Maombi yatawala nyumbani kwa Lulu

Maombi yatawala nyumbani kwa Lulu

Midekoo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
45,757
Reaction score
246,786
BYdQt8Jh7sN.jpg

Zikiwa zimesalia siku 12 tu kabla ya hukumu yake kusomwa kufuatia kesi yake ya kuua bila kukusudia inayomkabili, taarifa zinasema maombi na sala zimekua zikitikisa nyumbani kwa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Mtu wa karibu wa msanii huyo alilidokeza , baada ya kesi hiyo kufikia katika hatua ya hukumu, hivi sasa kila siku maombi yanafanyika asubuhi, mchana na jioni, kwani kwa hali ilivyo hivi sasa, kila kitu kimo mikononi mwa Mungu.

“Si Lulu, si Mama yake, si ndugu zake, kila mmoja anaomba kwa muda wake, wakati mwingine kwa pamoja, au mmoja mmoja, wanachojua wao hatima ya kila kitu ipo mikononi mwa Mungu, ndiyo maana sala zinaelekezwa kwake,”

Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia, aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba, katika tukio lililotokea nyumbani kwa msanii huyo, Sinza Vatican mwaka 2012.

Baada ya kusikilizwa kwa ushahidi wa Jamhuri, upande wa utetezi na wazee wa mahakama, sasa hukumu hiyo itasomwa Novemba 13, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji Sam Rumanyika.
 
Mungu hachezewi,ukiwa huna shida humjui unamjua ukiwa na shida?Maombi yapi na ukahaba ule anaofanyaga?Kwanza si alitangaza kuokoka kipindi ametoka mahabusu?Mbona hakuonyesha kuendelea?
Kwenye matatizo Ndio watu humjua Angekuwa mpole na kumjua Mungu Kwenye kipindi chote nadhani angepata watetezi wengi .
 
Mungu hachezewi,ukiwa huna shida humjui unamjua ukiwa na shida?Maombi yapi na ukahaba ule anaofanyaga?Kwanza si alitangaza kuokoka kipindi ametoka mahabusu?Mbona hakuonyesha kuendelea?
Mungu si mwanadamu. Mungu anafurahi mkosefu anapoiacha njia yake mbaya na kumrudia Mungu. Pia wakati wa shida ndo wakati haswa wa kumrudia Mungu maana Mungu hashughuliki na mambo yanayowezekana kwa mwanadamu bali anashughulika na mambo yaliyo nje ya uwezo wa Mwanadamu. Tusimhukumu mtu, kazi ya kuhukumu ni ya Mungu.
 
Lakini hapo hapo tunaaswa tusimjaribu Mungu.
 
Sala zitabadilisha ushahidi uliotolewa? kama kuna incriminating evidence, sala zitaubadilisha?
All in all, IMANI INAPONYA, tuombe zaidi tunapokuwa na matatizo ya kiroho na kimwili. Naungana nao katika maombi. AMEN
 
Mungu si mwanadamu. Mungu anafurahi mkosefu anapoiacha njia yake mbaya na kumrudia Mungu. Pia wakati wa shida ndo wakati haswa wa kumrudia Mungu maana Mungu hashughuliki na mambo yanayowezekana kwa mwanadamu bali anashughulika na mambo yaliyo nje ya uwezo wa Mwanadamu. Tusimhukumu mtu, kazi ya kuhukumu ni ya Mungu.
Sio kweli Mungu anayajua yaliyo mioyoni mwetu,kwamba wakati wa shida ndio umjali afu akikutoa kwenye shida umsahau yeye anayajua yooote.Anajua akikusaidia kama utaokoka au utafanyaje yeye anayajua in advance.Pia anajua alichompangia Lulu kwenye maisha yake.
 
Mungu hachezewi,ukiwa huna shida humjui unamjua ukiwa na shida?Maombi yapi na ukahaba ule anaofanyaga?Kwanza si alitangaza kuokoka kipindi ametoka mahabusu?Mbona hakuonyesha kuendelea?
Acha kuhukumu Mkuu we umefanya dhambi ngapi?? Na je umemuomba Mara ngapi akakusikiliza?? Ni vile tu sio maarufu lkn ukute Una dhambi kubwa zaidi ya lulu .. Muache Mungu afanye Kazi yake usimuingilie
 
Mungu anatoa wakati wowote ila ni vyema zaidi ukafanya maombi kila leo na si kipindi cha shida tu by the way Mungu atakusimamia kwa hili jela si kitu kizuri mbaya zaidi kwa maisha ulioyazoe Lulu hata mwezi mmoja gerezani ni mkubwa sijui wale jamaa wakikupa mvua ya aka 10,20 au 30...itakuwaje ?
 
Kwenye matatizo Ndio watu humjua Angekuwa mpole na kumjua Mungu Kwenye kipindi chote nadhani angepata watetezi wengi .
Kwani akifanya maombi mpaka akuambie kwamba hapa yuko kwenye maombi ?? Yaani wabongo kwa kuhukumu hamjambo
 
Kwani akifanya maombi mpaka akuambie kwamba hapa yuko kwenye maombi ?? Yaani wabongo kwa kuhukumu hamjambo
Sio kuniambia matendo Ya mtu yanadhihirisha yeye ni mtu wa namna ipi wakati mwanzo alitangaza Kuokoka Huku ni kumjaribu Mungu Kikubwa ni yeye kuwa na subira lakini hili ni funzo kwa sisi wengine.
 
Kawaida ya binadamu tunajisahau, sana Mungu unafijiri hasikii tukiomba ila anaona hata nikimpa atanikufuru tuu
 
Yohana 9:31 inasema, “Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi. Yeye husikiliza mcha Mungu anayetimiza mapenzi yake.“ Na pia imesemekana kwamba “sala tu Mungu anasikia kutoka kwa mwenye dhambi ni sala kwa ajili ya wokovu.” Kwa madhumni hayo, , baadhi ya wengine huamini kuwa Mungu hawasikizi / au kamwe hajibu maombi ya asiyeamini. Kwa mkudhatha ingawa, Yohana 9:31 inasema kwamba Mungu hatendi miujiza kupitia kwa asiyeamini. Kwanza Yohana 5:14-15 inatuambia kwamba Mungu anajibu maombi kama yameombwa kwa mujibu wa mapenzi yake.
 
Back
Top Bottom