Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

una kikwetephobia? taarifa Rais hapew uwanjani. Taarifa hii ya Nujoma imeletwa toka jumapili na mimi nimesikia ikisomwa taarifa ya habari ya TBC Taifa juzi juaa mbili usiku.Mechi ilikuwa leo

sasa kama imetolewa jumapili ina maana gani? Haibadilishi ukweli kuwa amefanya timing mbaya. Sasa leo kama kuna watu wengine wametoa salamu zao alizipokea au zinasubiri hadi arudi in "maombolezo mode" hapo kesho!?
 
una kikwetephobia? taarifa Rais hapew uwanjani. Taarifa hii ya Nujoma imeletwa toka jumapili na mimi nimesikia ikisomwa taarifa ya habari ya TBC Taifa juzi juaa mbili usiku.Mechi ilikuwa leo

Juzi saa mbili usiku siyo jumapili,juzi ni jumamosi,uko wapi wewe?Jumapili si jana?Mechi ni leo jumatatu ama kesho jumanne?Maana kesho ndo unaweza kusema "Juzi jumapili" ndio taarifa ililetwa na mechi ilichezwa jana siku ya jumatatu.
 
Jamani si munasema mh Rais wetu hana maamuzi mazito?si munamuona
au mulitaka..... lakini kweli mmkjj hata matanga bado hayajaisha chozi la kinfiki alilolimwaga halija kauka
 
Jamani huu ukosoaji sasa umezidi! Kwani kwenda kwake uwanjani na kuangalia mpira ndio kunaondoa 'maombolezo'? Mkosoe Rais Kikwete kwenye mambo mengine yaliyo wazi lakini kwa hili sikubaliani na wewe Mzee Mwanakijiji.

Rais huyu ndiye aliyetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku saba. Yeye kama kiongozi wa Taifa alitakiwa afanye hivyo hivyo na asijihusihe na sherehe zozote katika kipindi hicho; huwezi kuomboleza na kushangilia kwa pamoja (huo ni usiku na mchana). Ndiyo maana tuna haki ya kuhoji kama kweli maneno anayotuambia huwa yanatoka moyoni mwake kweli au anayatoa tu bila hata kujua anasema nini.
 
Kikombe kipi kilikuwa kinashindaniwa kwani nilidhani tumeshatolewa kwenye michuano yote muhimu Afrika Mashariki, Afrika na Dunia. Sitaki kuamini kuwa alienda kutazama mechi ya mazoezi tu na huku tuko kwenye maombolezo - no, that would not make any sense at all.
 
MKJJ ...Maombelezo maana yake nini? Kulala nyumbani? Hivi ukiwa ktk Luninga na Uwanjani..tofauti yake ni nini?

Mbona ktk Mazishi ya wakristo kunakuwa na Pombe.(Bar ya Muda)..!!!! ni kusikitika au kufurahi...?

Mtu akishakufa watu wanatakiwa ku-move on na mambo Mengine.

Hata Nguo za Maiti hazitakiwi kuwa za Expensive..ma-suit..ma-dhahabu etc...ni shuka tu inamtosha.
 
NAsema hivi, kwetu ndingala na pombe hufanyika kwenye msiba wa mtu mashuhuri. Sio hayo tu, kimele na kibota ni usiku kucha kiasi kwamba kina kaka na dada hupashana moto migombani kwa sana tu na hata nyumba ndogo huserebuka sana kwa kisingizio cha msiba. Ni kwa sababu ya uharibifu wa kufyeka kila kitu kwa jazba kwa kutumia mikuki kwenye ndingala (ngoma ya kilio) ilipigwa marufuku labda kama inachezwa kwa low grade morale. Lakini pombe na ling'oma bado hadi kesho hasa kwa marehemu aliyekuwa mshiriki wa ngoma hiyo.

Siku 7 za msiba hazikusema tusiende kazini na tusichane nywele au kupaka mafuta vichwa vyetu. Kawawa alikuwa nambari moja Simba Sports Club na Kikwete kaenda kumuenzi baba yake kwa mchezo huo, hakucheza mwenyewe. Kipi bora, angekaa ofisini kutwanga mzigo kama kawa, au alie mfululizo siku 7 na asile wala kunywa?

Sijaona ubaya hapo.

Leka
 
MKJJ ...Maombelezo maana yake nini? Kulala nyumbani? Hivi ukiwa ktk Luninga na Uwanjani..tofauti yake ni nini?

