Maongozi yangu ya kuacha kujichua yalitoka kwa mwanamke

Maongozi yangu ya kuacha kujichua yalitoka kwa mwanamke

Ras John I

Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
39
Reaction score
22
Ilianza kama utani tu nikiwa nimekaa mwenyewe chumbani kwangu wakati nimeingia kwenye mitandao ya kijamii kuchati na kusoma yanayoendelea humo, ila baada ya muda nikaona mbona hamna jipya humo nakiangalia salio la bando nikakuta nina bando la kutosha, sasa nikaanza kujiuliza nifanye nini kingine tena kwenye simu yangu!!????

Basi nikaamua kuangalia na kupakua picha na video za ngono nikawa naangalia mara ya kwanza sikuona madhara makubwa sana kwangu niliona kama ni za kawaida tu, lakini nikiwa kijana ambaye sikuwa nimekutana na mwanamke toka nimezaliwa nilijikuta najiingiza kwenye dibwi kubwa ambalo si rahisi kujitoa lakini kwa wakati ule sikulitambua hilo.

Ghafla kakaanza katabia kila nikipakua picha zile na video za ngono nikaanza kujichua (kufanya punyeto) mara ya kwanza ya pili, ya tatu basi ikawa hivyo ikawa ni tabia sasa kila siku lazma nifanye kile nilichokuwa nakifanya jana ikafika pahala nikaona mbona ni kitu cha kawaida hiki!?

ILA SIKU ZILIVYOZIDI KWENDA HALI YANGU YA KIAFYA IKAANZA KUBADILIKA ...
(a) Mwili ukadhoofika na kushindwa kusimama kwa muda mrefu kwani viungo vyote vya mwili vikawa vinauma mpaka UTI wa mgongo nao ukawa unaleta shida mno.

(b) Nikaanza kupoteza kumbukumbu, hivyo nikawa msahalifu hata kwa jambo ambalo niliambiwa asubuhi nikajikuta jioni nimeshasahau HII ILIPELEKEA KUSHUKA KWA UWEZO WANGU DARASANI kiasi cha walimu kuniita na kuniuliza ni nini kilikuwa kinanisibu.

(c) Nikaupoteza utu wangu kiasi cha kufikia wakati sioni Thamani ya mwanamke katika maisha yangu kwa kudhani kuwa kile kitu ambacho nilipaswa kukipata kwa mwanamke sasa naweza kukipata nikiwa mwenyewe chumbani Kwa kutumia simu yangu ya mkononi au Laptop yangu (KOSA KUBWA HILI)

(d) Kutokujiamini kukazidi kuongezeka mwilini mwangu kiasi cha kukimbia wanawake haTa Kama tunafanya wote kazi za makundi darasani hata uwezo wawangu wa kujieleza sehemu yeyote ukapptea kabisa.

(e) Siwezi kusahau mara ya kwanza kukutana na mwanamke kimwili kwani sikuweza kufanya chochote akiwa pale kitandani taswira zilizokuwa zikinijia ni za zile video za ngono nilizokuwa nikiangalia kiasi kwamba baada yeye kuvua nguo zake mimi nikawa tayari nimeshamaliza kila kitu hivyo kumuacha dada wa watu akiwa na kiu wakati mimi nilishamaliza kiu Yangu tayari nilishamaliza.

(f) Sikuwa tofauti na Teja wa madawa ya kulevya kwa tulikuwa tunacheza mipira tofauti kwenye uwanja mmoja ilifika pahala nikimuona mwanamke sehemu yeyote ile naweza kumvua nguo kwa kutumia fikra zangu na kumaliza shida zote.

(g) Nilitumia nguvu nyingi za kifikra kumtoa mwanamke darasani au barabarani kimawazo na kumleta chumbani kwangu kwa ajili ya kujichua kumbe fikira hizi ningeweza pia kuzitumia kufanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi kama tu ningeztumia katika mfumo ulio chanya.

[HASHTAG]#UKWELI[/HASHTAG] usiopingika kuwa kuwa asilimia karibu 80% ya vijana na wazee ni mateja wa picha na video za ngono na hizi zimekuwa na madhara makubwa kiafya na kiakili kwao, na sasa tunapokuja kuongelea MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME tunaweza kujua ni wapi tuanzie.

[HASHTAG]#JINSIYAKUACHA[/HASHTAG].
Zipo njia nyingi za kuacha uteja huu ambazo zimekuwaiwa na wataalamu mbalimbali zikishauriwa na wataalamu mbalimbali jinsi ya kuachana na uteja huu, mimi nilijaribu nikaacha kwa siku mbili na baada ya muda nikarudi kulekule nilikotoka.

Njia rahisi na ngumu ya kuacha uteja wa picha na video za ngono pamoja na kujichua au kufanya punyeto ni KUAMUA KUACHA KWA HIYARI YAKO MWENYEWE.

>Siwezi Kusahau mara ya kwanza nilimona mwanamke ambaye sikuwahi kuongea nae ila nilimpenda na nikajiukiza hata kama nikamwambia nampenda akanikubalia je ataweza kudumu na mimi na haya matatizo yangu niliyonayo...? Hivyo kabla ya kumueleza yule mwanamke HISIA zangu kwanza ilibidi NIPAMBANE NA HALI YANGU KWANZA na huo ndio ukawa mwisho wa uteja wangu.
Hivyo mwanamke ndiye aliyekuja kuwa mwokozi wangu.

CHAGUA SASA NJIA GANI UPITE....

RasJohn
 
Mimi nimejitahid kuacha kwa miezi 6 kwa sasa....ila kuacha hii kitu inahitaji roho ngumu sana yan sana kupita maelezo maana mimi nilikua naacha siku 3 narudi...ila saiv nina miezi 6...
Kuacha ghafla ni vigumu,na amini tu kwamba kuiacha punyeto kabisa nako ni kugumu vilevile ila kupiga mara moja ka hamu baada ya miezi mitatu sio mbaya{sisemi iendelee kufanywa ila kama mtu zile fikra zinakujia bado na huwezi kuzishinda}...nimeowa ila still kuna wakati huwa najilipua kimoja kuchangamsha damu na maisha yanaendelea ila sasa ni kipindi kidogo sijafanya.ila punyeto ni hatari sana sio jambo la kujaribu kwa ambaye hakuwahi kufanya.
 
Kuacha ghafla ni vigumu,na amini tu kwamba kuiacha punyeto kabisa nako ni kugumu vilevile ila kupiga mara moja ka hamu baada ya miezi mitatu sio mbaya{sisemi iendelee kufanywa ila kama mtu zile fikra zinakujia bado na huwezi kuzishinda}...nimeowa ila still kuna wakati huwa najilipua kimoja kuchangamsha damu na maisha yanaendelea ila sasa ni kipindi kidogo sijafanya.ila punyeto ni hatari sana sio jambo la kujaribu kwa ambaye hakuwahi kufanya.
Nina miezi 6 yani sitaki hata kufikiria kurudi ila inahitaji uwe umeamua haswa kuacha..yan umedhamiria
 
Hayo matatizo mengine ni uzembe wako tu sio punyeto..kama namba 1
 
Kwahivyo sahiz shughuli hiyo unaiweza ama ndo kama zaman tyuu
mkuu umeiponda sana punyeto humu kwani imekukosea nini, wewe una matatizo yako tu na wala sio punyeto. punyeto ina faida lukuki kuliko madhara yake
 
Back
Top Bottom