Limekuwa ni swali katika Bongo za vijana wengi, kipi ni bora ama muhimu zaidi katika ulimwengu wa sasa baina ya Fedha na Elimu? Bila shaka kama swali la aina hii angeulizwa kijana wa miaka ya 80’ jibu lake lingekuwa “ELIMU NI BORA KULIKO FEDHA!” na bila wasiwasi wowote angekuwa sahihi kwa jibu lake hilo kwani ndio dhana iliokuwa ikitawala bongo za vijana wa zama hizo.
Kulingana na mfumo wa Elimu uliokuwepo kwa kipindi hicho, na mifumo ya maisha, mtu msomi zaidi ndiye alieonekana mtu bora zaidi na muhimu katika jamii hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa uhaba wa wasomi katika nchi nyingi za kiafrika hususa ni Tanzania. Hivyo basi wasomi wachache waliozalishwa kwa kipindi hicho hawakuweza kukidhi haja ya uitaji wa wasomi na wataalamu katika sekta mbalimbali nchini zikiwemo SEKTA YA ELIMU, AFYA, MIUNDOMBINU, SIASA nk.Hivyo ajila kwa wakati huu zilizidi idadi ya wasomi waliozalishwa nchini, kwa namna hio nadhalia ya “ELIMU NI BORA KULIKO FEDHA!” Ilikuwa sahihi vichwani mwa vijana wa miaka hio.
ELIMU AMA FEDHA?
Swali lile lile anajiuliza kijana wa Zama hizi za sayansi na teknolojia, Zama ambazo wasomi ni wengi kuliko nafasi za ajira duniani na hali ikiwa mbaya zaidi kwa nchi za Kiafrika ambazo baada ya ukoloni ziliwekeza zaidi katika Elimu zikiamini Ujinga ndio ulikua adui namba moja kwa maendeleo ya nchi za kiafrika. Aliekuwa Rais wa Tanganyika HAYATI MWL JULIUS K. NYERERE na farsafa ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA aliuita ujinga kama adui wa maendeleo hivyo Serikali ya TANU baadaya azimio la arusha la mwaka 1967 Iliazimia kuondoa ujinga nchini Elimu ilianza kutolewa bure kwa watu wote na sekta ya elimu kuimalika kwa kiasi kikubwa, Huu umekuwa ni muendelezo hata baada ya kuja kwa serikali ya Jamhuri baada ya muungano sekta ya Elimu imeendelea kupewa kipaumbele hali iliyopelekea kuongezeka kwa wasomi maradufu, Tunaweza kuona kipaumele iliyopewa sekta ya elimu huku serikali ikijisahau kuzipa vipaumbele sekta nyinginezo ambazo ndizo hutoa Ajira kwa wasomi hao na hapo ndipo tatizo la upungufu wa ajira lilipoanzia.
Licha ya Serikali kuliona suala hili ila hakuna jitihada zozote za kimkakati zilizofanyika kutatua tatizo la upungufu wa ajira, Taasisi za Elimu ya juu nchini zimeendelea kuzalisha Wasomi wengi ambao baada ya kumaliza masomo yao hakuna ajira za kutosha kuwaajiri badala yake Serikali inawabeza na kuanzisha nadharia zisizo na tija kwa vijana ikiwemo nadharia Maarufu ya “SOMA UKAJIAJIRI!”Jambo ambalo nitofauti na matalajio ya vijana wengi na wasomi wengi walio lelewa na kuaminishwa ELIMU NI BORA, Elimu ndio itakayofanya wao kutimiza ndoto zao. Ni dhahiri kwamba katika zama hizi za sasa Elimu sio tena ufunguo wa maisha kama ilivyokua Awali,Simaanishi hakuna haja kabisa ya kusoma wala Elimu HAPANA.Nafasi ya elimu katika jamii ni kubwa na muhimu,Ila umefika muda kwa Jamii, Wazazi na Serikali kuzifuta nadharia za kizamani katika vichwa vya vijana na Watoto kuhusu Elimu. Ni muda sasa kuwaandaa vijana kukabiliana na Ulimwengu mpya Ulimwengu ambao Elimu ni moja ya vitu vya msingi kwa mwanadamu na sio jambo ambalo litamfanya yeye kutimiza ndoto zake au kuwa na maisha yaliyo bora hapo baadae.
