Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nadhani wengi tunapenda kurahisisha sana suala la dini. Suala la kutaka taifa litoe maombi ili tuepuke ugonjwa wa Coronavirus ni nzuri - lakini je, mbona tunakuwa wepesi kusahau kanuni juu ya maombi?
Kanuni ziko wazi, ikiwa kama taifa tunataka mombi yetu yasikilizwe, basi kama taifa kwanza tunapaswa kuwaomba msamaha wale tuliowakosea - iwe ni katika masuala ya siasa, ya biashara, ya kuwanyima haki zao za kuishi, ya kuwanyima haki zao za binadamu, ya kuwanyima haki zao za kikatiba nk.
Ikiwa kama taifa tumefikia mahali, kwa sababu tu ya tofauti zetu za kisiasa tunauana, tunafungana jela kwa kuoneana, tunatekana, tunabambikiana kesi, nk, basi hatupaswi hata kudiriki kutoa wito wa kufanya maombi kabla hatujaomba msamaha juu ya dhambi zetu hizo nyekundu kama damu na wale tuliowakosea!
Tusipofanya hivyo, basi tutaomba hadi jasho la damu litutoke - na hatutasikilizwa! Tutabaki kuwa wafu tunaozika wafu wetu.