Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani


hakwenda kama Rais kwani hakuna ulazima wa Rais kwenda; ni kama kwenda kufungua hoteli ile ya Arusha ambapo hakukuwa na ulazima wake. Kama alitakiwa kwenda Rais angeenda Makamu wa RAis au hata Waziri Mkuu.. Au angalau ingekuwa ni mechi ya kugombania nafasi fulani au point fulani muhimu..
 


Mkuu,

Hapa tuko pamoja, kama suala ni kuendeleza soka basi tunafanya mambo kinyume kabisa...tulitakiwa tuanzie chini, mashuleni, vyuoni n.k. Nakubaliana na wewe kabisa; hata kuwa na kocha wa Taifa Mbrazili au atoke Mbinguni...ili tuinue soka lazima tuazie kwenye grass roots.

Ila hapa kwa mujibu wa post yapo hapo juu; hoja sio hii.

Ni nani leo hii akiwa amefiwa na ndugu yake ambaye amemzika siku mbili nyuma anaenda kucheza cheza na kuruka ruka kwenye michezo isiyo na maana wala mantiki?

I beg to differ, naona na wewe una-personalise hii issue. Rais sio Mjomba wa nchi, Rais ni mtumishi wa nchi. Leo hii hata kama akifiwa yeye binanfi (God forbid) Taifa likimuhitaji; anatakiwa aweke majonzi yake pembeni akalitumikie Taifa.

Nitasita kujibu maoni yako kuhusu mchozo wa Footbal kwa sababu hapa kwa uelewa wangu hoja sio umuhimu wa football kwa taifa wala iwapo football ni mchezo makini au ni mchezo wa "kucheza cheza na kuruka ruka"


Taifa kuwa msibani haimaanishi kabisa kuwa Ofisi ya Rais inasimama kulitumikia Taifa.

Hii spirit aliyonyeshwa na ofisi ya Rais inahitajika kwenye kila Sekta ya Taifa letu.
 

MKJJ

Unaangalia ziara hii ya Ivory Coast kwenye angle moja tuuu "FOOTBALL" angalia kwa pande zote ambazo zimepelekea Serikali kutenga Tshs Bilioni 7 (nisieleweke kuwa naunga mkono matumizi haya). Ndio maana nikasema kwa gharama hizo I don't care tumefiwa jana au leo; life has to go on.

Kama Taifa tumeadhirima vya kutosha na desturi za aina hii. Labda sasa wakati umefika tubadilike.
 

well.. hakuwa Nyerere ni kitu ambacho mtu yeyote anakijua lakini mchango wake kwa Tanzania huwezi kulinganisha na wa Msuya, Warioba, Malecela, Lowassa, Salim wala hata Sokoine. Historia ya Tanzania tuijuayo sasa hivi haiwezi kuandikwa bila majina ya Nyerere na Kawawa kutajwa kwenye sentensi moja.

Na nafasi yake haiwezi kupimwa kwa vipimo unavyotumia. Aliyevuma baharini alikuwa Papa (Nyerere) na wengine walikuwepo.. Tatizo yawezekana unaamini sana stori za caricature ya RMK ambayo wengi wetu tulikuwa tunaamini.

nitakupa mfano..


Hilo la msaada wa Kawawa kwa Mandela hata Mandela mwenyewe alirudia alipokuwa kwenye kesi yake mwaka 1964. Alisema hivi kwenye hili hotuba ya "Nimejiandaa kufa"


utaona kuwa msaada wa Tanganyika unatajwa kwanza na ni nchi pekee ambapo aliona ulazima wa kutaja majina yote mawili la Nyerere na Kawawa! Of course wengine watasema Nyerere ndiye aliyestahili..!

No sir, mchango wa Kawawa hatujaungalia vizuri zaidi na hili limethibitishwa na kitendo cha kpuuzi cha JK kwenda mpirani wakati nchi iko kwenye maombolezo ya kitaifa. Yes I said "cha kipuuzi"!
 

I beg to differ, naona na wewe una-personalise hii issue. Rais sio Mjomba wa nchi, Rais ni mtumishi wa nchi. Leo hii hata kama akifiwa yeye binanfi (God forbid) Taifa likimuhitaji; anatakiwa aweke majonzi yake pembeni akalitumikie Taifa.

Atakuwa ni RAis mpuuzi kweli kama baada ya kufiwa na akaamua kwenda kushangilia netball kwa ababu taifa linamhitaji! Kama kushangilia mechi isiyo na umuhimu wowote ndio kumhitaji Rais basi tumekwisha!



Taifa kuwa msibani haimaanishi kabisa kuwa Ofisi ya Rais inasimama kulitumikia Taifa.

Kama kwenda kushangilia mechi kama hii ndiko kutumikia taifa basi tumekwisha!


Hii spirit aliyonyeshwa na ofisi ya Rais inahitajika kwenye kila Sekta ya Taifa letu.

Not really.. roho ya namna hii inahitaji kukemewa!
 
we babako akifa then within 2 days toka umzike tukuone bar umeshika fimbo ya kuchezea pool unadhani tutakuelewa??in simple terms hatuna rais serious....

Kazungukwa na banyamulenge na mafisadi kibao unafikiri nini?
 
SO hoja hapa ni:

1. taifa kama taifa kuto 0bserve ''maombolezo" kama tulivotangaziwa, au
2. Rais kwenda kuangalia mpira wa kirafiki kati ya Taifa stars na Ivory Coast?
 
