Maoni kuhusu rasimu ya katiba

syanga.mushisa

New Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
4
Reaction score
0
Maoni ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


  1. Uhuru na haki ya mazingira safi na salama: Ibara ya 40 (2)
· Haki ya kuishi katika mazingira safi, salama na ya kiafya inahusisha haki kwa kila raia kutumia maeneo ya umma au sehemu mbalimbali za mazingira yaliyotengwa kwa madhumuni ya burudani,elimu, afya, ibada, utamaduni na shughuli za kiuchumi “bila ya kuathiri au kubugudhi wengine”


  1. Haki ya mtoto: Ibara ya 42 (1)(b)
· Kila mototo ana haki ya kutoa mawazo “endapo ana ufahamu wa kutosha na uwezo wa kufanya hivyo”


  1. Haki za watu wenye ulemavu: Ibara ya 44(1)
· Mtu mwenye ulemavu anastahiki (b) – (f) “endapo mazingira na hali aliyo nayo vinaruhusu”


  1. Haki za wanawake: Ibara ya 46(1)
· Kila mwanamke ana haki ya (a) – (g) Ongeza (e) “Kumiliki mali bila ya kuathiriwa na mila, desturi za kikabila au imani za kidini”


  1. Haki za wazee: Ibara ya 47
· Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu utakaowezesha wazee kupata fursa ya (a) – (e) Ongeza (f) Kulindwa na jamii au mamlaka za nchi kuendana na hali za uzee wao kama ugonjwa n.k (g) Kupata matibabu bila malipo yatakayogharamiwa na serikali katika hospitali za umma au nyingine zilizoainishwa


  1. Uraia wa kuzaliwa: Ibara 55(2)
· Ongeza: Mtoto aliyezaliwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano hata kama wazazi wake sio raia wa Tanzania isipokuwa kama ataukana uraia wake atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano
· Katiba itaje wazi kwamba “Raia wa washirika wa Muungano ni raia yeyote halali wa Jamhuri ya Muungano”


  1. Muundo wa Muungano: Ibara ya 57(1)
· Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni: (a) – (b), (c) Tanzania Bara “inatakiwa kuwa Tanganyika” Huwezi kuitaja Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bila kuitaja Tanganyika kwani ndio mataifa mawili huru yaliyoungana kuunda Tanzania. Endapo majina yanabadilika katiba itamke badiliko hilo vinginevyo kama Tanganyika inakuwa Tanzania Bara na Zanzibar inatakiwa kuwa Tanzania Visiwani
· Ongeza: Bila kuathiri katiba hii Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaweza kukubaliana kuunda shirikisho lenye serikali moja kama watakavyoona inafaa.



  1. Mambo ya Muungano: Ibara ya 60
· Mambo ya Muungano yatajwe hapa


  1. Serikali ya Jamhuri ya Muungano: Ibara ya 67
· Ili kuondoa mkanganyiko wa kuwa na maraisi watatu kuwepo na raisi wa Jamhuri ya Muungano na makamu wake wawili ambao watakuwa ndio wakuu wa Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kaika kutekeleza majukumu yao katika serikali ya Muungano itafuata mgawanyo wa mambo au majukumu yatakayoainishwa
· Watendaji wakuu hawa wa serikali za Tanganyika na Zanzibar ambao ndio makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wanaweza kuwa na jina jingine kwa mfano “Gavana” badala ya kuitwa raisi.
· Gavana wa Tanganyika atakuwa mkuu wa serikali ya Tanganyika na makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano atakayeshughulika na mambo fulani ya Jamhuri ya Muungano na Gavana wa Zanzibar atakuwa ni mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na makamu wa raisi wa Jamhuri ya Muungano atakayeshughulika na mambo fulani ya Jamhuri ya Muungano


  1. Madaraka na Majukumu ya Raisi: Ibara ya 69(1)
· Raisi akiwa Mkuu wa nchi, atakuwa na madaraka na majukumu yafuatayo: (c) Kuhutubia na kufungua Bunge jipa “la Jamhuri ya Muungano”
· Katiba itamke wazi kwamba endapo raisi aliyechaguliwa anatokana na chama cha siasa na alikuwa na uongozi wowote kwenye chama chake hana budi kujiuzulu nafasi hiyo kabla ya kuapishwa kushika madaraka ya raisi


  1. Sifa za raisi: Ibara ya 75
· (g) chimbuko la raisi litenganishwe na lipewe maelezo ya kina


  1. Haki ya kuchaguliwa tena: Ibara ya 76
· Kipengele cha (4) na (5) hakieleweki vizuri
· Ongeza (6) Raisi aliyemaliza muda wake kwa mujibu wa sheria aweza kugombea tena baada ya kuwa nje ya madaraka baada ya muda fulani


  1. Utaratibu wa uchaguzi wa raisi: Ibara ya 77
· Kipengele cha (4) hakieleweki vizuri


  1. Bunge kumshitaki raisi: Ibara ya 84
· 1(d) Uhaini – raisi aliyeko madarakani anafanyaje uhaini!!!! Ina maana raisi anaweza kupanga kupindua serikali yake mwenyewe?
· (3) (b) Asilimia ya wabunge inayotakiwa kutia saini kwa kumshitaki raisi iwe ni “moja ya tatu” badala ya asilimia ishirini na tano
· (6) Hoja ya kuunda kamati ya uchunguzi iungwe mkono na “mbili ya tatu” ya wabunge badala ya asilimia sabini na tano
· (12) Kamati ya uchunguzi iungwe mkono na “mbili ya tatu” ya wabunge badala ya asilimia sabini na tano


  1. Kiapo, muda na masharti ya kazi ya Waziri na Naibu Waziri: Ibara ya 95
· 4(c) hakieleweki vizuri
· Madaraka ya waziri ni yapi? Katiba ifafanue mawaziri wana madaraka yapi.


