Maombi ya usiku wa manane kufunguliwa milango yako ya baraka usiku huu ikafunguke🙏🏽

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Eee Bwana ni usiku tena asante kwa neema hii. Tuliikabili siku kwa juhudi zetu huku tukiwa na tumaini ndani mwetu. Yawezekana haikuwa vile tulivyotarajia yawezekana haikuwa fungu letu kesho inaweza kuwa vile tulivyotami leo

Bwana wakati mwingine hili nililopitia leo ni kwasababu ya kusababishiwa na mtu kwa hila zake au kwa makosa yangu ya kibinadamu. Nashinda nikiwa mwenye huzuni na nalala mwili tu akili na nafsi zinakesha zikiweweseka kwa hili nilinalopitia kwenye maisha yangu

Bwana ulisema, wewe ni mwingi wa rehema, naomba rehena zako kwenye maisha yangu. Nipe zaidi ya nilichoporwa au kupoteza. Nipe zaidi ya nitamanivyo ili furaha yangu iwe kubwa kuliko wasemavyo watesi wangu juu ya yangu

Bwana kama kuomba kwangu kusipokuwa kitu sadaka, machozi na imani yangu iwe nguzo ya kunitendea wema wako kama ulivyowatendea watumishi wako waliokuwa kwenye mapito na changamoto mbalimbali ila uliwastahilisha na wakastahili kwenye maeneo ya matamanio yao

Bwana nitendee wema wako nami nistahahili nisipostahili na ukawe ushuda wa kesho njema
1731107296976.jpg
 
Giza limeipisha nuru, sasa ni siku mpya kwetu sisi waja wako. Asante Mungu kwa neema hii

Baba yawezekana nililala nikiwa na maswali na matamanio ndani mwetu nililala mwili tu ila nafsi na akili yangu ilikuwa macho usiku kucha ikiweweseka kwa hili ninalokabiliana na nalo

Bwana mwaka ulipoonza niliweka malengo juu ya jambo hili liitesalo akili yangu na kuninyima usingizi. Matamanio yangu wayajua vyema naomba unitendee wema wako Eee Bwana

Yawezekana nitamanicho sisitahili basi namba unistahilishe kwenye hili mimi mja wako Eee Bwana ila mapenzi yako yatimizwe kwangu

Bwana nitakapoikabili ratiba ya leo naomba uwepo wako uende nami Eee Bwana niendako
 
MUNGU WANGU NIREHEMU MJA WAKO

Mungu wangu naomba usiku huu ukawe usiku uliobeba jawabu hitaji langu na ukawe mwanzo wa maisha ya furaha na tabasamu kwangu

Bwana njia zako hazichunguziki za kuwajibu waja wako, wakati mwingine huwajia katika ndoto na kuwapa taswira za kesho zao njema kwa kuwapa taswira ulimwengu wa ndoto

Bwana ulishawahi kufanya hivyo kwa wateule wako uliwapa taswira na maono uliyoyapanda kwao katika ndoto nao wakayakaishi maono

Bwana wakati mwingine niombacho sisitahili ila wewe huwastahilisha wale wenye uhitaji. Bwana nistahilishe mahala au kwenye maisha ya matamanio yangu kwa utukufu wako

Bwana ulisema tuombe kwako maana wewe si kiziwi utatusikia na utatundea wema wako basi nami naomba niwe miongoni mwa watakaotendewa wema wako kwenye haja zao

Bwana yawezekana ninachopitia leo ni makosa yangu ya uchaguzi ulinionisababishia maumivu haya yawezekana sikustahili ila makosa yangu mwenyewe basi naomba huruma yako mja wak

Bwana yawezekana nimesababishiwa hili anguko kwa hila za wanadamu wala sikudhamiria. Yawezekana ni makwazo yao yamenileteleza anguko hili kwasababu nami ni mwanadamu nikakwazika kukanipelekea kuanguka kwenye hili linaloniumiza sasa.

Bwana maandiko yako yanasema, ijapokuwa utajaribiwa kwa namna mbalimbali ila utafurahi sana wakati ujao. Bwana niwe mwenye furaha nyakati zijazo kama maandiko yako yasemavyo

Naomba kesho yangu iwe kesho iliyobeba ushuhuda wa maneno HAIKUWA RAHISI ILA NI MUNGU TU alitenda kwangu nami nakawa hivi

Bwana kama kuomba kwangu kusipokuwa kitu basi huruma yako iliyojaa upendo inirehemu mimi mja wako nistahili hata kama sisistahili vile niombavyo kwako unitendee wema wako.
 
"Mpendwa naomba ufanikiwe katika mambo yote na katika afya yako, kama vile roho yako mwenyewe ifanikiwavyo." 3 Yoh 1:2

Tusiache kuombeana na kubarikiana sisi kwa sisi hii ni sehemu ya upendo mkubwa kwetu
1731107981890.jpg
♥️
 
Giza limeipisha nuru, sasa ni siku mpya kwetu sisi waja wako. Asante Mungu kwa neema hii

Baba yawezekana nililala nikiwa na maswali na matamanio ndani mwetu nililala mwili tu ila nafsi na akili yangu ilikuwa macho usiku kucha ikiweweseka kwa hili ninalokabiliana na nalo

Bwana mwaka ulipoonza niliweka malengo juu ya jambo hili liitesalo akili yangu na kuninyima usingizi. Matamanio yangu wayajua vyema naomba unitendee wema wako Eee Bwana

Yawezekana nitamanicho sisitahili basi namba unistahilishe kwenye hili mimi mja wako Eee Bwana ila mapenzi yako yatimizwe kwangu

Bwana nitakapoikabili ratiba ya leo naomba uwepo wako uende nami Eee Bwana niendako
Amina! Mungu na akakutendee sawa sawa na imani yako!
 
