Dickson Ng'hily
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 473
- 508
Na Dickson Ng’hily
Utangulizi
Katika jamii yoyote inayothamini taaluma na uadilifu wa kitaaluma, shahada za heshima (Honorary Degrees) hutazamwa kwa heshima na umakini mkubwa. Hata hivyo, hali hiyo imeanza kuporomoka kwa kasi baada ya watu kuona ni sehemu ya kupata ‘taito” ya udaktari.
Siku za hivi karibuni kuna baadhi ya Watanzania wamepokea na nimeona kwenye baadhi ya machapisho mtandaoni, wakitumia hizo ‘taito’ za udakitari walizopata baada ya kupewa "digrii za heshima" kutoka taasisi inayojulikana kama London Institute of Skills Development (LISD).
Makala hii inalenga kufanya uchambuzi wa kina, kwa kutumia hoja za kimantiki na vielelezo hai, juu ya hali hii inayoathiri hadhi ya taaluma, udanganyifu wa kijamii, na kuporomoka kwa viwango vya maadili ya uongozi na elimu nchini.
1. LISD: Taasisi isiyo na mamlaka ya kitaaluma
Kwa uchunguzi uliofanywa kupitia tovuti ya Office for Students UK, LISD haijatajwa popote kama taasisi ya elimu ya juu yenye mamlaka ya kutoa shahada ya aina yoyote ile. Vilevile, haipo kwenye orodha ya vyuo vinavyotambulika na Ofisi ya Udhibiti wa Elimu ya Juu Uingereza (Ofqual), wala Quality Assurance Agency for Higher Education (QAA).
Kwa kifupi:
•LISD sio chuo kikuu.
•Haina mamlaka ya kisheria ya kutoa shahada yoyote (Bachelor’s, Master’s au PhD).
•Imejisajili kama taasisi ya mafunzo ya kozi fupi (professional skills).
Hii ina maana kuwa vyeti vya digrii kutoka LISD havina hadhi wala uzito wa kitaaluma katika mfumo rasmi wa elimu duniani.
2. Mfumo wa RPL wa LISD: Kigezo cha kisanii cha kutunuku vyeo
LISD hutoa "digrii za heshima" kupitia mfumo uitwao Recognition of Prior Learning (RPL). Lakini mfumo huu hutumika kwa lengo la kutambua uzoefu wa kazi kwa ajili ya kujiunga na masomo rasmi – sio kama mbadala wa digrii kamili, na kamwe hauwezi kuwa msingi wa kutunukiwa Udaktari wa heshima.
Pia inamfumo wa Nomination ambapo mtu aweza kupendekezwa jina lake au mwenyewe mhusika kujipendekeza kwa kujaza fomu maalum ukiambatisha na CV yake na andiko ama ushahidi wa kazi ulizofanya plus malipo na kisha ‘mchakato’ huanza.
Katika LISD:
•Hakuna mchakato wa kisomi (peer review, panel ya seneti, au bodi ya wasomi).
•Kama nilivyosema hapo juu, mtu anajaza fomu, anaambatanisha CV, analipa fedha (takriban milioni 15 Tsh) kisha anatangazwa “Daktari.”
•Huu si utambuzi wa kisomi, bali ni biashara ya vyeo.
3. Watanzania waliopokea "digrii" kutoka LISD na matumizi ya cheo cha 'Dk'
Baadhi ya Watanzania maarufu waliopokea digrii hizi kutoka LISD hivi majuzi ni pamoja na:-
•Monica Joseph - CEO wa Mokasi Medical System,
•Hilda Nakajumo- Group Broadband Lead wa Airtel Africa,
•Fuad Ahmed Edha - Group CEO wa Azania Group,
• Bakari S. Machumu - CEO wa BSM Washauri.
Nimeona kwenye chapisho moja kutoka BSM Washauri kwenye ukurasa wake wa LinkedIn, sasa wanatambulika kwa ‘taito’ ya "Dk." Jambo ambalo kimsingi linawapa faida ya kijamii, kisiasa na hata kiuchumi kwa kutumia hadhi ya taaluma ambayo hawajasomea wala kustahili kwa mujibu wa taratibu za elimu ya juu.
4. Matumizi ya vyeo visivyo halali: Udanganyifu wa kijamii na kisera
Kwa mujibu wa sheria nyingi za elimu duniani, kutumia cheo cha kitaaluma ambacho hujastahili ni kosa la kimaadili, na katika baadhi ya nchi, ni kosa la jinai.
Hoja muhimu ni hizi:
•Wananchi wanaamini kuwa mtu anayeitwa "Dk" ni msomi wa hali ya juu, hivyo hutegemea maamuzi yake kwa uaminifu wa kisomi.
•Viongozi wanaotumia vyeo vya bandia hudanganya jamii na kupata uhalali wa kisiasa au mamlaka kwa njia ya udanganyifu.
•Hii inatengeneza mazingira ya kudharau wataalamu wa kweli, na hujenga kizazi cha "wanaovua digrii kwa pesa badala ya maarifa."
5. Mbinu za ushawishi wa LISD: Kutumia jina la "London" kuhalalisha biashara
LISD hutumia jina la "London" kuashiria kuwa ipo Uingereza – jambo linaloaminika haraka na jamii nyingi za Afrika. Zaidi ya hapo:
•Huweka picha za watu maarufu waliopokea “digrii” zao ili kuaminika.
•Hutangaza tuzo kupitia vyombo vya habari vya mitandaoni na magazeti ya kawaida – siyo majarida ya kitaaluma.
•Hupendekeza wahitimu wajitangaze kama “Dr. So and So” – kabla hata haijapita siku moja!
Mbinu hizi ni ushahidi wa wazi kuwa taasisi hii inalenga biashara na si maendeleo ya taaluma.
6. Tishio kwa mfumo wa elimu na ustawi wa taaluma
Matokeo ya hali hii ni mabaya sana kwa mustakabali wa taaluma:-
•Vyuo halali vya elimu ya juu vinaonekana kama vya kawaida tu, kwani kila mtu sasa anaweza kuwa “Daktari” kwa kulipia.
•Wataalamu wa kweli wa masuala ya afya, sheria, elimu na theolojia hupoteza heshima yao.
•Tunaweka jamii katika hatari ya kuongozwa na watu wasio na sifa, lakini wenye vyeti vya heshima bandia.
7. Mapendekezo ya mabadiliko ya haraka
i.Serikali kupitia TCU, NACTVET na Wizara ya Elimu itoe tangazo rasmi juu ya digrii zisizo halali na taasisi zinazojihusisha na biashara ya vyeo.
ii.Vyombo vya habari vichunguze kwa kina vyanzo vya digrii kabla ya kuandika maneno kama “Dk.”
iii.Jamii ijifunze kutambua tofauti kati ya digrii ya kisomi, ya heshima, na ya kibiashara.
iv.Wanasiasa na viongozi wa umma wanaotumia vyeo bandia wachunguzwe kimaadili na wapewe onyo rasmi.
Hitimisho
Mchele wa elimu unatakiwa kutenganishwa na pumba za sifa za kununua. Kama taifa, hatupaswi kuruhusu soko huria la heshima ya kitaaluma. Kila cheo kina thamani yake, lakini thamani hiyo hujengwa kwa juhudi, maarifa, na muda — si kwa kutuma CV na kulipia jina.
Watanzania tunapaswa kusema: HAPANA kwa digrii bandia — na NDIO kwa elimu halisi.