Geo C Starfish
Member
- Jul 17, 2021
- 5
- 7
Kifungo ni moja ya hatua za kumuwajibisha mkosaji ili atambue kosa lake na aweze kujirekebisha kwa kutokufanya tena kosa hilo na hata makosa mengine.
Mtu anapofanya kosa na kupewa kifungo au kuwekwa kifungoni huitwa mfungwa. Kifungo hufanya watu kufuata sheria na hupunguza kwa kiasi fulani uvunjifu wa sheria na amani katika jamii.
Japo kuna changamoto nyingi hutokea katika mchakato mzima unaompelekea mtu kupewa kifungo na kuwa mfungwa. Kwani baadhi yao huwa ni wakosaji kweli na baadhi yao huwa si wakosaji ila hujikuta kifungoni baada ya kushindwa kuonyesha ushahidi makini mbele ya chombo kinachohusika na kutoa hukumu yaani mahakama.
Moja ya makosa ambayo humfanya mtu kufungwa ni MAUAJI. Mauaji ya binadamu mwenzake au hata mauaji ya mnyamapori ambae ni mali ya Serikali bila idhini ya serikali. Mtu anapofanya mauaji ya binadamu mwenzake dhahiri huwa ni ngumu kuwalipa ndugu na jamaa wa marehemu kwani huwa hakuna chochote kinachoweza kufanyika ili marehemu huyo arudi tena katika maisha yao. Hivyo hata muuaji anapofungwa huwa ni suala tu la kuwafariji wafiwa na pia kujaribu kuzuia mauaji mengine yanayoweza kutokea baina ya ndugu hao na muuaji labda kwa sababu za visasi na mengineyo.
Pia muuaji anapofungwa inatoa somo hata kwa watu wengine walioko huru kujua kuwa watakapofanya kitendo kama hicho wataishia kuwa kifungoni.
Hili hakika ni suala zuri linalodumisha amani na kupunguza uharifu katika jamii zetu.
Kosa lingine ni UBAKAJI. Kitendo cha mwanaume/mwanamke kulazimisha kufanya mapenzi na mwanamke/mwanaume bila ridhaa yake. Hapa tuongelee ubakaji tuliouzoea zaidi katika jamii zetu, ubakaji wa mwanaume kumlazimisha mwanamke au binti kufanya nae mapenzi bila maelewano au ridhaa yake.
Kosa hili linapotokea na mchakato mzima wa kesi kufanyika na ushahidi ukapatikana kuwa ni kweli mwanaume kafanya kitendo hicho cha kubaka, basi huukumiwa kifungo kulingana na mujibu wa sheria za nchi.
Hii husaidia kumfanya mkosaji kujua kitendo alichokifanya si kizuri na ni uvunjifu wa sheria na pia kutoa onyo kwa watu wengine kutofanya kitendo hicho.
Hukumu zote hizi zinafaida katika kuilinda sheria na kudumisha amani. Lakini ulishawahi kufikiria juu ya wategemezi wa wahanga wa kesi hizi?
Mfano katika familia anapouawa baba wa familia ambae alikuwa anategemewa kwa kila kitu na familia, je mke na watoto wake hubaki na hali gani?
Ushauri wangu ilikuwa inafaa angalau kwa namna moja ama nyingine muuaji anapohukumiwa kifungo basi anatakiwa kufanya kazi za kuingiza kipato akiwa huko huko gerezani na kisha kipato chote anachotakiwa kulipwa kiende moja kwa moja kusaidia familia ya marehemu katika majukumu yao ya msingi. Japo ni ngumu kuziba pengo la marehemu lakini inaweza kusaidia kwa kiasi flani kutatua baadhi ya changamoto za familia.
Vile vile kwenye suala la ubakaji, inapotokea binti au mwanamke amebakwa na bahati mbaya akapata mimba, mtuhumiwa hufungwa lakini maisha ya aliyebakwa na mtoto atakayemzaa hubaki kuwa ni juu yao katika utafutaji wa ridhiki. Yaani mtoto anapozaliwa hukua bila baba na bado mama yake hutakiwa kupambana zaidi kwa ajili ya kumlea. Hivyo mateso hubaki kwa mama ambae ni muhanga wa kubakwa na mtoto kuishi maisha ya shida.
Hapa ni vema kama sheria ingewekwa kwa ajili ya kumfanya mama wa mtoto na mtoto mwenyewe kutokuishi maisha ya kuteseka zaidi. Mtuhumiwa angefungwa na kupewa kazi za kuingiza kipato akiwa gerezani na kipato kinachopatikana kiwe kinaenda moja kwa moja kwenye malezi ya mtoto huyo na mama yake.
Mambo kama haya yanaweza kusaidia sana jamii na wahanga wa matukio haya kutokuteseka zaidi katika utafutaji wa ridhiki. Ikizingatiwa aliyeuawa alikuwa ni tegemeo la familia na pia hata mbakwaji kuwa bado tegemezi kwa wazazi wake au walezi.
Japo haiwezekani kurudisha kila kitu katika hali yake lakini hapa kinachotafutwa ni kufuta wahanga machozi na kuwapa watoto uhakika wa kuendelea na maisha wanayostahili kuyapata kama kupata elimu bila shida na mahitaji mengine madogo madogo.
Ilivyo sasa mkosaji anapofungwa, bado haiwasaidia wahanga kuondokana na tatizo la kuteseka katika utaftaji na ndio maana wakati mwingine kesi kama hizi watu huamua kuziacha tu zisiendelee kwa kutotoa ushahidi mahakamani sababu wanaona ni kama watajiongezea matatizo na hakuna watakachoambulia.
Vyombo husika vijaribu kulitazama hili.

Upvote
3