Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?
 
Jamani huu ukosoaji sasa umezidi! Kwani kwenda kwake uwanjani na kuangalia mpira ndio kunaondoa 'maombolezo'? Mkosoe Rais Kikwete kwenye mambo mengine yaliyo wazi lakini kwa hili sikubaliani na wewe Mzee Mwanakijiji.
 
the time is very critical politically, possible Yahya and other fortunetellers have advised him to, lest voters think he has started to neglect 'sposisis'
 
Kimya cha Dakika moja kilifanyika. Maombolezo ya siku 7 na bendera kupepea nusu mlingoti, the rest ni issues za judgement, a man with a mission to sell Tanzania, as a sales man, baada ya kutoa pole, unapanga na bidhaa zako bazarani kwa wafiwa ili wale wanaokuja kutoa pole wazione nao japo wanunue. Msiba umemkuta kipindi cha mauzo, as a good salesman of his nation, maadam tumeshiriki hatua zote mpaka maziko, then life goes on, biashara kama kawa.

RIP Simba wa Vita.
 
Jamani huu ukosoaji sasa umezidi! Kwani kwenda kwake uwanjani na kuangalia mpira ndio kunaondoa 'maombolezo'? Mkosoe Rais Kikwete kwenye mambo mengine yaliyo wazi lakini kwa hili sikubaliani na wewe Mzee Mwanakijiji.

Mganga wa kupindisha mbona unalia sana ?Naona umeumia sana mwananchi na mzalendo mwanakijiji ku hoji hili . Kaniwahi tu hata nilitaka kuuliza . Kama unapinga JK kukosolewa jenga hoja sasa usilie lie tu
 
SpinDoctor, binafsi sipendi kubishana na kuwa upande wowote kuhusu suala hili. Lakini tuje kimantiki zaidi kuliko ki ushabiki. Hivi kwa mfano kulikuwa na ulazima gani kulitangazia taifa kwamba tutakuwa katika maombolezo kwa kipindi cha siku saba.

Kwa tafsiri ambayo siyo sahihi sana (tafsiri binafsi) Maombolezo ni ile hali ya kuwa katika majonzi mazito kuzingatia jambo baya lililo tokea na mara nyingi ni msiba kwa maana ya kufiwa. Ili kupata maana ilete katika kiwango cha familia. Hebu niambie unadhani kweli Mhe.Vita na ndugu zake wengine walikuwepo kiwanjani kweli?

Kama ni lazima tunatakiwa kusema ukiwa mwongo usiwe msahaulifu. Hakukuwa na sababu ya kutangaza kitu ambacho wewe mwenyewe kama kiongozi huwezi kukitekeleza. Kifupi wakati mwingine kiongozi ni lazima awe mnafiki ili kulinda alichokisema bila kujali kama alichokisema anakiamini au la (busara hapa ni kujenga imani kwa watu wanaokuanimi kupitia uyasemayo) na hii ndiyo hekima ya uongozi.
 
Jamani huu ukosoaji sasa umezidi! Kwani kwenda kwake uwanjani na kuangalia mpira ndio kunaondoa 'maombolezo'? Mkosoe Rais Kikwete kwenye mambo mengine yaliyo wazi lakini kwa hili sikubaliani na wewe Mzee Mwanakijiji.

we babako akifa then within 2 days toka umzike tukuone bar umeshika fimbo ya kuchezea pool unadhani tutakuelewa??in simple terms hatuna rais serious....
 
Yakhe Mzee wakati mwengine unabowa! Hivyo kufa kwa mtu mmoja ndani ya Taifa ndio kila kitu kisimame? Basi vilabu vya Pombe na hata hii burudani ya JF vyote vifunge! Mzee una kisu na muungwana na pengine ummoja wa wale waliowaona yeye mwenyewe!
 
Jamani huu ukosoaji sasa umezidi! Kwani kwenda kwake uwanjani na kuangalia mpira ndio kunaondoa 'maombolezo'? Mkosoe Rais Kikwete kwenye mambo mengine yaliyo wazi lakini kwa hili sikubaliani na wewe Mzee Mwanakijiji.

Hivi tulitegemea kuwa JK alale uvunguni kule Ikulu kwa siku saba?
Wakuu this is the 21st cetury, life MUST go on.
 
we babako akifa then within 2 days toka umzike tukuone bar umeshika fimbo ya kuchezea pool unadhani tutakuelewa??in simple terms hatuna rais serious....

Una maana leo hii Kawawa amekuwa Babaake Kikwete? Mbona nafasi ya Kiwete ni sawa na mwananchi mwengine kwa Kawawa, Labda wanawe wa kuwazaa.
 
