MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Wakuu habari.
Kwanza nichukue fursa hii kuwapongeza wanawake wote walio kwenye ujasiriamali na biashara kwa ujumla. Uchapakazi wao umetukuka. Ila pia Ninaandika post hii nikiwa na masikitiko makubwa sana kwa mama zetu na dada zetu ambao ni wajasiriamali na wafanyabiashara hasa wa jijini Dar. Kina mama hawa wengi wao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii katika mazingira magumu yanayokatisha tamaa ila kwa uvumilivu walio nao huendelea kusonga mbele. Wengi wao hutengeneza faida kwenye biashara zao hata kama sio faida kubwa. Masikitiko yangu huanza wakati wa matumizi ya hizo pesa zilizopatikana. Kina mama wa Dar wengi huitumia faida yao iliyopatikana kwenye kitu kinaitwa "shughuli". Hizi ni tafrija zisizokuwa na ulazima sana lakini hugharimu. Kwamfano kuba sherehe nyingi za birthday, mtoto kufikisha siku 40 nk. Hizi siku zingeweza kusherehekewa hata kwa kinywa pepsi mojamoja lakini utakuta hadi sare hushonwa kwa ajili ya shughuli pamoja na gharama za muziki, vinywaji, vyakula nk. Mara baada ya hizi shughuli kuna baadhi ya kina mama hupoteza hadi mitaji yao.
Wito wangu kina mama naomba tafadhalini tuwe macho na matumizi tunayoyafanya. Mambo yasiyo ya lazima tuyaache kama sio kupunguza. Pia tumieni faida sio mtaji.