  1. Madaraka ya Mkuu wa Nchi kuhusu muswada wa sheria: Ibara ya 114
· (6) Kuna tatizo hapa endapo muswada utapitishwa na kuwa sheria ya nchi bila kuwa na saini ya raisi na kwa kipengele hicho ni kama pia raisi analazimishwa kusaini muswada kwa kuwa tu umeungwa mkono na bunge. Muswada usiokuwa na saini ya mkuu wa nchi inakuwaje!


  1. Kupitishwa kwa hoja za serikali: Ibara ya 115
· (2) Bajeti ya serikali inapita bila baraka za wabunge, hii ni kuwanyang’anya wabunge madaraka yao na kuipa serikali mwanya wa kutokuwajibika kwa bunge kwa kupitisha hoja zisizoungwa mkono


  1. Uchaguzi wa wabunge: Ibara ya 116
· (4) na (5) ni mawazo mazuri kupunguza gharama za kuendesha uchaguzi kila wakati lakini kuwe na angalizo lifuatalo:
Ø Mbunge aliyeshindwa akijua kwamba pindi mpinzani wake akiacha ubunge kwa sababu yeyote ile yeye ndiye anakuwa mbunge bila juhudi ya ziada kuna hatari ya kufanyiana hila na mauaji
Ø Suala la kuchagua mbunge mrithi kutoka chama hicho hicho liangaliwe upya kwa maana kwamba mrithi anatakiwa awe yule aliyeshika nafasi ya pili kwa kura kwenye uchaguzi ule na kwa jinsi hii lazima atatoka kwenye chama kingine au mgombea binafsi kwa vile hakutakuwa na wabunge wawili waliopigiwa kura na wananchi toka chama kimoja.
Ø Kumchagua mbunge wa kurithi toka orodha iliyowasilishwa na chama ni kumpa mtu ubunge ambaye hajapigiwa kura na wananchi
Ø Katiba haijazungumza endapo nafasi ikiachwa wazi na mgombea binafsi mrithi wake anapatikanaje!


  1. Sifa za kuwa mbunge: Ibara ya 117
· 1(a) – (e) Ongeza (f) ikiwa mgombea alipowasilisha hati ya kugombea kwake ameambatanisha na fomu ya kutaja mali alizonazo au shughuli yeyote inayomwingizia kipato.
· (2) (a) – (g) Ongeza (h) ikiwa mtu huyo anamiliki mali au fedha visivyo halali na ameshindwa kuthibitisha uhalali wa umiliki wake


  1. Spika na Naibu Spika: Ibara ya 128 – 132
· Katiba haijasema Spika na Naibu Spika wanapatikanaje!
Ø Wanaomba kupitia nafasi zilizotangazwa au
Ø Wanapendekezwa au kuteuliwa na makundi au mamlaka fulani kugombea nafasi hiyo?



  1. Sifa za mtu anayefaa kuchaguliwa kuwa spika au naibu spika: Ibara ya 132
· (d) Katiba itamke wazi uongozi wa juu wa chama ni ngazi ipi!


  1. Akidi ya vikao vya Bunge: Ibara ya 139 (1)
· Akidi ya kila kikao cha Bunge kinatakiwa kuwa “mbili ya tatu” ya wabunge na sio nusu ya wabunge kwani wabunge wanataka wawe wapi wakati wa kikao cha bunge!


  1. Mipaka ya majadiliano Bungeni: Ibara ya 142
· Katiba iweke mipaka ya matumizi ya lugha na kauli bungeni ili kudhibiti lugha chafu na kebehi bungeni.


  1. Muda wa kuwa madarakani kwa Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Majaji wengine: Ibara ya 155
· Miaka ipunguzwe toka miaka sabini kuwa sitini na tano. Hii ni kuhakikisha kuwa mtu ana afya ya kutosha kumudu majukumu yake.


  1. Wajibu wa Tume Huru ya Uchaguzi: Ibara ya 184 (1)
· Vipengele (d) - (f) vinaonekana zaidi kuwa ni kazi ya msajili wa vyama vya siasa


  1. Masharti kuhusu utaratibu wa kukabidhi madaraka: Ibara ya 236
· Kipengele cha (4) hakieleweki vizuri
 
The president must be accountable kwa maamuzi yote aliyoyafanya kinyume na sheria anapokuwa madarakani. Hii itasaidia kupiga vita ufisadi unaofanywa na watawala wakiwa madarakani kwa kudhania tu kuwa wao hawatashtakiwa wakimaliza muda wa utawala wao!! Kipengele hiki pia kitawapunguzia kasi wale wanaotaka URAIS kama njia ya kwenda kujitajilisha kwa kuiba rasilimali za nchi kwani wakifanya hivyo watawajibika baada ya kutoka madarakani; kinyume na sasa ambapo watawala mafisadi wanaachiwa waende kufaidi matunda ya wizi wao bila kuthibitiwa na juu ya hayo hulipwa pension nono muda wote wa maisha yao!!
 
ahsante jf tuchangie tupate katiba kwa maendeleo yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…