ni kwamba kwa sehemu kubwa wasanii walishirikiana kuishinikiza serikali kutunga sheria ya hakimiliki na hakishiriki. World intellectual property organization (wipo) ilishiriki kuisukuma hoja ya kuundwa sheria husika.
Faida za kuwepo kwa sheria tajwa ni pamoja na kupitishwa na kutekelezwa kwa kanuzi za ukusanyaji wa mirabaha ya matumizi ya kazi za sanaa. Hapo awali hadi sasa zoezi la kusajili kazi za wasanii linaendelea ili kuweza kusimamia mgawanyo wa haki za wasanii kwa mujibu wa sheria. Pia sheria imeendelea kupunguza uharamia wa kazi za wasanii ingawa kuanzia mwaka 2009 serikali kupitia waziri nagu (viwanda na biashara) ilianza kujiweka mbali na utekelezaji wa sheria yenyewe hali iliyopelekea wizi kushamiri upya na sasa kupitishwa sheria ya utoaji wa stika maalumu kwa kazi za sanaa unaoendeshwa na tra ambapo msanii ameminywa haki zake na mapato kugawanywa baina ya msambazaji na serikali pekee. Awali wasimamizi wa sheria hii cosota waliandaa kanuni tangu mwaka 2007 inayohusu matumizi ya stika maalumu na namna mapato yake yatakavyogawanywa. Ila waziri hakuipitisha kanuni hiyo na bahati mbaya hakukuwepo na juhudi za dhati wizarani kuiridhia hiyo kanuni hadi iliponyakuliwa na wizara ya fedha na kuletwa rasmi bungeni ili ianze kutumika 2013/2014.
Tukirejea kwenye hoja ya katiba mpya.
Wasanii waliona kuna mapengo ya wazi kabisa kuhusu utamaduni kutamkwa kama ni mojawapo ya utambulisho wa mtanzania na nchi ulimwenguni. Na pia tulipendekea kuondoshwa ibara inayotamka matumizi ya kiingereza kwani katiba imeshatamka kwamba lugha ya taifa ni kiswahili. Na yamekuja mapendekezo namna ya kusimamia, kulinda na kuendeleza kiswahili ili kukipa chapuo ulimwengun. Kuna mapendekezo kuhusu wageni na wawekezaji kuweza kuwa proofed na proficiency ya kiswahili wanapokuwa ktk harakati zao za uwekezaji kwani inaonesha kwamba uwekezaji wa kwenye ardhi huko vijijini kumekuwa na sintofahamu kubwa kutokana na barrier ya lugha hasa kwa watanzania walioko huko.
Kwenye mahakama, sote tunafahamu kwamba lugha ya kiingereza imekuwa ikitumika kurekodi daawa (kesi) na mara nyingine nakala za hukumu zinazoandikwa kwa lugha hiyo zimekuwa zinawanyima haki watanzania waliohukumiwa ama walio na nia ya kukata rufaa hivyo tumeshauri lugha ya kiswahili itumike kwenye vyombo vya kutoa haki.
Kuna lingine ambalo ninyi wanasiasa hamkulizungumzia katu. Nalo ni la uhifadhi na ulinzi wa katiba. Viongozi wakuu wa nchi wanapoapa kulinda katiba imeonekana kwamba kuna haja ya kuwepo na chombo huru kitakachosimamia hilo. Tumeshuhudia katiba imevunjwa mara kadhaa ambapo 2010 baada ya uchaguzi mkuu, rais wa zanzibar aliapishwa huku akiwa hajakoma kuwa makamu wa rais wa muungano. Hivyo uwepo wa chombo huru cha kuhifandi na kulinda katiba kutatoa nafasi kwa viongozi kuwajibika zaidi wanapotekeleza majukumu yao bila kuvunja katiba. Chombo hicho kipewe uwezo kisheria kumhoji na kuchungua madai yoyote ua uvunjwaji ama uchezewaji wa katiba na kikiridhika kuwa kuna makosa, kiandae mashtaka ya mhusika na kupeleka bungeni ambapo spika hatokuwa na veto ya kuzuia kujadiliwa hoja hiyo na taratibu za kumshati na kumchunguza mhusika kuendelea hadi maamuzi ya haki kutolewa bungeni.
Wasanii pia waliona kuna haja ya kuwa na serikali moja kwani, uwepo wa serikali mbili ama tatu hakuepuki matumizi ,akubwa ya kuendesha serikali hizo. Pia kuwepo na migogoro ya kimamlaka hakujaepukika tangu mwanzo hadi sasa zanzibar imeshapiga hatua ndefu kuelekea dola kamili. Hivyo badala ya kukwepa tatizo na kufufua serikali ya tanganyika, basi iwezekane tukaudumisha muungano kwa kuondoa mamlaka za serikali mbili ama tatu na kuweka serikali moja. Bunge la seneti litakuwa bunge la juu ambapo bunge la congress litakuwa la chini. Katiba hii itawezesha kutoa mwanya kwa nchi zingine kujiunga na jamhuri ya muungano kwa kuridhia kwenye mabunge yao katiba hii na kujiunga. Jeshi liwe moja. Kuhusu mahakama wasanii walishauri iwe ktk ngazi tatu.
- mahakama ya juu,
- mahakama ya rufaa,
- mahakama ya jimbo na mwanzo.
kuhusu sarafu iwe moja na usimamizi wake uwe kama ifuatavyo.
- benki kuu (muungano wa benki kuu za majimbo)
- benki za majimbo
naamini ktk dodoso kuna mengi yatakayoelezwa na ninaahidi kuyaleta hapa endapo yatakuwa tayari ktk mfumo rasmi.
#justsaying