Mbona ktk Mazishi ya wakristo kunakuwa na Pombe.(Bar ya Muda)..!!!! ni kusikitika au kufurahi...?

Mtu akishakufa watu wanatakiwa ku-move on na mambo Mengine.

Hata Nguo za Maiti hazitakiwi kuwa za Expensive..ma-suit..ma-dhahabu etc...ni shuka tu inamtosha.

Mwanakijiji,binafsi silioni kosa kabisaa kwa Rais Kikwete kwenda uwanjani kuangalia mpira..Kwamba yeye ndo katangaza msiba na maombolezo kuwa siku 7 nayo haimzuii yeye kwenda uwanjani kuuangalia mtanange ule.

Siku 7 za maombolezo haimaanishi kwamba kila kitu ndo kisimame(watu wasiende makazini walasehemu yoyote kama pale uwanjani),mbona watu walikaa kimya kwa dakika 1 kuomboleza huo msiba wa mzee Kawawa pale uwanjani??.Ni vizuri tumkosoe JK kwa utendaji wake aisee na si kwa hili la kwenda uwanjani ilhali siku za maombolezo ya msiba wa Kawawa hazijakwisha
 
Rais huyu ndiye aliyetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku saba. Yeye kama kiongozi wa Taifa alitakiwa afanye hivyo hivyo na asijihusihe na sherehe zozote katika kipindi hicho; huwezi kuomboleza na kushangilia kwa pamoja (huo ni usiku na mchana). Ndiyo maana tuna haki ya kuhoji kama kweli maneno anayotuambia huwa yanatoka moyoni mwake kweli au anayatoa tu bila hata kujua anasema nini.

maneno mazito hayo.. watu wanafikiria tunamuonea wivu kaenda kuwaona Ivory Coast!
 
Una maana leo hii Kawawa amekuwa Babaake Kikwete? Mbona nafasi ya Kiwete ni sawa na mwananchi mwengine kwa Kawawa, Labda wanawe wa kuwazaa.

wewe ndo unasema Kikwete ni sawa na wananchi wengine.Mbona hao wananchi wengine hawakukaa kwenye luninga na kututangazia msiba wa kitaifa na maombolezo kwa siku 7?think loud...JK kachemsha na watu makini hawamuoni kama yuko serious
 
MKJJ ...Maombelezo maana yake nini? Kulala nyumbani? Hivi ukiwa ktk Luninga na Uwanjani..tofauti yake ni nini?

Well.. kama maombolezo hayana maana zaidi ya neno tu, sasa kwanini taifa zima likalishwe chini kama watoto kwenye kivuli cha mwembe na kuambiwa tutakuwa na maombolezo? Kama maombolezo ni maneno tu yasiyoendana na matendo yoyote ya kuomboleza next time mwambieni asitutangazie kabisa abakie nayo huko huko Magogoni!
 
Siku 7 za maombolezo haimaanishi kwamba kila kitu ndo kisimame(watu wasiende makazini walasehemu yoyote kama pale uwanjani),mbona watu walikaa kimya kwa dakika 1 kuomboleza huo msiba wa mzee Kawawa pale uwanjani??.Ni vizuri tumkosoe JK kwa utendaji wake aisee na si kwa hili la kwenda uwanjani ilhali siku za maombolezo ya msiba wa Kawawa hazijakwisha

you guys are missing the whole point; hakuna mtu aliyedai tukiomboleza kitaifa manake watu wasiende kazini, wasitabasamu, wasicheke au wasinywe tutakuwa wajinga kufanya hivyo hata siku babangu alipokufa tukiwa tunasubiri kuzika watu walikuwa wanacheka kwa kumbukumbu ya mambo fulani n.k

Sasa, kama msiba wa kitaifa hauendani na maombolezo ya kitaifa kwanini mtutangazie? Kama vinavyotakiwa kuomboleza ni bendera na bunduki basi next time wateremshe tu bendera tutajua tumefiwa.
 
