Maoni - Katiba Mpya

Maoni - Katiba Mpya

Goodrich

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2012
Posts
2,091
Reaction score
1,178
Naamini mchakato wa Katiba Mpya utakuwa makini kwa kuwa tume iliyoteuliwa ni makini.

Maoni yangu ni kwenye masuala ya msingi kama ifuatavyo;

Katiba mpya itenganishe kabisa mihimili mitatu ya dola, yaani Bunge, Mahakama na Serikali. Mihimili hii isiingiliane kwa namna yoyote ile, wala muhimili mmoja usiwe juu ya mingine kama ilivyo sasa ambapo Rais ambaye ni mkuu wa serikali, ana madaraka juu ya Bunge na Mahakama.


Hili ni la msingi kwa kuwa litaipa uhuru mihimili mingine ya dola, pia litaepusha mambo mengi ikiwamo wabunge kuwa mawaziri jambo ambalo linaondoa uwajibikaji wa wabunge kwa wananchi, litaepusha majaji kuwajibika kwa serikali au kuteuliwa na Rais jambo ambalo linaondoa haki.

Kila Chombo cha Dola (Bunge, Mahakama na Serikali) kiwe na mfumo wake chenyewe.

Pia, kwa maoni yangu, vema Miundo ya Bunge, Serikali na Mahakama iwekwe kwenye katiba. Hii itadhibiti mtu mmoja kuwa na nyadhifa tatu au zaidi, itaweka muundo rasmi wa baraza la mawaziri na serikali kwa ujumla, itaepusha teuzi zisizo na maana na pia itaongeza ufanisi na kuleta matokeo yenye tija. Aidha, Tume ya Uchaguzi inaweza kuwa ni idara iliyo chini ya muhimili wa Mahakama.

Aidha, wananchi wanataka mfumo bora wa Muungano. Mpaka sasa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inapingana kabisa na Katiba ya Zanzibar. Wananchi wanataka kero hizi zipatiwe ufumbuzi kupitia Katiba.

Mambo hayo yakizingatiwa tutapata serikali inayowajibika kwa wananchi, na hivyo kujenga taifa jipya lenye heshima, demokrasia ya kweli, amani, na maendeleo ya kiuchumi.
 
True !!!!
Haya ndio maoni yanayopaswa kufanyiwa kazi na tume ya katiba.
Msingi wa matatizo ya nchi yetu ni kukosekana kwa uhuru Bunge na Mahakama.
Pia tume ya uchaguzi iwe taasisi chini ya mhimili wa mahakama.
 
Swali la kujiuliza ni kama JK atakuwa na uwezo wa kusimamia mapendekezo yatakayokusanywa na Tume ya Katiba !
 
Back
Top Bottom