TATIZO LIKO WAPI?
Mfumo wa Elimu uliopo haumuandai mwanafunzi au msomi namna ya kuishi baada ya kumaliza elimu yake,kwa ufupi hakuna namna ambao elimu yetu inamuandaa msomi kuja kukabiliana na maisha halisi.Nidhahiri kwamba kuna tofauti kubwa ya nadharia zinazofundishwa mashuleni na vyuoni na uharisia wa maisha. Wasomi wengi wanaozalishwa na Elimu yetu hawajengewi uwezo wa kuja kukabiliana na maisha ya mtaani, nikama mfumo wa Elimu uliopo unawaaandaa wasomi nje ya uharisia wa maisha na jamii wanazotokea. Matokeo yake badala ya kutengeneza wasomi watakaokuja kuleta mabadiliko katika jamii wanaotoka tunatengeneza tabaka la watu wanaoshindwa kuendana na uharisia wa jamii wanazotoka, Watu wazembe,watu wa kuwabeza wengine kwa kuhisi wao ni bora kushinda wale wasio na Elimu.Matokeo yake wanashindwa kua msaada katika jamii na jamii pia zinashindwa kua msaada kwao,kwanamna hio kunakua hakuna matumizi ya Elimu walizozipata sio kwao pekee bali hata kwa jamii zinazo wazunguka.
Mfumo wa elimu tulionao unamuandaa msomi katika Taaluma fulani (proffesional),yawezakua taaluma ya afya,elimu,sheria nk,hivyo inamfanya msomi huyu kutegemea ajira pekeyake kwani hana ujuzi wa elimu ya kitu kingine tofauti na taaluma aliosomea kwa kipindi chote.Kama ww n Msomi tumia muda huu kujiuliza muda ulioutumia kusoma kwa zaidi ya miaka kumi na mitano(15) Kujifunza taaluma moja tu, ambayo ndio unatarajia ijekua mkombozi wa maisha yako. Je, kwa muda wa miaka kumi na mitano ni mambo mangapi mtu anaweza kujifunza pekeyake? Je, kwa muda huo huo ni aina ngapi za ujuzi mtu anaweza kujifunza nje ya mfumo wa Elimu? Baada ya kujiuliza hayo sasa na imani utakua umepata picha kua Mtu anahitaji elimu zaidi ya taaluma anayoisomea kama kitu cha ziada kwa mfano ufundi stadi, elimu ya ujasilia mali na biashara,kilimo nk Hii ingesaidia kwa namna moja au nyingine kupunguza tatizo la ajila pia.
Licha ya kuwa mfumo wa elimu kuwa umeegemea zaidi katika kutoa mafunzo ya taaluma mbali mbali, lakini bado taaluma hizo pia hutolewa kwa Nadharia zaidi kuliko vitendo. Hivyo kuwajengea wasomi wetu Uwezo mdogo wa kiutendaji katika taaluma zao, jambo hili pia limekuwa kikwazo kikubwa kwa upatikanaji wa ajila hususani katika soko la ajira la kimataifa. Wasomi wengi nchini wanashindwa kuleta ushindani katika soko la ajira la kimataifa kulinganisha na wasomi wa nchi nyingine zikiwemo nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kama Kenya na Uganda. Hii inaonesha kuwa kiwango cha elimu kinachotolewa nchini kiko chini au hakikidhi vigezo vya kimataifa.
CHAGUA MOJA
Ifike muda kwa Serikali, jamii na wadau wa Elimu nchini kukubaliana na ukweli kuwa zama zimebadilika sio kama zamani,watoto wetu na wasomi hawaitaji kuendelea kuaminishwa kuwa Elimu pekee ndio itakayo fanya wao kutimiza ndoto zao. Dunia imeshuhudia mapinduzi ya kiuchui makubwa sana katika zama hizi,watu wengi walio fanikiwa duniani ikiwemo wana siasa,wasanii,wanamichezo na matajiri wakubwa duniani ambao ndio mitazamo ya kuigwa na wenye ushawishi zaidi kwa vijana wala sio wasomi. Wengiwao wakiwa na Elimu za chini au walio acha Elimu wakafuata ndoto zao.Kutoka katika chapisho maarufu la nchini Marekani la “FORBES” la mwaka 2020 wanamzungumuzia Tajiri bilionea wa kimarekani JEFF BENZON mwanzilishi na mmiliki wa Kampuni ya usambazaji na uuzaji wa bidhaa kwanjia ya mtandao Maarufu kama “DELIVERY” ya AMAZON kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wazaidi ya fedha za kimarekani Bilioni 130.BENZON sio msomi wa uchumi bali mjasilimali na mbunifu akiwa na Elimu ya chini kabisa,Hii inaonesha wazi kua kuna tofauti kubwa sana kati ya Elimu ya darasani na maisha harisi.