Mzee Mwanakijiji kwenye hili umemiss the points 'mbili muhimu' kwenye 2 different issues.
1. Umechanganya matanga, na maombolezo. Matanga ndicho kipindi cha kutulia na kutafakari, maombolezo ni to observe recognition ya msiba husika. Baada ya mazishi, huwa kuna matanga, siku hizi tanga ndugu, mhusika wa matanga akionekana kwenye burudani hiyo ni issue nyingine. Kawawa siyo ndugu na JK, hivyo JK siyo sehemu ya matanga Mzee Kawawa, unless anabaki kwa ridhaa yake. Baada ya mazishi, watu hutangaziwa matanga, wahusika huendelea na matanga na wasio husika husambaa na kuendelea na shughuli zao za kila siku, life goes on. Ndivyo alivyofanya JK.
2.Point ya pili iliyoimisi, ni kuhusu significance ya hii mechi, kama ilisoma jibu langu la awali, nilisema this was not a friendly match, this was a sales strategy. Hii jamani sio mechi ya kirafiki, hii ni biashara kubwa ahead. JK sio amekwenda kurukaruka uwanjani, amekwenda kuisell Tanzania ili ulimwengu u buy Tanzania. Hii ni sales campaign ya uwanja wetu kwenye on coming kombe la dunia ndio maana nikakuambia its a matter of judgement. It has nothing to do with soccer development in Tanzania, its pure bussiness.

JK pamoja na maroroso yake, tusikabe mpaka kona, kwenye mazuri machache ama tuya-acknowdge ama tuyaignore na kujinyamazia ila 'Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni'.
 
Jamani huu ukosoaji sasa umezidi! Kwani kwenda kwake uwanjani na kuangalia mpira ndio kunaondoa 'maombolezo'? Mkosoe Rais Kikwete kwenye mambo mengine yaliyo wazi lakini kwa hili sikubaliani na wewe Mzee Mwanakijiji.
Mimi nadhani umeamua kumtetea Kikwete kwa sababu hafifu sana.

Alietangaza kuwa nchi iko kwenye maombolezo ni JK mwenyewe. Alietangaza kuwa bendera zitapepea nusu mlingoti ni JK mwenyewe. Sasa kwanini asionyeshe kuwa kweli Taifa liko msibani? Kwanini atafute njia za kushangilia, kusherehekea na kuburudika na ushindi (hadharani) endapo timu ya Taifa ikishinda? Angeshangilia kwa kujificha basi!!

Mkuu, JK ni mtu wa mwisho kutegemewa kuwa mpirani au kwenye burudani nyingine zozote hadharani. Si kwa kuwa akifanya hivyo anaharibu maombolezo, bali anakiuka majonzi aliyotaka kuonyesha Taifa na heshima aliyoitoa kwa marehemu. Angekuwa hamaanishi kuwa nchi inatakiwa kuomboleza, angeamua tu kusema "Taifa limepoteza kiongozi mahiri..... endeleeni kazi kama kawaida". Ama sio Mkuu?

Ni desturi za kibinadamu tu. Kama sio protocol.
 
Asilimia kubwa ya waTz hususani wasomi reasoning capacity yao ni ndogo sana but wao wenyewe hujiona ni wajanja na ndiyo maana mtu akiwa mjanja kidogo tu nakuligundua hilo basi atawadrive the way anavyotaka na kukaapembeni akicheka maana anaweza sema kitu kwa kutegesha uone respond ya Great thinkers....WATZ WANAJUDGE NANI KASEMA NA SIO KASEMA NINI HASA NA KINA ENDANA NA TUKIO AU MAANA HALISI?????........na WANASIASA WATZ wanalijua sana na ndoo maana wataendelea kutesa kwa kwenda mbele.....
" IF YOU REAL HAVE A BRAIN YOU WILL KNOW WHAT I REAL MEAN"
BABA na wewe umeshakubali kuwa 'Asilimia kubwa ya waTz reasoning capacity yao ni ndogo sana' kwanini na wewe bado unawafumbia mafumbo?. Kwa nini usimtaje huyu ' mtu akiwa mjanja kidogo tu nakuligundua hilo basi atawadrive the way anavyotaka na kukaapembeni akicheka maana anaweza sema kitu kwa kutegesha uone respond ya Great thinkers' uone utakavyoshukiwa!.

Mimi I belong kwenye hili kundi kubwa la watanzania wengi, ningeomba basi utusaidie kutufafanulia " IF YOU REAL HAVE A BRAIN YOU WILL KNOW WHAT I REAL MEAN" -what do you real mean?.
 
Jamani huu ukosoaji sasa umezidi! Kwani kwenda kwake uwanjani na kuangalia mpira ndio kunaondoa 'maombolezo'? Mkosoe Rais Kikwete kwenye mambo mengine yaliyo wazi lakini kwa hili sikubaliani na wewe Mzee Mwanakijiji.

