Maoni, Mawazo & Ushauri kuhusu biashara ya Rasta na Weaving

Maoni, Mawazo & Ushauri kuhusu biashara ya Rasta na Weaving

Kweli hata biashara haujawahi kufanya Bali unataka kuleta akili uchwara za kiccm,umesema dazeni ni 12000tsh na zipo piece 12,na kwa piece 1 unauza 1600tsh,sasa hiyo faida ya 19200tsh inatoka wapi!?
Wakati ukifanya 1600×12=19200tsh,kumbuka umenunua 12000tsh kwahiyo hapo ni 19200-12000=7200tsh
7200tsh hapo hatujajua inachukua muda gani kuuza ili tuweze kujua faida halisi inapatikana vipi
Biashara ya saluni inalipa sana. Mfano dazeni ya nywele za bandia ni sh.12000 tu (kwa bei ya jumla jumla) ambapo kwa reja reja kila pic moja inauzwa sh.1600 tu.

Hivyo ukiwa na dazeni 100 na kila dazeni ina pic 12 ili itimie dazeni, hivyo,

Kila pic moja kama utaiuza sh.1600 utapata faida ya sh.19,200 (yaani 12 zidisha kwa sh.1600)

Hivyo, chukua faida ya dazeni moja ambayo ni sh. 19,200 zidisha kwa dazeni 100 utapata sh.1,920,000. Hata ukifanikiwa kumaliza hizo dazeni ndani ya mda mfupi hiyo hela itakuwa yako yaani faida.

KUMBUKA: Hapo unahitaji mtaji wa sh.1,200,000 tu. Pia biashara hii hakikisha huna Tabia za kutamani tamani wanawake maana faida hutaiona!

Kazi ni kwenu sasa!

Sent by Diaspora
 
Unazoziona kariakoo tunanunua China na South Africa...nenda tuu kkoo changanya Wigi kadhaa na weaving baadhi zingine wananunua Uganda hapo hizo Brazilian.. Nunua lolo rangi nyeusi na Purple (Papo),Jialong ndefu na Fupi ndefu chukua rangi 99j,# 1 na colour 4, lovely lady fupi rangi zote..HP ukipata colour zote changanya chache chache,Wigi za watoto na spray carton hata Mbili za Wigi nazo utauza nunua midoli ya kuwekea Wigi kkoo ipo angalia ukubwa wa fremu yako ndio ununue mikubwa na midogo ujanja mwingine utaupata ukiendelea kufanya hiyo biashara..
Nashida na wewe mkuu nakupataje?
 
Back
Top Bottom