Habari wakuu,
Bwana YESU atukuzwe na ufalme wake uje na mapenzi yake yatimizwe...
Leo naomba niwape Siri iliyopo kwenye maombi ya Kushukuru na kujitabiria...
Tumezoea Kushukuru kwa sadaka zaidi ila Leo naomba tujifunze maombi ya Kushukuru na kujitabiria...
Maombi ya Kushukuru na kujitabiria ni maombi ya Kushukuru Mungu kwa mambo ambayo Bado hujayaona...
Ikiwa na maana unajitabiria mambo ambayo hauna huku ukimshukuru Mungu kuwa umepokea...
Maombi haya kwanza kama ujuavyo nilazima uweze kujisafisha kwa damu ya YESU yaani Toba....
Alafu unaanza kumshukuru Mungu kwa mfano, unatafuta kazi wewe unaanza kumshukuru Mungu kuwa Asante kwa kuwa umeshanipa kazi, Bwana asante kwakuwa naona vile ninaenda kuchukua mshahara wangu na kiti nimekaa nikiwa kama Boss nk..
Tena uwe unavuta picha halisi ya kitu unachoomba, ikiwa ni mfano wa kazi basi na mavazi ya ofisini unayeona kabisa umevaa na umekaa kwenye kiti Cha ofisi...
Maombi haya yanahitaji uwe unaomba ukiwa na Imani kubwa,
Kama ilivyo Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo na ni bayana ya mambo yasiyoonekana...
Maombi haya ya shukurani na kujitabiria yanaweza kukufanya ukaenda kwenye viwango ambavyo hukutarajia...
Badilisha mtazamo wa kuwaza, waza mema, neno la Mungu, linasema, linda sana moyo wako maana ndipo zitokapo chemchem za uzima ...
Anza kuwaza mawazo ya kumshukuru Mungu, hata kama huoni, wewe shukuru hata kwa vile ulivyonavyo na shukuru kwa vile usivyoviona...
Ukisoma kitabu Cha Mfalme Daudi, Zaburi 118 na kuendelea ila ni vyema ukasoma chote utaona vile alikuwa akishukuru Mungu...
Anza sasa kuomba kwa kushukuru kwa kujitabiria mazuri...
Nimalize kusema, Mshukuruni Bwana kwakuwa ni mwema kwa maana fadhili zake ni za milele...