Acha dogma. Ndo maana ya mwanasiasa. Calculate your every step.

Tuliambiwa sherehe na burudani zote zimepigwa marufuku. Hata sherehe za New year ziliwekewa gavana. Iweje yeye aende kucheka-cheka kiwanjani.
 
Mzee Mwanakijiji kwenye hili umemiss the points 'mbili muhimu' kwenye 2 different issues.
1. Umechanganya matanga, na maombolezo. Matanga ndicho kipindi cha kutulia na kutafakari, maombolezo ni to observe recognition ya msiba husika. Baada ya mazishi, huwa kuna matanga, siku hizi tanga ndugu, mhusika wa matanga akionekana kwenye burudani hiyo ni issue nyingine. Kawawa siyo ndugu na JK, hivyo JK siyo sehemu ya matanga Mzee Kawawa, unless anabaki kwa ridhaa yake. Baada ya mazishi, watu hutangaziwa matanga, wahusika huendelea na matanga na wasio husika husambaa na kuendelea na shughuli zao za kila siku, life goes on. Ndivyo alivyofanya JK.

Vizuri. Hoja yako ingekuwa na nguvu na wala tusingebishana kama aliyekufa hakuwa Kawawa. Unachosema ni kweli kwenye misiba yetu ya kawaida. Kawawa kwa Kikwete alikuwa ni karibu zaidi na ndugu. Vinginevyo nini kilichomfanya kutangazia taifa msiba wa kitaifa? Na kama suala la msiba wa Kawawa ni swala la familia na familia ndiyo wanatakiwa kuombeleza ni kitu gani kiliwafanya serikali kusimamia msiba na mazishi badala ya kwenda kutoa pole tu na kuondoka zao msibani? Ni kitu gani kilimgusa Kikwete kwenda asubuhi na mapema kwenda kumuona mtu asiye ndugu yake akiwa hospitali tena yeye na mkewe? Unless.. unless Kawawa hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe.. you tell me. Kwanini serikali imejihusisha kwa karibu kuanzia ugonjwa, kuaga, mazishi na hata kututangazia maombolezo?

2.Point ya pili iliyoimisi, ni kuhusu significance ya hii mechi, kama ilisoma jibu langu la awali, nilisema this was not a friendly match, this was a sales strategy. Hii jamani sio mechi ya kirafiki, hii ni biashara kubwa ahead. JK sio amekwenda kurukaruka uwanjani, amekwenda kuisell Tanzania ili ulimwengu u buy Tanzania. Hii ni sales campaign ya uwanja wetu kwenye on coming kombe la dunia ndio maana nikakuambia its a matter of judgement. It has nothing to do with soccer development in Tanzania, its pure bussiness.

Ni nadharia ya ajabu kufikiri kuwa tutaitangaza nchi kwa mechi ya Ivory Coast! Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!! Kama lengo ni kutangaza nchi kuna njia nyingine rahisi zaidi na wala hazimuhitaji rais kuitangaza. Yaani miaka minne yote ya safari zote na kukutana na kila aina ya watu huko majuu bado hajaitangaza Tanzania na kuiuza nchi ndio ije leo kwenye mechi ya Ivory Coast?

If this was a business strategy.. then it is the most ill-thought business strategy ever! And if I had a chance to know who came up with this idea I would parade him in public and do something better left unmentioned!

You really think this was a good business strategy?

Nitakuambia kitu kingine, kama suala lilikuwa ni kutangaza uwanja kuna njia nyingine za kuutangaza.. otherwise.. nijibie swali hili:

Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?

JK pamoja na maroroso yake, tusikabe mpaka kona, kwenye mazuri machache ama tuya-acknowdge ama tuyaignore na kujinyamazia ila 'Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni'.

wakati hata kona zinakabwa kama hazipigwi moja kwa moja!
 
jamani huu ukosoaji sasa umezidi! Kwani kwenda kwake uwanjani na kuangalia mpira ndio kunaondoa 'maombolezo'? Mkosoe rais kikwete kwenye mambo mengine yaliyo wazi lakini kwa hili sikubaliani na wewe mzee mwanakijiji.

heri mimi sijasema
 
Kikwete mzee wa mabembea endeleza burudani kama cloudzzzzz efuem...
waacheni wafu wazike wafu wao.
tulio hai wacha tuendelee kula raha hadi umauti utakapotukumba
 
Back
Top Bottom