Uchaguzi 2020 Maoni huru: Awamu hii Urais wakipata hata kura Milioni 3 wana bahati sana

Uchaguzi 2020 Maoni huru: Awamu hii Urais wakipata hata kura Milioni 3 wana bahati sana

CCM ni mfu anayejikongoja!
Tunasubiri kuhitimisha mazishi ifikapo 28.10.2020
tapatalk_1593965156914.jpg
 
Ndivyo ilivyopaswa kuwa lakini tatizo ni wapinzani wa Tanzania .
Tuna wapinzani wa ajabu sana.

Upinzani ndani ya CCM ndio upinzani halisi nje ya CCM ni Vikampi vya watu binafsi.
CCM ya Kikwete ilishindwa na CCM ya iliyokuwa imebeba hasira za Lowasa kukatwa.
Halikadhalika 2025 CCM itakayoshinda ni ile itakayotoka kwa Mtu atakayekuja na hoja za kufanya tofauti na CCM ya Magfl .
Upinzani upo ndani ya CCM.

Leo hii wapinzani kama Chadema wangeruhusu Mageuzi ya ndani na chaguzi huru ndani ya Chama Bila shaka Mwenyekiti angekua ni ama Zito Kabwe au Komu au Heche au Halima. Chama kingekua na mtizamo mpya na nguvu mpya. Leo hii Chadema inaongozwa na MTU aliyeipoteza njia mwaka 2010,2015, 2020 sasa.
Wapiga kura wakimuona Mbowe jukwaani wanapoteza imani ya kushinda. Miaka mitano Mbowe amekua ni MTU wa kulilia Uenyekiti tu huku Chaguzi zikiwa zinavurugwa bila tamko lolote. Sasa kamanda anabaki kwenye kiti na ujasiri wa kujificha nyuma ya shujaa Tundu Lisu.

Kama Kikwete aliwapa watanzania maziwa na nyama na samaki lakini walimkataa kwa kumwita dhaifu asiye na maamuzi na walitamani aondoke madarakani kwa ushawishi wa Mbowe na Dr.Slaa huku wakiamini kuwa nchi inapaswa kuendeshwa kidikteta basi watanzania Chini ya Upinzani wa Mbowe hawawezi kamwe kuiondoa CCM madarakani.

Kwanza Sheria za Uchaguzi zinafanana sana na zile za CCM.
Yani Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wana nguvu kuliko wananchi wote milioni 28+ wanaopiga kura.
CCM wajumbe wa wale wanaopitisha majina Dodoma wapo wachache lakini wana nguvu kubwa kuliko wapiga kura wote ndani na nje ya Chama.

Wapinzani hawana Sera zinazowavutia wananchi zaidi ya kumshambulia Magufuli binafsi. Wakati huo huo wananchi kwa uelewa wao ama mdogo au mkubwa wanazungumza Lugha moja kuhusu Magufuli kuwa ameleta maendeleo makubwa . Yani hata mtu ambaye kijijini kwake hakuna maji ,barabara na dawa hospitalini huku biashara zikiwa zimedoda lakini ana matumaini kuwa Magufuli anabana kwa Muda tu lakini akikamilisha Kujenga miundo Mbinu hali ya maisha itapaa na kuwa nzuri kuliko Ulaya na Uarabuni na tutatoa misaada kwa Wazungu badala ya kuomba misaada. Imani hiyo ipo mpaka kwa wasomi , Wachungaji na mashekhe na wasanii wa Muziki mpaka watoto wadogo ,wazee na wafanyakazi pia wanamatumaini kuwa Hali ni ngumu kwa muda tu. Mpaka kule kusini kwenye wakulima wa Korosho, wote wana matumaini na JPM na wapo tayari kwenda naye kwa matumaini kuwa naye pia ni maskini mwenzao kwa sababu hasafiri kwenda kwa mabeberu kuomba misaada.

Wapinzani wengi hawajui maisha ya vijijini yalivyo kwa uhalisia matokeo yake wanaongelea mambo yasiyo na tija kwa mamilioni ya watanzania huku wakijikita kwenye Hotuba za kumkejeli Magufuli muda wote.
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuwa na matumaini kwa jiwe, chunguza hao unaowasema, wengi hawajielewi au ni wachumia tumbo kama wewe.
 
Uchaguzi wa 2015 jamaa alipata kura laki tisa. October atapata laki Tatu. Kinachompa jeuri, kiburi na kujiamini ni Jeshi, TISS na polisi.
Hata hao ulio wataja wana machungu pia maana kwa yanayo endelea hayamfurahishi mtu yeyote
 
Kweli kabisa mkuu.
Lisu atapoteza mvuto Kwa upumbavu kabisa.
Alikuja kwa kasi kubwa lakini ghafla akavaa kichwa cha MTU mjinga na Mlevi mkubwa ,muhuni na fisadi mkubwa, mzinzi na msanii,mwizi wa Ruzuku za Chama, DJ .Mbowe.
Mtu kweli unasimama jukwani unawaambia watu wa vijijini habari za korona kuwa inaua watu wengi bila kuwapa ushahidi. Hivi kijijini MTU anaweza akafa watu wasijue.??
Yani Lisu amepotezwa mapema sana na Misimamo ya Chama kinachomilikiwa na Bilionea Mbowe
Lazima kuna kitu mbowe alikufanya au hakukulipa hela yako
 