Mganga wa kupindisha mbona unalia sana ?Naona umeumia sana mwananchi na mzalendo mwanakijiji ku hoji hili . Kaniwahi tu hata nilitaka kuuliza . Kama unapinga JK kukosolewa jenga hoja sasa usilie lie tu

Mie hata 'silii' kama unavyodai mheshimiwa Lunyungu. Kwangu mimi 'kulialia' ni pale mnapoanza kukosoa hata mambo yasiyo na mshiko kama hili la rais kuhudhuria mechi ya mpira wa miguu. Tumempoteza mheshimiwa Kawawa tangia tarehe 31 December. Taratibu zote za kitaifa zimefanyika na mazishi tayari sasa tupo kwenye 'maombolezo ya siku saba'. Tatizo ni kuhudhuria mechi? Huwa nakubaliana na hoja za msingi aziletazo Mwanakijiji lakini sio hii...Mimi sipendi kufata upepo...Mzee Lunyungu acha 'kulialia'!
 
Maombolezi ni formality lakini mtu akishakufa basi amekufa na shughuli zinaendelea.
Unahoji Kiwete kwenda mpirani si ungeangalia Luninga wakati wa mazishi jinsi hao vigogo walivyokuwa wakipiga stori na kucheka huku swala za Kiislamu zinaendelea . AU hili wewe na Mwanakijiji hamkuliona?
 
Mkuu Pasco,

Sina la kuongeza kwenye hii hoja yako...kama Taifa tumekuwa watu wa kwenda slow kwenye kila kitu angalau kwenye hili JK ameweka nchi mbele badala ya kukaa Ikulu na kuombeleza kifo (no offence kwa wafiwa).

I wish rais angekuwa aggresive hivi hivi kwenye vipaumbele vyote vya Taifa.
 
tuige basi hata vile vizuri vya huko ugenini; hivi kama ingekuwa ni kifo cha Nyerere angeenda mpirani ndani ya siku za maombolezo ya kitaifa? AU maana ya maombolezo ya "kitaifa" imeshapotea? Kuomboleza imekuwa ni kuteremsha bendera tu na kuinamisha kichwa kwa dakika moja?
 
we babako akifa then within 2 days toka umzike tukuone bar umeshika fimbo ya kuchezea pool unadhani tutakuelewa??in simple terms hatuna rais serious....

Hapa ndipo tunaopokesea Watanzania kwenye hoja/mambo mengi sana. Tuna-personalise mambo bila ulazima wowote.

Rais amekwenda kama Ofisi sio kama Kikwete...kwanza hiyo ziara ya Ivory C. (sijui kama kuna nchi zingine zitakuja) zimetengewa Bilioni 7. Sasa kwa hela hiyo sio Rais tu na Bunge lote (bila kupewa posho..!!) lingetakiwa kufika hapo uwanja wa Taifa kuweka msisitizo zaidi.
 
we babako akifa then within 2 days toka umzike tukuone bar umeshika fimbo ya kuchezea pool unadhani tutakuelewa??in simple terms hatuna rais serious....
Mimi nilikuwa mbishi mpaka nilipoona ni picha yake haswa kwenye ile bembea.Nikaungana na wengine wengi kuhisi lipo tatizo ambalo pamoja na kujaribu kulificha ficha, linajiweka bayana lenyewe bila kusukumizwa.
 
MKJJ

Marehemu Kawawa hakuwa Nyerere, sio kwa Cheo, Utashi wala Elimu. Usichanganye viongovi hawa wawili ili kujenga tu hoja yako.

Kwa kifupi JKN alikuwa Rais tena kwa miaka zaidi ya 20, na tangu amengatuka nchi imekuwa na maraisi 3 tu baada yake....sasa tangu Kawawa angatuke/aondolewe Uwaziri Mkuu tumekuwa na Mawaziri Wakuu wangapi..?? Hizi ofisi 2 moja ni kubwa sana kuliko nyingine...in fact hatuhitaji hata kuwa na Waziri Mkuu (but that's a topic for another thread).
 
si kweli; hivi leo hii Taifa Stars ingeifunga Ivory Coast si tungeshabikia kwa kuchanga nusu bilioni nyingi kuisaidia Stars kama tulivyofanya ilipoifunga Togo; Rais hakuwa na sababu hata chembe ya kwenda kwenye mechi hii ya kirafiki isiyo na umuhimu wowote (i repeat haina umuhimu wowote ule) kwa soka la tanzania. Tunajidanganya tukifikiria kuwa kwa kucheza na Ivory Coast basi wachezaji wetu wamejifunza kitu.. Si tulifikiria hivyo hivyo walipoenda Brazili?

Ni nani leo hii akiwa amefiwa na ndugu yake ambaye amemzika siku mbili nyuma anaenda kucheza cheza na kuruka ruka kwenye michezo isiyo na maana wala mantiki?

Aliyetutangazia msiba huu "mkubwa wa kitaifa" na ambaye alishindwa kujizuia machozi ndiye wa kwanza kwenda kushangilia mechi ya mpira ambayo matokeo yake hayana maana yoyote kwa Taifa Stars wale kwa Ivory Coast zaidi ya kuwapa taste ya matumizi ya uwanja wetu mpya..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…