Kaulimbiu ya maonesho ya mwaka huu ni “Ushirikiano wa Huduma Unakuza Maendeleo, Uvumbuzi wa Kijani, Unaleta Mustakabali Mzuri”. Ikilinganishwa na awamu zilizopita, maonyesho ya mwaka huu ni makubwa zaidi, na yameshirikisha takriban kampuni 2,400 ikiwemo zaidi ya makampuni 400 kati ya makampuni 500 makubwa zaidi duniani, na kuwavutia watu laki 2.5.
Maonyesho hayo pia yamevutia ushiriki wa nchi za Afrika. Kutoka vitu vya kisanii kutoka Togo na mafuta ya mikono ya maparachichi kutoka Ghana, hadi mradi wa Burundi wa “Jukwaa la Biashara Mtandaoni”, nchi za Afrika zinatarajia kukuza ushirikiano na China katika biashara ya huduma.
Kwa mujibu wa takwimu, tangu mwaka 2017, wastani wa ongezeko la uagizaji wa huduma za China kutoka Afrika umekuwa asilimia 20 kwa mwaka, na ushirikiano wa biashara ya huduma kati ya pande hizo mbili umetoa ajira laki nne kwa nchi za Afrika kila mwaka.
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China yalianzishwa mwaka 2012. Katika miaka 10 iliyopita, thamani ya sekta ya huduma nchini China imeongezeka kwa mara 1.49, na thamani ya jumla ya huduma zinazoagizwa na China kutoka nchi za nje imezidi dola trilioni 4 za kimarekani.
Maonyesho hayo si kama tu yanatoa jukwaa kwa makampuni ya China kutumia kikamilifu masoko makubwa ya ndani na ya kimataifa, bali pia yanatoa fursa kwa makampuni ya nchi nyingine duniani kuingia kwenye soko la huduma la China. Wakati huu ambao dunia inakabiliwa janga la UVIKO-19 na kudidimika kwa uchumi, Maonyesho hayo yana umuhimu zaidi katika kuhimiza ufufukaji wa uchumi wa dunia.
Maonyesho Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China ni kama kioo, yanaakisi ukuaji wa wenzi wa kibiashara wa China. Kwa China, kuendeleza ushirikiano wa biashara ya huduma si kama tu ni sehemu muhimu ya juhudi za kuanzisha uhusiano mpya wa biashara ya kimataifa wenye haki na manufaa ya pamoja, bali pia ni utekelezaji wa nia ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Kwa dunia, China kuendeleza ushirikiano wa biashara ya huduma kunasaidia kukabiliana na changamoto za kimataifa, na kutachangia zaidi maendeleo ya uchumi wa dunia.