Maoni kutoka kijiwe cha msafisha viatu: Watanzania wengi hawapendi Mabadiliko, wanangoja Magufuli aondoke

Magufuli hana good intentions.

Inaonekana hajui ana intention gani. Au anafikiri - pamoja na Watanzania wengi- kwamba ana good intentions, lakini hajafikiri kwa kina kuhusu hizo intentions zake. End result ni unintended consequences. Negative ones.

He is all over the place.

He is a simpleton. A country bumpkin.

Playing checkers in a game that requirres three dimensional color coded chess underwater while swimming with the sharks without being eaten alive.
 
Mageuzi hayawezi onekana leo au kwa haraka huchukua muda na yawezekana yasionekane kwa wasoguswa nayo.

Pili, bado hatujafikia kuchagua kikanda au kikabila.

Nadhani, sera za kikanda na ukabila zilikuwa ni za Chadema wanapozungumzia majimbo.

Nasema hivi mageuzi ni zaidi ya ujenzi wa miundombinu kadhaa. Kama angekuwa ameleta mageuzi kweli, usingekuwa na wasiwasi kuwa akitoka watu wataendelea na kawaida yao.

Cdm waliweka wazi suala la uongozi wa majimbo, ila hiki alicholeta Magufuli ni ukabila na ukanda usio rasmi, lakini uko bayana kwenye matendo.
 
Nikisema ana "good intentions" ni kuangalia aina ya mawaziri ambao sasa angalau wanaonyesha wanawajibika.

Kwa mfano pale Afya kamweka Dr Gwajima anafahamu jinsi wizara inavyopigwa na sasa analifanyia kazi hilo.

Kule uvuvi tumemwona yule binti akifuatilia ulaji.

Jana Bashe kagundua ulaji kwenye chama cha ushirika.

Waziri mkuu huko Ruvuma kagundua ulaji uanofanywana madiwani.

Sasa, haya mambo yahitaji watu wenye uelewa na nia ya dhati kuyakabili maana watanzania wengi tumezoa upigaji na maisha ya urahisiurahisi.

Waziri Lukuvi imebidi aanze kuwapigia simu wananchi kuwahimiza kwenda kuchukua hati zao za viwanja wengine walikata tamaa kwamba wasingepata hati hizo kutokana na kuamini wamedhulumiwa.

Hata wewe Kiranga yawezekana chuki zako kwa Magufuli ni kutokana na kubanwa kwa kiasi fulani au kuathirika na uongozi wake kwa kiasi fulani hatuwezi fahamu hilo.

Maana najaribu kupata mantiki ya kumwita kiongozi wa nchi "a country pumpkin", hii yasema wazi aina ya watu wanaomchukia huyu raisi.

Wengi waloathirika walizoea fedha za bure za kupatikana kimagendo, ulaji kwenye mashirika ya umma vikao na semina za kulipana fedha nyingi tu zingine ni za wastaafu wanaosumbuka leo.

Hivyo hali si nzuri ila ulitaka hali iendelee vilevile, rasilimali kuibiwa, madawa kuuzwa kila kona au upigaji kuwa ni sehemu ya maisha yetu?
 
Tusimlaumu mtu bali tujilaumu sisi wenyewe kwa kutozingatia sera ya Azimio la Arusha ambayo inasema ,Ili jamii yoyote iendelee inahitaji vitu vinne ambavyo ni WATU,ARDHI,SIASA SAFI na UONGOZI BORA.

Shida yetu ipo kwenye siasa safi na uongozi bora.Tukianzia siasa,tangu mwaka 1995 nchi yetu ina falsafa ya MULT-PARTY SYSTEM yaani mfumo wa vyama vingi aya siasa,ambao huu mfumo unaendeshwa kwa maneno na hisia za chuki hasa kwa tabaka tawala ambalo linaongozwa na chama kile kile tangu mwaka 1977 ambacho hicho chama kimejaa wivu na dhuluma za wazi kwa vyama vikuu vya upinzani.

