MAONI: Kwenye battle ya flagships, hakuna brand inayoizidi Samsung, hata iPhone haishiki moto wa Samsung

MAONI: Kwenye battle ya flagships, hakuna brand inayoizidi Samsung, hata iPhone haishiki moto wa Samsung

Mm nilinunua sm note 20 kavu...hii simu weka mbali na watoto kwanza kiooo chake yaan ukiwa unatumia unasikia rahaaaa sasa njoo camera ni balaaa na chaji inakaa vizuri sana battery 4300 mAh, Ram 8gb, internal storage 256gb.Hii simu ni nzuri sana.Nilisha wahi tumia redme note 11 ni nzuri sana ila kwa samsung hapana acha niwape maua yao.
Note 20 Ultra sijui kwanini Samsung waliacha hizo mambo.
Note kama Note,tumehamia S24 Ultra😀😀😀ila bado naikumbuka Note 20 Ultra ipo kama Backup siku zote.
 
Hiyo namba sita ni ya muhimu sana japokuwa nina ugonjwa wa kununua simu zenye kuleta gumzo kwenye jamii hali ya uchumi inavyokuwa nzuri.

Ukitaka kulijua hilo kwamba watu hawazitumii simu kikamilifu, mtu akienda kununua simu anaangalia camera, storage na brand angalau aonekane wa bei ya juu kidogo Kwa ajili ya kujaza nyimbo na picha pamoja na asionekane mchovu Kwa kuwa na simu latest mengine hayahusu ila wachache sana wanazitumia simu kikamilifu
Ni matumizi yapi yanaonesha kuwa mtu anaitumia simu yake kikamilifu?

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Kila mmoja aishi ajuavyo mie kwa sasa nafikiria kuendelea kutumia oppo chinese versionbaada ya kuanza na hii reno 7 nikaona ufanisi wake siwazi hata kuhama
Umewakimbia Redmi mkuu?
Ulinifanya nizipende simu za redmi japo saiz natamani kushika flagship moja hata ya used tu.
 
Umewakimbia Redmi mkuu?
Ulinifanya nizipende simu za redmi japo saiz natamani kushika flagship moja hata ya used tu.
Nitabaki kua team xiaomi ila nazurura zura kwanza now niko oppo nataka niende china kwa huawei nikitokea apo narudi xiaom
 
Mm nilinunua sm note 20 kavu...hii simu weka mbali na watoto kwanza kiooo chake yaan ukiwa unatumia unasikia rahaaaa sasa njoo camera ni balaaa na chaji inakaa vizuri sana battery 4300 mAh, Ram 8gb, internal storage 256gb.Hii simu ni nzuri sana.Nilisha wahi tumia redme note 11 ni nzuri sana ila kwa samsung hapana acha niwape maua yao.
Nafikiria kuzama huko next month. Ni bei gani ulichukua?
 
Nimeikubali Samsung s24 , hawa jamaa ni hatari Tupa kule iPhone 15 , nilipanga kununua iPhone 16 mwez wa kumi nafkr zitakuwa zimetoka , nimeona unyama wa Samsung s24 , naenda kuchukua huyu mkali , umbo lake Tu linakera ila content ni balaa
 
Samsung wako vzr sana sababu wameweza kupata balance kati ya uwezo wa software na hardware, kitu ambacho kwa wengine bado.

Brands nyingine utakuta hardware nzr ila software chenga, and vice versa
Mimi nimekuelewa sana kwani natumia zote Iphone na samsung
 
Sony Xperia its the best kwa upande wangu. Sijajua wajapan wanakwama wapi kwenye marketing. Kampuni nyingi tunazozisifia za sinu wana tumia camera sensors za Sony..ila sony wenyewe sokoni wanachaowa vibaya mno na kina samsung
 
Shida kubwa ni kubalance hardware na software. Unaweza tengeneza hardware nzr ila software chenga.

Nina sony hapa juzi nlikua napiga videocall whatsapp ghafla camera ikakataa kurespond, baadae ikawa nikiwasha torch inakataa inasema camera is on, confusions tu zisizoeleweka mpaka nikarestart simu
 
Back
Top Bottom