Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,921
- 4,683
Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana. Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na nchi ile ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.
Ee Bwana, usikie; Ee Bwana, usamehe; Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu nchi yako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.
Mbona taifa linafanya ghasia,
Na makabila wanatafakari ubatili?
Mfalme na watesi wa nchi wanajipanga,
Na wakuu wanafanya shauri pamoja,
Juu ya BWANA,
Na juu ya haki ya watu
wake,
Na tuvipasue vifungo vyao,
Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.
eeh Mungu wa mbingu na nchi tizama ukiwa wa watu wako Tanzania na uchungu wa mateso ya watawala wanayowalisha.
ukakumbuke Mungu kwamba mataso wanayoyapokea kutoka kwa watawa ni kwa sababu ya ukaidi wao.
Hata hivyo hawa watawala wawalao masikini wa nchi kama mtu aulavyo mkate hawana haki hiyo ya kufanya hivyo.
Basi Bwana nakusihi ukaukumbuke uovu huu wa watawala ukajilipize kisasi.
Maana imeandikwa kisasi ni juu ya yangu mimi Mungu.
Yeye aketiye mbinguni anacheka,
Bwana anawafanyia dhihaka.
Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,
Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.
Imenenwa
Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi;
Bali mwovu atawalapo, watu huugua na ni Heri kijana maskini mwenye hekima
Kuliko mfalme mzee mpumbavu.
ambaye hajui tena kupokea maonyo.
Mtu yule uliyemwokoa kwa ishara na mkono wenye nguvu walipo mmiminia risasi 32 na 16 zikamwingia asife ndio leo hii kwa ushirika ule wa waovu wa nchi hii uliojipanga kuiba kila kitu cha nchi kuanzia uchaguzi wamemkamata ili asiendeleze kazi ya mlinzi.
Eeh Mungu wa mbingu na nchi chungulia kutoka mbingu zako ukaone nafsi za hawa watawala kama sii za hatia ya wizi.
Mapato yao na anasa zao na biashara zao haziendani wala kufanana na mishahara yao. Zimetoka wapi sasa? Ni wezi wa hazina ya nchi. Wameiba uchaguzi na kujimilikisha uongozi kwa nguvu, ni ufalme wa kiimla na kwa hivyo hauna taji ya washiriki.
Wameiba pesa ya matibabu ya masikini wa nchi wanaotozwa kodi ya hadi mchicha na chumvi wanayokula.
Wameiba elimu ya hawa masikini hata wengi wao wamebaki kwenye lindi la ujinga wa kutoweza kupambanua. Wameingia ushirika wa kidhalimu na wageni kwa kuuza rasilimali za nchi kifisadi kupata pesa ya kununua haki ya masikini wa nchi hii.
Muumba wa mbingu na nchi chungulia kutoka katika mbingu zako ukaone mashauri yao maovu. Maana wamejiwekea haki na kujiapiza kwamba mtu yule uliyemwokoa kwa risasi 32 walizo mrushia umemrudisha mikononi mwao wamwangamize yeye pamoja wa wana wa nchi wanaolilia haki.
Basi twaomba sasa eeh Mungu na iwe kwao kama ilivyokuwa kwa farao na jeshi lake pale bahari ya shamu walipo fikiri muujiza ule uliowafungukia wana wa Israeli ni kwa ajili yao pia kuwapata ili wawaangamize.
Ndipo walipo ufikilia mwisho wao.
Na hawa wadhalimu wa nchi eeh Muumba uwafikishe panapo maji ya bahari kwa ajili ya hukumu yako ya haki.
Shakula cha hawa watawala walapo ugenini na majumbani mwao na watoto wao ni udhalimu na wizi mtupu, ni damu na nyama ya masikini wa nchi wanaokufa kwa kukosa matibabu na dawa ilihali wanagharimia kwa kodi na tozo zote.
Eeh Mungu kwa watawala hawa dhalimu na iwe hivi kwao kama ilivyokuwa kwa farao na jeshi lake,
Kwamba hukuufanya moyo wake mgumu ila ujilipize kisasi na kuonyesha kuwa unatawala Mbingu na nchi.
Nasi wana wa nchi tutauimba wimbo wa Musa mtumishi wako na wa mwana kondoo wako kama Israel walipo uimba wimbo wa Musa hapo kando ya bahari walipo tizama na kuona jinsi maangamizi ya Farao na jeshi lake lilivyochinjwa na yale maji ya bahari.
Naomba hivi katika jina la Bwana Mungu wa mbingu na nchi. Amen.