Tulizoea kusoma tafiti kuhusu uchaguzi kipindi hiki; mwaka huu kimya. TWAWEZA wako wapi.
Utawala wa kidikteta huwa haupendi mambo kama hizo, fanya utafiti ujikute siyo raia tena. Jiwe ni hatari kwa maendeleo ya Taifa hili
 
Tatizo ni kura kuhesabiwa kwa haki. Uchaguzi ukiwa huru na haki ccm wanafutika saa 2 asubuhi tarehe 28/10/2020
 
waTanzania wa ss sio wajinga maendeleo wanayaonaa barabara,ma flyover ,huduma za afya zilizo boreshwa,elimu mzee kagusa kila sekta ndani ya miaka mitatu tu.
Je akipewa mitano tena tarajia watoto wenu mashuleni kura chipsi kuku asubuhi, wali nazi mchana,wali kuku usiku.
Kundi gani katika jamii watampa kura jiwe?

1: Wafanyabiashara?
2: Wafanyakazi?
3: Wakulima?
3: Wanafunzi?

Kwa kifupi sioni kundi lolote linaloweza piga kura kwa jiwe, mana wote wameathiriwa na utawala wa jiwe
 
Na safari hii ndiyo itakuwa aibu kubwa kwa ccm maana ndiyo itakuwa mara ya kwanza kwa mgombea wao kuiondoa madarakani baada ya miaka 60 ya uhuru.
Umeona eeh walifikiri ikitoka form moja ya mwenyeki wa chama itakua nafuu atapita bila kupingwa kumbe TL alikua nangoja wajichanganye angalia miti yote inateleza anga zote zimegoma ukungu mtupu sauti za bundi kila sehemu CCM mtavuna mlicho kipanda hili ni kosa la kiufundi tangu uhuru kutoa form moja kwa chama kikongwe kama CCM rudi tena chekechea hata watoto wadogo wanatucheka mlishindwa kujua kua maisha nikama gwalide wakwanza anakua mwisho Lissu naye zamu yake tutulie mpe mitano yake.
 
Kweli kabisa mkuu.
Lisu atapoteza mvuto Kwa upumbavu kabisa.

Alikuja kwa kasi kubwa lakini ghafla akavaa kichwa cha MTU mjinga na Mlevi mkubwa ,muhuni na fisadi mkubwa, mzinzi na msanii,mwizi wa Ruzuku za Chama, DJ .Mbowe.

Mtu kweli unasimama jukwani unawaambia watu wa vijijini habari za korona kuwa inaua watu wengi bila kuwapa ushahidi. Hivi kijijini MTU anaweza akafa watu wasijue?

Yani Lisu amepotezwa mapema sana na Misimamo ya Chama kinachomilikiwa na Bilionea Mbowe
Kapotezwa sana kwanini unateseka nae sasa?
 
"......... Wapinzani wakiungana wote wenye nguvu CCM ipo pekee yake hata kura milion 3 hakiwezi kupata. Watu wamechoka wanataka kuona changes za kweli zenye kuleta neema kwa nchi yetu.

Wakiungana wapinzani na wanajiandaa bila uoga kusimamia ushindi wao wa haki basi CCM chalii. Tuliona KANU ya Kenya ilivyodondoshwa collaboration ya vyama vya siasa chini ya Mwai Kibaki.

KWA TAMAA MLIZONAZO KUUNGANA HAITAWEZEKANA. KILA UCHAGUZI MNAISHIA KUSEMA KUUNGANA, VITENDO HAKUNA.
Jiulize kwanza kwanini hawaungani kabla ya msimu wa uchaguzi?Kwanini kuna wagombea uraisi wa Muungano zaidi ya 10?
Jibu ni mmoja tu wanasaidia CCM kushinda kwa kishindo kwenye Udiwani,Ubunge na Urais.
 
umeona eeh walifikiri ikitoka form moja ya mwenyeki wa chama itakua nafuu atapita bila kupingwa kumbe TL alikua nangoja wajichanganye angalia miti yote inateleza anga zote zimegoma ukungu mtupu sauti za bundi kila sehemu ccm mtavuna mlicho kipanda hili ni kosa la kiufundi tangu uhuru kutoa form moja kwa chama kikongwe kama ccm rudi tena chekechea hata watoto wadogo wanatucheka mlishindwa kujua kua maisha nikama gwalide wakwanza anakua mwisho Lissu naye zamu yake tutulie mpe mitana yake
Jiwe anakipelekesha ccm anavyo taka maana hakuna mtu wa kusema ekosea. Kila mtu anamuogopa kwa kuhofia kibarua chake kuota nyasi.

Ccm imekuwa ya mtu mmoja hata kama wanachama hawataki lkn hawana njia ya kuwasilisha maoni yao.
 
Back
Top Bottom