DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Najikita moja kwa moja kwenye mada husika. Naiomba serikali iboreshe mfumo wa ukataji tiketi kwenye tren yetu ya mwendokasi SGR. Nalisema hili kwa sababu nimeshuhudia zaidi ya mara moja mfumo unaonesha tiketi zimeisha (nafasi zimejaa) lakini ukisema vizuri na wahudumu unapata nafasi. Hii nahisi inaweza kuleta mwanya wa wahudumu wasio wazalendo kupiga (kwa lugha isiyo ramsi). Nachelea watu wakanunua risiti za mkononi kwa gharama (bei) ya juu zaidi ya kawaida, hivyo ikawanufaisha wachache wasiopenda maendeleo ya nchi yetu.
Natoa maono haya kama mwananchi mpenda maendeleo, ambaye ninanufaika kwa kiasi kikubwa na uwepo wa SGR. Kwa hili naipongeza serikali na pia Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
#kaziiendelee