Asilimia kubwa ya waTz hususani wasomi reasoning capacity yao ni ndogo sana but wao wenyewe hujiona ni wajanja na ndiyo maana mtu akiwa mjanja kidogo tu nakuligundua hilo basi atawadrive the way anavyotaka na kukaapembeni akicheka maana anaweza sema kitu kwa kutegesha uone respond ya Great thinkers....WATZ WANAJUDGE NANI KASEMA NA SIO KASEMA NINI HASA NA KINA ENDANA NA TUKIO AU MAANA HALISI?????........na WANASIASA WATZ wanalijua sana na ndoo maana wataendelea kutesa kwa kwenda mbele.....
" IF YOU REAL HAVE A BRAIN YOU WILL KNOW WHAT I REAL MEAN"
 
Lakini Kikwete ni kawaida yake hata wakati alipokuwa ziarani Uingereza alikutana na Watanzania kwa muda wa nusu saa na baadaye alikwenda kuangalia mpira wa timu yake ya Spurs.(Kipenzi cha roho). Huyo ndiye rais mliyemchagua. Watanzania walisafiri kwa matreni kutoka kila sehemu zaidi ya masaa kadhaa kumbe yeye alikuwa na hamsini zake.

Na hiyo ni tabia yake hawezi kuacha na utendaji wake wa kazi ndio hivyo hivyo goi goi. Sijui atakwenda kubembea wapi safari hii.
 
Hivi kuna mtu anakumbuka mara ya mwisho tulipokuwa na maombolezo ya kitaifa ilikuwa ni lini?
 
Hivi hizo 7 billioni zilikuwa kwenye bajeti na kupitishwa na bunge au ndio dharura yenyewe? Sikuona dharura kule Temeke Hospitalini.
 
It's just not a good look for him to be out there at a football game while the country is supposedly still observing seven days of mourning. He should have just stayed at home and watched the game if it was that serious. It is things like this that call into question his judgement as a leader.
 

Kwani umesahau Jakaya aliposema asilimia 70 wanafuata upepo. Sasa angalia wewe mwenyewe sijui unafuata upepo upi?
 
It's just not a good look. He should have just stayed at home and watched the game. It is things like this that call into question his judgement as a leader.

ndio tatizo la watu walichoshindwa kusoma nilichoandika na wewe umekinyambulisha vizuri. Sina tatizo kama Rais angeamua kuangalia mpira huo kama mamilioni ya Watanzania wengine kwenye luninga.

Kwa kwenda kwake mpirani wakati yeye mwenyewe katutangazia msiba mkubwa wa kitaifa kumetrivialize umakini wake na zaidi ya yote umeonesha kuwa anasukumwa na vitu vidogo vidogo tu! Aliwahi kukatiza ziara kadhaa muhimu na kwenda misibani hapo nyumbani na kurudi na kuendelea na ziara hizo..

Kwa sababu huko mbeleni watakufa watu kwenye janga moja na jioni yake mtamuona anaangalia watu wanacheza ready!
 
MKJJ; Mzee Kawawa RIP si nasikia alikuwa upande wa JK wakati wa uteuzi wa mgombea urais?Historia ya Mzee Kawawa kuhusiana na huu ufisadi uliopamba moto iko vipi?
Mh Rais naona alikuwa na sababu "Nzito" za kutokuikosa mechi hiyo?
Duh!Ama kweli mla nawe si mfa nawe.
 
hii intuthibitishia kuwa sisi ni wanafiki wakubwa ,tunajidai kuwalilia watu ilhali moyoni hatuwafeel,binafsi naamini haikuwa sahihi kabisa kwa rais kuongoza kushangilia wakati taifa lipo kwenye majonzi angeangalia kwenye tv basi kama alikuwa na shida ya kumuona drogba angeenda tareha 7 watakapocheza na rwanda hii isingeleta picha mbaya ila kwa leo MR PRESIDENT im sorry to say this but umechemsha
 
Leo hii Sam Najuma ametuma salamu hizi🙁tanzania daima)



sasa alipopewa taarifa hiyo akiwa uwanjani au Ikulu alifanya nini. Sitoshangaa alikataa kuifungua isije ikamharibia mood yake ya kushangilia taifa stars!
 

Hapa unakosea. Mechi ni muhimu sana babu mbili. Moja, viwango vya FIFA hupimwa katika mechi zote ikiwemo za kirafiki. Mbili, Ivory Coast ni timu iliyo katika kombe la Dunia na hivy kuna umuhimu wa kuwavutia weeke kambi hapa Tanznaia kala ya kwenda Afrika Kusini na hivyo nchi kufaidika na kuitangaza.

Inawezeana Rais nkwenda ni tatizo lakini umuhimu wa mechi ni mkubwa sana kwa Taifa.
 
Leo hii Sam Najuma ametuma salamu hizi🙁tanzania daima)




sasa alipopewa taarifa hiyo akiwa uwanjani au Ikulu alifanya nini. Sitoshangaa alikataa kuifungua isije ikamharibia mood yake ya kushangilia taifa stars!

una kikwetephobia? taarifa Rais hapew uwanjani. Taarifa hii ya Nujoma imeletwa toka jumapili na mimi nimesikia ikisomwa taarifa ya habari ya TBC Taifa juzi juaa mbili usiku.Mechi ilikuwa leo
 

Mi nafikiri kuna tofauti kati ya maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti. Nafikiri kinachofanyika ni bendera kupepea nusu mlingoti lakini kama ni maombolezo huwezi omboleza kwa burudani (kwenda mpirani).
1999 baada ya kifo cha Nyerere tulikaa mwezi mzima bila mipira kuchezwa wala TV na vyombo vya habari kutangaza au kuonesha burudani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…