MAONI: Kwenye battle ya flagships, hakuna brand inayoizidi Samsung, hata iPhone haishiki moto wa Samsung

Yaani watu mnacoment mtafikiri mmetumia simu za aina yoyote duniani kumbe hamna
 
Unaweza kutaja hayo matumizi unayoyaita ya kikamilifu
Mleta uzi ameshakuambia kama wewe ni una matumizi mengi ya simu aka simu yako ni ofisi ametoa ushauri tumia angalau Samsum S21 itafaa.

Jifanyie tathimini mwenyewe kwenye simu yako kama unatumia kikamilifu au la, mbona simple tu
 
Mleta uzi ameshakuambia kama wewe ni una matumizi mengi ya simu aka simu yako ni ofisi ametoa ushauri tumia angalau Samsum S21 itafaa.

Jifanyie tathimini mwenyewe kwenye simu yako kama unatumia kikamilifu au la, mbona simple tu
Kwahio matumizi hayo ya kikamilifu ni simu kitumia kama ofisi, you think Sumsung A03 huwezi tumia kama ofisi au ofisi gani munazungumzia.

Basically, hizo simu zoote hazing matumizi makuubwa mengine munayojaribu kuyasema matumizi ni yaleyale tu ku Store files (You need storage), to take picture (Camera nzuri atleast), Kuperuzi just internet.

Hao wanaonunua flagship matumizi ni hayohayo huwezi kunitajia matumizi mengine zaidi ya kutumia kwenye S24 Ultra utafosi tu.
 

Ulichoandika wewe ndio nilichoandika mie kwenye post namba 33, tena nikaanza Kwa statement JAPOKUWA MIE NI MLEVI WA SIMU ZA GHARAMA wakati mwingine watu wakienda dukani wanaangalia storage, camera na brand ANGALAU AONEKANE EXPENSIVE (point yangu ya msingi ilikuwa hapo kwenye herufi kubwa kwamba mtu ananua SIMU Kwa vigezo hivyo vingine na brand / model ya bei Kali ili mradi wa bei Kali wakati simu haitumii kikamilifu (nikimaanisha kununua simu ya gharama huku unatumia kutuma sms, kupiga na Whatsapp huku Kuna simu zingine za kawaida zinaweza kuku-offer hizo huduma ndipo nilimaanisha hawazitumii kikamilifu na unakuta mtu huyo tena anaweza akawa na bundle na bado akaja kukuuliza sungura Kwa kizungu anaitwaje huku ana bundle alafu ameshindwa kujishughulisha Kwa google au ku-download dictionary. Hapo ndio nilimaanisha ukamilifu wa simu yaani sio bei tu Bali other factors kama ram na mambo ka refresh rate etc (huo ulikuwa mfano tu wa watu wakienda dukani akionyeshwa camera, storage na brand Kali tayari kwake sawa huku Kuna vitu vingine unakuta unavipata sehemu nyingine.

Nilichoandika kwenye comment ni kama ulichoona wewe ila Kwa lugha nyingine nadhani uli-concentrate kwenye UKAMILIFU bila kuangalia maneno mengine

Hayo ya S21 ni mdau amepropose Kwa wenye mambo mengi ya kutumia simu maana yake huna ulazima wa kwenda S24 na sio msahafu kwamba lazima ichukue hiyo maana hata INFINIX Kuna vitu vingi tu vina-serve purpose japo zinaonekana kawaida na ndio maana nikakujibu ifanyie simu yako tathimini maana sikuwa na mood ya kujibu na ningekuambia rudi ukasome upya comment yangu 33 ningeonekana sijakutendea haki.

KIUJUMLA ULICHOANDIKA SASA NDIO HICHO NILICHOSEMA AWALI KAMA INAVYOONEKANA KWENYE ATTACHMENT
 

Attachments

  • Screenshot_20240218-233649_1.jpg
    178.9 KB · Views: 21
S23 series model zote walitumia snaodragon worldwide...S24 ultra wanatumia Snaodragon worldwide kasoro s24 vanilla na plus version
 
Na baadhi ya material ya iPhone wanauziwa na Samsung hawa jamaa sio mchezo nipo nao tangia 2018 wapo vizuri.
 
Your disclaimer is hell as shit

Mada yako imekaa kimihemko sana, you are truly android fan, kikubwa nikwambie punguza chuki na iOS,

I don't like iOS too lkn kwa mahitaji yangu nahitaji iOS, kwasabu android haitimizi, don't mention about latest brands as nishakua huko.

Apple ni mtakuja hata useme nn, guys are serious. Labda kama una surf na kudowload kwenye android.
 
Sijawahi kutumia samsung bado hawajanishawishi ,sawa na laini ya tigo sijawahi kutumia wala sina time nao..

Nipo google pixel kwa sasa.
Watu wa mkoani utawajua tu 😂 wao laini ya tigo ni kama mtandao wa ki-alien

Samsung ni mashine ila najichanga niipate ile S23 in the mean time ngoja niendelee kujitafuta huku kwa mchina
 
 
Wazee i phone inateleza sana yaani simu tamu adi raha.

Mimi ni fans wa IOS nyie wadau wa androids mtajijua wenyew
 
Redmi wanajitahidi, tena hasa kwenye software lkn hardware bado, zinadepreciate haraka sana, yaan the more unavyotumia ndo inazidi kuzolota.

Samsung ana balance hardware na software
sio kweli
 
Kuwa na S24 Ultra
*Utatumia Samsung DeX
*Utatumia feature ya "circle to search"
*Utapiga picha mwezi na utatokea vizuri huku umeng'aa kwa msaada wa AI
*Utapata Always on Display
*Utapata S Pen
*Utacheza heavy games smoothly kuliko unavyoweza kudhania
*Utatumia feature ya AI summaries
*Utapata features kibao

Huwezi sema matumizi ya flagship na low end ni sawa
 
Mbona ndio inajadiliwa hapa si tunajadili flagship za Samsung au?
 
Kukurekebisha founder wa iphone si tim cook, na tim cook kuwa shoga haku athiri ubora wa bidhaa za apple

For the record tim cook was hand picked kuongoza apple na steve jobs akiwa katika hali mbaya kitandani
Naona kachanganya kati ya founder na successor.
 
Wajuvi .Kwa bajeti ya mtu ya 330k anaweza pata simu gani nzuri ambayo atleast inaweza sukuma video game ya 1gb kushuka chini na pia camera nzuri? Kuna kakijanaa ka ndugu yangu kanataka simu kwa bajeti hiyo. Ila isiwe infnx
Ukitaka vitu vizuri kubali kuumia japo maramoja mfuko utoboke ila ukishalipia utafurahia hadi ukome.
 
Flashships ndio kitu gani wakuu ? mimi sielewi kitu.
Flagship ni ile toleo la simu ambalo linabeba jina la kampuni kwenye mauzo.

Yaani kwa mfano ukisikia Toyota, je ni magari gani ambayo ni brand ya Toyota yanalipa umaarufu hilo jina la kampuni? Magari kama Land cruiser, IST, Rav 4, crown, Harrier, etc.

So kwa Samsung wanasimu nyingi sana ila zipo zile model ya simu kama Galaxy S series zinafanya kampuni ipate heshima na brand kubakia sokoni.
 
Wewe simu unaitumia vipi productively? [emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…