Uongozi Bora nalo ni jipu letu ambalo linatusumbua kwa kisingizia cha uzalendo na amani.Hapa viongozi wakubwa wa chama tawala wanatumia madaraka yao vibaya kwa vile tu hawawezi chukuliwa au kushtakiwa mahali popote pale kama kuna mapungufu ya kiutendaji pindi walipokuwa kwenye himaya.Ndiyo maana hata awamu hii inajitamba kwa kisingizio cha kujenga uchumi imara na kuleta nidhamu nchini huko ikizalisha nyufa ambazo itatuchukua muda kuziziba,mwenye macho yote mawili haambiwi tazama Tuipende nchi yetu kwa ustawi wa maisha yetu.
 

Richard rekebisha hapo unaposema kuwa watanzania walizoea kupata bila kuvuja jasho. Sema kuna kikundi kilizoea kupata bila kuvuja jasho. Hapa naona una tofauti zako binafsi na JK, ila una maslahi na Magufuli hivyo unatetea maslahi yako, lakini sio ubora baina yao.

Magufuli kama alivyo JK, hakuna muadilifu baina yao, bali wanatofautiana tu kwa mapungufu, lakini wote ni wale wale. Wakati JK aliruhusu vyombo vya habari kuwa huru, na demokrasia kutawala kwa kiwango cha kuridhisha, hiyo ilipelekea mabaya na udhaifu wa serekali yake kuanikwa. Leo Magufuli anahadaa umma kuwa ni mtu muadilifu, lakini hataki uhuru wa habari, haruhusu demokrasia na pia hataki uwazi kwenye serikali yake. Mtu ambaye hataki kukosolewa wala uwazi, unaweza vipi kutaka kuonyesha ni bora, wakati anatumia jazba kutotaka mambo kufahamika?

Wakati wa JK kwenye uchaguzi kulikuwa na wizi wa kura, ila chaguzi zilikuwa na fairness ya kuridhisha japo haikuwa na haki. Lakini toka Magufuli ameingia madarakani hakuna uchaguzi wowote uliofanyika kwa haki wala kwa uhuru. Hakuna kiongozi yoyote anayeweza kuwa muadilifu iwapo hata kuingia madarakani haingii kwa ridhaa ya umma.
 
Ukisikia ubabaishaji ndio huu.... Tunataka mfumo ndio ufanye kazi... How come , usikie kwa police , eti IGP ndie anaenda kukamata wahalifu... Maana yake polisi wa chini wameshindwa au wanashirikiana na wahalifu..

Ningefurahi kuona mawaziri wanashughulika na kutoa uongozi, kuonyesha njia... Kuamua msitu upi ufyekwe , siyo wao kuwa wakataji msitu.... Mawaziri wamekuwa managers badala ya kuwa leaders..

Tungetaka kuona mfumo ambao uko transparent, viongozi wakionyesha KPI zao za uongozi ni zipi? Vingenevyo wanafanya mambo ya mzee wa Kiraracha ya kuita watu nyumbani na kumalizana..

Mimi najiuliza kwanini watumishi ambao wamepewa oversight ya wizara , wasione hayo .. Matokeo yake unasikia waziri kasimamisha mtu au kamuondoa mtu... Hii ni cheap popularity na uongozi wowote haujajengwa..
 
Hebu acha kutuletea vitu vya kipuuzi puuzi! Wasomi kama wewe ndiyo matatizo makubwa Nchi hii. Yaani msomi umejipinda kuandika upuuzi kama huu! Ndiyo wale wale umesoma lakini HUKUELIMIKA. Pole zako.
 

Good intentions haipo kwa yeye kutuambia, au ww unayefaidika na madaraka yake kutuambia. Good intentions ipo kwenye kuruhusu mifumo kufanya kazi, na sio kusubiri kiongozi mmoja mmoja kwenda kuibua upigaji. Mtu mwenye nia njema kisha anakwenda kuhakikisha yeye, spika wa bunge na makamu hawashitakiwi wakitoka madarakani, hapo inabidi ujiulize vizuri.