Ewe rafiki yangu mwema, enenda kwa imani katika ratiba yako ya siku hii mpya. Kafanikiwe katika matamanio yako na furaha iwe kwako

Baraka na neema zake Mungu Baba zikawe kwenye maisha yako. Wala usijiinamie tena kwa jambo lolote lile Mungu Baba ameyasikia maombi ya haja zako. Atakutendea wema wake katika hilo ulitamanilo liwe katika maisha yako.

Mungu Baba tunakuomba uonekane katika mahusiano yetu uchumi wetu, masomo yetu na kwenye afya zetu. Tupe kibali machoni pawatu kila tutakapokuwa tukaaminike na kukubalika.
1731108075977.jpg
 
Bwana ni usiku tena, giza limetawala anga yawezekana hata maisha yangu yana giza wala nuru haimo ndani mwangu kwasababu ya hili ninalokabiliana nalo kwa sasa linaniumiza😢

Eee Bwana ulisema wewe ni Mungu ujibuye maombi, ndani mwangu ninalo jambo Bwana nilitamanilo liwe walijua vyema. Ulisema wewe tukukumbushe na tujitie nila nawe utatukaribia katika kwikwi za matamanio ya maisha yangu

Bwana kinywa changu yawezekana kisinene vyema na kwa usahihi kilichoko ndani mwangu

Yawezekana hili ninalopitia ni makosa yangu mwenyewe au nimesababishiwa na mtu basi usiutazame udhaifu wangu ila itazame IMANI yangu ndio iwe ngao na sauti ya hitaji langu

Yawezekana niombacho sisitahili ila huruma yako iwe juu yangu, nitendee wema wako katika hili nilitamanilo liwe katika maisha yangu

Bwana wangu naomba nilalapo nilale katika tumaini na kesho yangu ikawe njema na yenye nuru na giza likaondoke katika maisha yangu.
 
Ewe rafiki yangu mwema, enenda kwa imani katika ratiba yako ya siku hii mpya. Kafanikiwe katika matamanio yako na furaha iwe kwako

Baraka na neema zake Mungu Baba zikawe kwenye maisha yako. Wala usijiinamie tena kwa jambo lolote lile Mungu Baba ameyasikia maombi ya haja zako. Atakutendea wema wake katika hilo ulitamanilo liwe katika maisha yako.

Mungu Baba tunakuomba uonekane katika mahusiano yetu uchumi wetu, masomo yetu na kwenye afya zetu. Tupe kibali machoni pawatu kila tutakapokuwa tukaaminike na kukubalika.View attachment 3147500
Amina
 
MUNGU WANGU NIREHEMU MJA WAKO

Mungu wangu naomba usiku huu ukawe usiku uliobeba jawabu hitaji langu na ukawe mwanzo wa maisha ya furaha na tabasamu kwangu

Bwana njia zako hazichunguziki za kuwajibu waja wako, wakati mwingine huwajia katika ndoto na kuwapa taswira za kesho zao njema kwa kuwapa taswira ulimwengu wa ndoto

Bwana ulishawahi kufanya hivyo kwa wateule wako uliwapa taswira na maono uliyoyapanda kwao katika ndoto nao wakayakaishi maono

Bwana wakati mwingine niombacho sisitahili ila wewe huwastahilisha wale wenye uhitaji. Bwana nistahilishe mahala au kwenye maisha ya matamanio yangu kwa utukufu wako

Bwana ulisema tuombe kwako maana wewe si kiziwi utatusikia na utatundea wema wako basi nami naomba niwe miongoni mwa watakaotendewa wema wako kwenye haja zao

Bwana yawezekana ninachopitia leo ni makosa yangu ya uchaguzi ulinionisababishia maumivu haya yawezekana sikustahili ila makosa yangu mwenyewe basi naomba huruma yako mja wak

Bwana yawezekana nimesababishiwa hili anguko kwa hila za wanadamu wala sikudhamiria. Yawezekana ni makwazo yao yamenileteleza anguko hili kwasababu nami ni mwanadamu nikakwazika kukanipelekea kuanguka kwenye hili linaloniumiza sasa.

Bwana maandiko yako yanasema, ijapokuwa utajaribiwa kwa namna mbalimbali ila utafurahi sana wakati ujao. Bwana niwe mwenye furaha nyakati zijazo kama maandiko yako yasemavyo

Naomba kesho yangu iwe kesho iliyobeba ushuhuda wa maneno HAIKUWA RAHISI ILA NI MUNGU TU alitenda kwangu nami nakawa hivi

Bwana kama kuomba kwangu kusipokuwa kitu basi huruma yako iliyojaa upendo inirehemu mimi mja wako nistahili hata kama sisistahili vile niombavyo kwako unitendee wema wako.
Amen 🙏
 
Tunakushukru Eee Mungu Baba kwa pendo lako kuu umetulinda na hatari zote za mwili na roho tumeamka salama tunazo changamoto ndani mwetu kwasababu sisi ni wahitaji Bwana

Tunaomba ututendee wema wako sisi wahitaji katika maeneo yetu ya uhitaji wetu Eee Bwana Tutakapoyakabili majukumu basi tunaomba uwepo wako uende nasi katika ratiba zetu

Tunaomba utukutanishe na neema zetu na pia wale watu uliowabebesha haja za mioyo yetu.

Tutangulie Bwana kila tutakapopagusa ikawe heri kwetu na utuepushie mbali na kila ubaya.
 
Back
Top Bottom