Mkuu Sijawahi Kuwa upande wa Kidini wowote wala sijawahi kuwa Katika upande wowote wa Waabuduo mabaya..
Instead naisoma biblia kama Refference ya Muongozo wangu na Quran pia Na Bhavagad Gita na Mahabarat pia na kitabu chochote kinacho Hubiri Amani Kwa watu wote na kurudisha Undugu TulioUharibu kwa Kudhani Tuko tofauti na kujidanganya kwa kujiwekea matabaka ya Kijinga na kipumbavu
" Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu."(Quran 41:33-34 (Suratul Fuss'ilat)
kwenye Bhagavad Gita pia kuna Aya inasema..
"Yule anayehisi furaha na huzuni ya wengine, aliye na utulivu wa ndani, asiye na ubinafsi, na anayetambua uwepo wa Mungu kwa kila kiumbe, huyo ni mtu aliye katika hali ya upendo na urafiki wa kweli." (Bhagavad Gita 12:15)
Pia
"Yeyote aliye na mawazo ya upendo kwa wote, asiye na chuki kwa yeyote, mwenye amani na uvumilivu, upole na unyenyekevu, aliye na akili imara, moyo ulio safi, na ambaye hujitolea kwa kujidhibiti na akili thabiti, anaweza kuitwa mtu aliyejitolea kwa Mungu." (Bhagavad Gita 12:13)
Namalizia kwa Kuquote mstari ndani ya Biblia..
1 Wakorintho 13:2-4,6,13
"Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo."
SIJUI MKUU UMENIELEWA HAPO..
HAKUNA TAIFA TEULE LENYE KUFURAHIA UHARIBIFU ..
WAWE WAARABU AU WAYAHUDI AU WATANZANIA