Kama u.likuwa unatetea mageuzi na unasema rais huyu kaleta mageuzi, tulitarajia mfumo ufanye kazi, na sio sifa za mtu mmoja mmoja kusaka sifa binafsi
 
Hebu acha kutuletea vitu vya kipuuzi puuzi! Wasomi kama wewe ndiyo matatizo makubwa Nchi hii. Yaani msomi umejipinda kuandika upuuzi kama huu! Ndiyo wale wale umesoma lakini HUKUELIMIKA. Pole zako.
Mkuu, kheri ya mwaka mpya.
 
Reactions: BAK
Nchi gani duniani haina tatizo la kukosa ajira, unailinganisha Tz na nchi gani interms of employment?
 
Hawa viongozi ambao inaonekana hawataki kuleta mabadiliko wanapatikanaje? Kama wanateuliwa kwa nini waliteuliwa? Kama waliteuliw kimakosa bila kuwajua vizuri kwa nini anayewateua asiwawajibishe ? Kama walichaguliwa na wananchi basi hata wananchi nao hawataki hayo mabadiliko.
 
Mimi sina maslahi na magufuli ila naeleza nilichokiona na nachoendelea kukiona.
 

Tusitumie maneno kama hawataki kuleta mabadiliko bali hawako tayari kuwajibika ipasavyo na hawajiamini.

Hivyo ni kwa sababu kama wanawajibika ipasavyo basi hawahitaji kutafuta vyombo vya habari waandamanae navyo pale wanapotekeleza majukumu yao.

Ni kama vile kutafuta "justifications" ambazo hazina msingi.

Au mtu anaamua kuchapa viboko watu wengine hiyo si sawa na wale wanaocharzwa viboko wanapaswa kushtaki ili isionekane kuwa kuna agizo "kutoka juu" la kucharaza viboko wale wanaozembea.
 
Ni kupoteza muda kuzungumzia nchi ambayo mtu 1 anaweza kuzima mifumo mingine yote iliyopo. Nchi inakuwa imara inapokuwa na mifumo thabiti kiasi kwamba hata mkikosea kuweka kiongozi (kama ilivyo sasa) bado hakuna shida!
 
Pia, Hao viongozi ambao inaonekana hawako tayari kuwajibika ipasavyo na hawajiamini wanapatikanaje? Kama wanateuliwa kwa nini waliteuliwa? Kama waliteuliw kimakosa bila kuwajua vizuri kwa nini anayewateua asiwawajibishe ? Kama walichaguliwa na wananchi basi hata wananchi nao hawataki hayo mabadiliko na hawaamini watayapata kupitia hao viongozi.
 
Wanayopitia Marekani ndio tunayopitia watanzania sema tu wenzetu wameamua kufanya kweli.
 
Kuna ka uzi nilikapandisha hapa nikasema kwamba kuna tatizo la tafsiri halisi ya malengo ya Magufuli,

Subordinates wake baadhi yao wamepata tafsiri potofu ya malengo yake.

Nikaenda mbele zaidi kussugest kwamba ipo haja ya kuwa na mtu wa Kati ambaye atakuwa kiungo mzuri baina ya Magufuli na subordinates wake,

Ila kuna mtu naona mwenye hili jukumu halitimizi ipasavyo,

Otherwise Magufuli akitumika vyema ni Rais Mzuri Sana.
 
Shida amegusa maisha ya wachache hasa wanufaika wake lkn majority ni dhoofu Hali,tunaombea Mungu ampe wepesi asibadili katiba Ili aingie Muislamu tule mema ya nchi na sio kuliwa na wachache.
 
Nchi gani duniani haina tatizo la kukosa ajira, unailinganisha Tz na nchi gani interms of employment?

Nimesema sasa chini ya Magufuli tatizo la ajira limeongezeka, ambapo mleta mada anataka kuonyesha sasa mambo ni mazuri kuliko wakati wa JK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…