mazaga one
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 2,514
- 4,042
Nimekaa nimewaza sana. Hivi sisi Watanzania kuna wachezaji wengi wa kutoka nchi za nje wanakuja kucheza huku kwetu, na wengineo wana viwango vizuri tu ila timu zao za Taifa wanakotoka hawapati nafasi.
Je, sisi Watanzania kupitia TFF hatuwezi kuona hii ni fursa ya sisi kuanza kuwashauri baadhi ya wachezaji kubadili Uraia wao na Kuwa Watanzania na kuanza kuwatumia kwenye Timu yetu ya Taifa Stars kama ambapo Mataifa mengine yanafanya kwa Wachezaji wanaocheza kwenye vilabu vya nchi zao.
Tuseme ukweli Kocha Ndayiragije tukimpa muda tutafika mbali nadhani tu tutafute na wachambuzi wa Soka kadhaa hasa Hawa waandishi wa habari wawe ni watu wa Karibu na benchi Letu la Ufundi. Sasa Timu inacheza na unategemea kabisa matokeo yatapatikana.
Nawasilisha.