Maoni: Je, ni wakati sahihi wa kuanzishwa ofisi ya mamlaka ya mkaguzi mkuu wa hesabu ya serikali (Controller and Audit General Authority)?

Maoni: Je, ni wakati sahihi wa kuanzishwa ofisi ya mamlaka ya mkaguzi mkuu wa hesabu ya serikali (Controller and Audit General Authority)?

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2020
Posts
905
Reaction score
1,540
Ndugu Abbas Mwalimu , anafikiri sasa kuna haja ya kuipandisha hadhi Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwa Mamlaka kamili yaani Controller and Audit General Authority (CAGA).

Kwa nini anasema hivi? Kwa sababu kwa mtazamo wake, anaamini ikiwa mamlaka kamili (Authority) itakuwa na uwezo wa kimaamuzi (ability to enforce sanctions) yatakayosababisha baadhi ya watu kuwajibishwa moja kwa moja kwa mujibu sheria itakayokuwa ikiongoza 'mamlaka' hiyo badala ya kuishia kushauri 'Mamlaka' tu.

Kwa maoni yake, CAG akikosa nguvu za moja kwa moja za kuathiri ama sanctions kisheria nadhani bado changamoto zitazidi kuwa kubwa na hivyo msukumo unaweza kupungua zaidi katika utawala bora na uwajibikaji wa serikali kwa maana ya kwamba baadhi ya watumishi wa umma wataendelea kutokuwa waadilifu kwa nchi na wananchi na hivyo kushindwa kuwaletea ustawi wananchi huku likiwa ndiyo lengo kuu la serikali kwa mujibu wa Katiba.

Hili liligusiwa pia na Razanno na Gruzd (2015) pia walipoeleza kwa lugha ya Kingereza kwamba, "...the lack of tough sanctions may mean that the political reputational incentive is not significant enough to warrant change". Tumeona mafanikio kadhaa kwa TAKUKURU tangu ilipokuwa taasisi inayojitegemea na hata Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa sana hivyo CAGA nayo itafanikiwa bila shaka.

Mbali na ofisi ya CAG kuwa 'mamlaka' kamili nadhani pia kuna haja ya kutazama upya mfumo wetu wa kutathmini uwazi (transparency), uwajibikaji (accountability), kupambana na rushwa (Jambo ambalo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliwaagiza TAKUKURU), kuwawezesha wananchi kushiriki katika maamuzi sambamba na kuhanikiza utumiaji wa teknolojia kuimarisha utawala bora kama vile kuhakikisha miamala yote inafanyika kwa njia za kielekroniki kupitia simu ya kiganjani ili kuondoa mianya ya rushwa na ubadhilifu?

Katika kufikia azma hizi nadhani kuna haja ya kuwa na mfumo wa kujitathmini wa serikali ambao unaweza kuitwa 'Tanzania Accountability and Participation Independent Review Mechanism au TAPIRM'

Kwa maoni anafikiri hii mechanism ingekuwa sehemu ya CAGA katika kufanya tathmini ni kwa kiwango gani wananchi wa kawaida wanatambua wajibu wao kwa wale waliowachagua na walioteuliwa kwa lengo la kuwahudumia kwa sababu kwa mfano, tafiti zinaonesha kuwa baadhi ya wananchi hawana imani na serikali za mitaa (local governments) kutokana na kuhofia kutosikilizwa. Hili liliainishwa katika utafiti uliofanywa na Anna Mdee na Lisa Thorley na kuchapishwa mwezi Oktoba, 2016 uliokuwa na kichwa cha utafiti, 'Good governance, local government, accountability and service delivery in Tanzania: Exploring the context for creating a local governance performance index' ambapo katika utafiti wao wamebaini kama ifuatavyo:

"Citizens are also less likely to engage with their LGAs as there is a perception their concerns will not be heard or taken seriously" (Mdee na Thorley, 2016:12).

Huenda hii ya kukosa imani ndiyo sababu wananchi hubeba mabango pindi waonapo ama kusikia ziara ya Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika eneo lao hali iliyopelekea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwaonya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi ambao watabainika kuzuia haki hiyo ya wananchi.

Hivyo basi kwa mtazamo anaamini ipo haja ya kuwa na mechanism yetu wenyewe ya kutathmini uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini yaani TAPIRM itakayokuwa ndani ya CAGA ili wananchi washiriki katika kufanya maamuzi na kupanua wigo utawala bora baada ya kuwa tumejitoa OGP.

1618054991228.png


Kimsingi anaamini kuwa kuna haja ya sisi kama watanzania kujitathmini na kwa serikali kuipandisha hadhi ofisi ya CAG kuwa mamlaka inayojitegemea yaani CAGA itakayokuwa na uwezo wa kuathiri (enforcing decisions/sanctions) kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaohusika na matumizi mabaya ya fedha za umma na ambayo itakuwa na tawi la kupima uwajibikaji (TAPIRM) kwa kuwashirikisha wananchi ili tufikie azma ya Dira ya Taifa 2025.

Kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wenu; Abbas Mwalimu na Mamlaka ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
 
Back
Top Bottom