Maoni kuhusu Mbunge/Wabunge kivuli/Vivuli (Shadow Member of the Parliament)

Maoni kuhusu Mbunge/Wabunge kivuli/Vivuli (Shadow Member of the Parliament)

Nyagawakelvin

Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
8
Reaction score
34
Maoni kuhusu Mbunge/Wabunge kivuli/Vivuli (Shadow Member of the Parliament)
Inaletwa kwenu nami Kelvin Nyagawa (Mwanasheria)

Kwani Prof. Rwekaza ni Professor wa sheria?
Kwanini hakupewa chairman Prof. wa sheria?

Tukimuuliza Prof. Rwekaza ili tuwe na tume huru kisheria nini inahitajika, anaweza kujibu kisheria??

Kwanini tusiwatumie wataalamu husika kwenye idara husika?? mfano hatuwezi kufanya Uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko,maambukizi kwa kumteua Proffesor wa sheria au uchumi wakati ma professor wa utabibu wapo.

Jawabu la matatizo ya TANZANIA ni kuwa na katiba mpya yenye maoni ya wananchi Kama tume huru ya uchaguzi kwa mujibu wa principle za kisheria na sio principle za baadhi ya wanasiasa.

Mahakama ya juu kabisa(Supreme Court of U.R.T, ambayo matokeo ya urahisi yatahojiwa na kunatakiwa kuwe na revision (marejeo) kwa civil case na criminal case, ikiwamo majaji wapya kwenye revision kuhusu asiyeridhika na matokeo ya urahisi.

Kwa mfano ibara ya 140(1) ya katiba ya Kenya 2010, inaruhusu mto yeyote kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais mahakama ya juu, lakini Uganda katiba yao inaruhusu Wagombea wa Urais ndo kupinga matokeo ya urais mahakamani, Uhuru wa watu Uganda umeminywa kwa sababu hao Wagombea nao ni binadamu na wanaweza wasifungue shauri au kupinga matokeo ya urais mahakamani.

NB. marejeo maana yake mahakama ya juu baada ya kutoa hukumu, inaweza kurejea tena marekebisho kuhusu shauri Hilo na kutoa maamuzi mengine, lakini TANZANIA tuboreshe kuliko Kenya, Revision kupangwa majaji wengine. Tumeona Kenya majaji nao ni binadamu so ili kujiridhisha mtu anaweza omba marejeo mahakama ya juu na kupangwa majaji wapya. Ripoti inajua hili na umuhimu wake???

Sheria za Afya za umma lazima ziwekwe kwenye katiba mpya Kama chanjo kwa watoto, Uchunguzi wa magonjwa ya maambukizi, usalama wa chakula na maji kwa raia, maudhui bora ya Sheria za uchumi Kama uwazi wa mikataba baina ya Serikali na wawekezaji kupelekwa bungeni na isiwe Siri, mipango bora ya ardhi na hati, utunzaji wa mazingira, vyanzo vya maji kutunzwa na reserved ya taifa ya maji na chakula
Sijasikia kuengeza Uhuru wa bunge cjui kwanini, cjaona mapendekezo ya uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi mafisadi, wanaovunja katiba ya nchi watashughulikiwa vipi.

Lakini jawabu la malalamiko yote ni kuwa na katiba mpya yenye maoni ya wananchi Kama tume huru ya uchaguzi kwa mujibu wa principle za kisheria, mahakama ya Juu kuweza kuhoji matokeo ya urahisi na pawe na revision. Bunge huru, ofisi huru ya DPP, katiba mpya yenye kulinda rasilimali za nchi kiuchumi Kama uvunaji wa rasilimali, wanyama pori, maji, madini na kuondoa usiri wa mikataba baina ya Serikali na wawekezaji wa nje, kuboresha mazingira Bora ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji pamoja na utunzaji wa mazingira na kutatua tatizo la ardhi kikatiba.

BIBLIOGRAPHY
Article 18(a) (b) of CURT 1977.
Article 140(1) Constitution of Republic of Kenya 2010.
 
Swala la katiba ni swala lenye sura mbili.
Lina sura ya kisheria na sura ya kisiasa.
Mkandala ni Prof wa Sayansi ya siasa.
 
Back
Top Bottom