Pongezi kwa uzi huu wa Askofu Bangoza unalolitakia taifa letu mambo mema na lisitekwe nyara na chama au kiongozi mmoja.
Inatakiwa sasa mjadala mpana nje ya Tume ya Kudumu ya Bunge utawala, sheria na katiba upambe moto kila siku hadi elimu hii ya uraia, haki na demokrasia ieleweke ndani ya Bunge la chama kimoja watapokutana tarehe 30 January 2024 bunge lighairi miswada pendekezwa iliyosomwa November 2023, na kutamka miswada hiyo ni mibovu hivyo itupiliwe mbali.
Na serikali iiagizwe na Bunge iandae miswada mingine mipya inayozingatia maoni yaliyosikika mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge na mijadala endelevu ambayo inaendelea kwa kasi katika jamii kwa sasa inayokosoa miswada iliyopo na kuwapa mwanga jambo gani sahihi lifanyike bila kujali vyama.