100 (TSH milioni 532.2)
Silver - $98,500 (TSH milioni 265.9)
Bronze - $65,700 (TSH milioni 177.4)
Taiwan:
Gold - $716,000 (TSH bilioni 1.9)
Silver - $250,000 (TSH milioni 675.1)
Bronze - $179,000 (TSH milioni 483.3)
Singapore:
Gold - $737,000 (TSH bilioni 1.9)
Silver - $368,000 (TSH milioni 993.7)
Bronze - $184,000 (TSH milioni 496.8)
Viwango vya nchi yako vikoje?
Nadhani Taiwan wameweka viwango vikubwa hivyo kwa sababu za kisiasa.
Nyumba isokuwa na amani ata ukiwapikia pilau la nyama si kituKenya vipi?
Jifunze kwanza fitina ya kuipata hiyo nafasi mpwa kabla ujajifunza hiyo baiskeli mpwaNext time najipeleka mwenyewe olympic NIkashiriki hata mbio za baiskeli najua ntatoboa,kule kijij8ni kuna baiskelu ya babu aina ya swala
Kenya wako vizuri wameshajua kitambo thamani ya hii kitu. Wameondoka na medali 10. Watu wao kibao wametoboa kupitia Olympics na mashindano mengine ya mbio duniani maana ukipata medali ya Olympics utapata mialiko mingine mingi duniani hadi mwènyewe uchoke.Kenya vipi?
Next time najipeleka mwenyewe olympic NIkashiriki hata mbio za baiskeli najua ntatoboa,kule kijij8ni kuna baiskelu ya babu aina ya swala
Jifunze kwanza fitina ya kuipata hiyo nafasi mpwa kabla ujajifunza hiyo baiskeli mpwa
Wajinga sana viongozi wetuNikisemaga nchi hii kuna mfumo wa kutupumbaza na kuwa tegemezi kwa mfumo wa ndani wa uchumi watu huwa hawanielewi. Njia zote za kutoboa kwa pesa za nje zimepigwa pini halafu wamejenga mazingira kama ni uzembe tu wa watu fulani ili mlalahoi asiweze kujumuisha moja na mbili.