Turejee katika swali letu au mada yetu tuone kati ya Elimu na Fedha kinachoitajika zaidi na kizazi hiki ni kitu gani? Mimi binafsi nikijana wa umri wa miaka 21, katika utafiti wangu mdogo nilioufanya kabla ya kuandika andiko hili nimegundua kuwa asilimia kubwa ya vijana wa rika yangu na zaidi, kuanzia miaka 20-30 wana ndoto za kujiinua kiuchumi zaidi na wengiwao wamejikita katika shughuli ndogondogo na kilimo, baadhi wanasoma huku wakijishughulisha na shughuli za hapa na pale. Kama utachukua muda wako kupitia taarifa ya Tume ya vyuo vikuu TCU ya miaka kumi iliopita mpaka sasa utagundua kuna ongezeko kubwa la vijana wanao acha masomo vyuoni kwa sababu mbalimbali zisizofahamika. Na kama utajaribu kujikita ndani zaidi basi utagundua wengi wa vijana hao huacha masomo na kujikita zaidi katika utafutaji wa maisha.
Na hapo ndipo utakapokubaliana na mtazamo wangu kuwa kizazi hiki kinahitaji Fedha zaidi kuliko Elimu. Najua bado unamaswali unajiuliza kichwani mwako nikweli uko sahihi kuhoji kua mbona kuna wasomi wengi pia waliofanikiwa. Ndio wapo sijakataa kua hawapo, lakini je ni Asilimia ngapi kati ya waliopo? Je, ni wangapi kutokea katika jamii zetu za maisha ya chini? Fanya utafiti wa haraka na mdogo katika mtaa wako ni vijana wangapi wanaomaliza vyuo chini ya miaka25 hawana ajira nabado nitegemezi kwa wazazi na familia? Ni aibu msomi badala kua msaada anakua tegemezi katika familia,wengi wao wanaishia kua walevi na waraibu wa madawa.
CHUKUA HATUA
Kuna mambo mengi yanaweza kufanyika kuliokoa Jahazi hili la vijna,tunaweza kuwa na mitazamo tofauti baada ya kusoma kurasa zilizopita. Kitakachonipa faraja nikuona kua umeweza kupata muda kulitafakari jambo hili pia. Huo ni zaidi ya ushindi kwangu na kwako pia kama mpenda mabadiliko”BIG UP” Kimtazamo tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye Mfumo wetu wa Elimu. Tunahitaji mfumo wa Elimu ambao utaendana na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi inayotokea duniani.Wakati ambao dunia iko katika mapinduzi ya kiuchumi ya kidigitali tujiulize sisi tuko wapi? Tuko katika nchi ambayo wananchi wake na wasomi hawajui chochote kuhusu matumizi mazuri ya fedha,uwekaji wa akiba,uwekezaji katika masoko ya hisa na masoko ya kidigitali ya fedha duniani. Kizazi hiki kinahitaji Elimu itakayo kua na matumizi ya moja kwa moja katika maisha ya kila siku,na sio Elimu ya nadharia nyingi na Taaluma zisizo na ajira, tuwafundishe vijana namna fedha inavofanya kazi, tuwajengee tabia ya kutunza akiba tangu wakiwa wadogo ili wanapokua waweze kujiajiri.Jamii pia inapaswa kutowakalilisha watoto kua Elimu pekee ndio itakayo wafanya watimize ndoto zao,Kama kila mtoto atakua akiamini anatakiwa kusoma kwa bidii ili aishi vizuri baadae basi hatutoacha kuzarisha kizazi kinacho soma ili kiajiriwe.
“NAFIKIRI ELIMU WALA HAIHUSIANI NA FEDHA!ILA ELIMU YA FEDHA.”

Upvote
1